Mwanaharakati wa Haki za binadamu na mwanasheria wa masuala ya Maliasili Mr. Amani Mustafa Mhinda, ambaye pia ni Mkurugenzi wa asasi ya kijamii ya HAKIMADINI,inayoshughulika na haki za binadamu katika maeneo ya machimbo ya madini akiwa anawahutubia wanaharakati nje ya jengo ampako mkutano wa barrick ulifanyika.
bahadhi ya wanaharakati wakiwa na mabango yao nje ya jengo ambalo mkutano wa barrick ulifanyika.
wanaharakati na wahandamanaji waliokuwa nje ya jengo ambalo mkutano wa Baarrick ulifanyika.

Mkutano wa mwaka huu wa Barrick Gold Mine uliofanyika Toronto Nchini Canada May 3, 2012, ulimzuia Mwanaharakati wa Haki za binadamu na mwanasheria wa masuala ya Maliasili Mr. Amani Mustafa Mhinda, ambaye pia ni Mkurugenzi wa asasi ya kijamii ya HAKIMADINI,inayoshughulika na haki za binadamu katika maeneo ya machimbo ya madini.

Mhinda alikuwa amedhamiria kueleza wahudhuriaji wa Mkutano huo kuhusu umuhimu wa kujenga uwezo wa wachimbaji wadogo na jamii zinazoishi katika maeneo ya machimbo, ili ziweze kunufaika na rasilimali ya madini ya Tanzania, pamoja na kulinda na kutetea haki zao, ambayo pia ni agenda kuu ya HAKIMADINI yenye makao yake makuu mjini Arusha.

Pamoja na kuwa na ajenda hiyo, Barrick Gold na uongozi wake walimzuia kuingia katika eneo la mkutano huo.

Akinukuliwa na gazeti moja la kitaifa la Canada liitwalo The Canadian, Mhinda alieleza uhalali wake wa kuhudhuria mkutano huu huku akinukuu matukio ya uvunjwaji wa haki za binadamu yanayofanywa na makampuni ya uchimbaji

“Kama shirika lisilo la kiserikali la kitanzania na wananchi wa Tanzania, tunataka kuona mauaji na uvunjwaji wa haki za binadamu unaohusishwa na makampuni ya uchimbaji madini ya Canada yanamalizwa. Niko hapa kumwakilisha watanzania wengi ambao ni wahanga wa mgodi huu pamoja na Mama Otaigo, aliyefariki mwezi wa nne kwa kunywa maji yenye sumu yaliyopo karibu na Mgodi wa North Mara”. Amani alisema

Mwanaharakati huyo pamoja na wanaharakati wengine wa masuala ya haki za binadamu walinyimwa kuzungumza kuhusu matendo ya kinyanyasaji yanayofanyika kwenye maeneo ya machimbo ya madini nchini Tanzania katika mkutano Mkuu wa Mwaka wa Barrick Gold mine.

Hatua hiyo ya kampuni ya Barrick Gold Mine kuwazuia wanaharakati wa Tanzania na kuwaruhusu wenzao wa nchi kama Papua New Guines na Chile kuliushangaza umati wa waalikwa kwenye mkutano huo.

Mhinda alishutumu hatua iliyochukuliwa na Barick Gold ya kumzuia kuingia katika mkutano huo kama “juhudi za wazi za kuficha uvunjwaji wa haki za binadamu unaofanywa na makampuni ya uchimbaji na wawekezaji wengine kwa jamii za kitanzania".

Pamoja na kufungiwa kuingia katika mkutano huo, Amani na wanaharakati wengine walipata nafasi ya kuelezea habari zao kwa maelfu ya watu waliokusanyika nje ya eneo la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Barrick kwa ajili ya kupinga unyanyasaji unaofanywa na kampuni ya Barrick Gold ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya uchimbaji dhahabu duniani, iliyoanzishwa na kusimamiwa na Peter Munk.

Miongoni mwa wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo ni pamoja na Waziri mkuu wa zamani wa Canada. Barick hupata fedha za serikali na misaada ya kidiplomasia. Makao makuu ya barrack yapo Toronto, Canada, wakati Africa Barrick, ni kampuni ya Uingereza ambayo humilikiwa kwa 70% na Barrick Gold

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2012

    BRAVOOOOOOOOOOOO! Mr Mhinda. Mapambano katika ukombozi wa wanyonge Udumu!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2012

    Shareholders meeting huwa ni kwa ajili ya shareholders peke yao. So ushauri wa bure kwa Bwana Mhinda ni kununua shares za Barrick then hawataweza kukuzuaia kuhudhuria huo mkutano. Wanaharakati wengi huwa wanatumia huo mwanya na kununua hata share moja ili kwenda kutoa duku duku lao kwenye hiyo mikutano.

    Marekani kuna mama mmoja mwanaharakati anaitwa Evelyn Y. Davis. Huyu mama anahudhuria karibia mikutano 40 kwa mwaka na kazi yake ni kwenda kutoa dukuduku lake kuhusu haya makampuni makubwa.

    Australia mwanaharakati wao mkubwa ni Jack Tilburn. Ameandika kitabu kizuri sana kinaitwa The Corporate Terminator. Jamaa ni mwiba kwa kampuni kubwa ya madini ya BHP Billiton.

    Shukrani.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2012

    Ili kupata chetu ktk Barrick Gold:

    1.Wawekezaji Viongozi wa Barrick wanajulikana kwa majina kama huyo Peter Munk na Maaafisa wawakilishi wake ktk migodi yake hapa Tanzania, Watu wanajipanga Watu wa kada mbali mbali nchini anawaalika wanawekwa kiti moto warekebishe mwenendo wa Maafisa wake Migodini.

    2.Barrick African Gold, wanazo Hisa ktk DSE (Soko la Hisa la Dar)tena cha ajabu waliweka Toleo la Awali la Hadharani 'Initial Public Offering' (IPO) mwaka 2010 lakini ni kuwa sisi Watanzania wenyewe hatukuzinchangamkia Hisa hizo matokeo yake wakazi peleka London Stock Exchange (LSE) kwa ajili ya 'CROSS LISTING' yaani kuzi orodhesha kwa mara ya pili ambapo huko ndio watafaidika na hisa hizo zaidi kuliko wale wa awali.

    Hivyo harakati za Bwana Amani Mustafa Mhinda juu ya Madini,zilihitaji sana afuate taratibu kwa ajili ya kuwarekebisha mwenendo wa Wawekezaji kupitia Kanuni, Halafu kwa suala la manufaa kwa Umma ilibidi afanye uhamasishaji watu wa kawaida Watanzania(Public) wanunue hisa Barrick huku akishirikiana na DSE(Soko la Hisa Dar), CMSA(Mamlaka ya Dhamana na Mitaji) pamoja na TMRC (Shirika la Dhamana za Kifedha) lipo chini ya Ndg. Rished Bade.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2012

    Bwana Amani Mustafa Mhinda,

    Panapo jiri masuala ya Ubepari agenda kuu ni umiliki na nafasi yaani who is who.

    Unapowakuta Mabepari mezani wanazungumzia chakula chao njia ya busara ni kuungana nao hata kama ni kimtindo na sio kutumia Harakati na Siasa kuwaingia,,,wanakuwa hawatakuelewa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...