Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akifyeka maua kuyaweka sawa katika moja ya bustani katika Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo leo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Ofisi ya Makamu wa Rais inayozitaka taasisi za Umma na Serikali kuwa na siku maalum ya usafi wa mazingira katika maeneo yao. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa imejiwekea utaratibu wa kufanya usafi kila siku ya alhamisi ya wiki ambapo kila mtumishi anashiriki katika jukumu hilo. Usafi huo huanza saa mbili hadi saa tatu asubuhi. Miongoni mwa kazi zinazofanyika ni pamoja kufagia, kufyeka, uzoaji wa taka ngumu, na usafi wa jumla katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akizungumza na watumishi wote katika ofisi yake leo ambapo waliwekeana utaratibu wa kufanya usafi kila siku ya Alhamisi ya wiki.
Kutoka kushoto ni Afisa Elimu Taalum Mkoa Domician Chose na Kaimu Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Frank Jailos Mateny wakijumuika kwenye usafi huo leo.
Baadhi ya watumishi wakijumuika kwenye usafi huo leo
Zoezi la usafi likiwa linaendelea
Charles Daudi dereva wa Mkuu wa Mkoa akijumuika kwenye usafi huo leo








anastahili pongezi Mh.mkuu wa mkoa maeneo mengi nchini ni machafu hasa jiji letu . wahusika hawaoni hili la Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ? natumaini tukijipanga linawezekana..www.rundugai.blospot.com
ReplyDeleteusafi na suti , hao jamaa wana geresha tu.
ReplyDeleteJamani hebu ondoeni utani......hao vingunge wanafyeka majani wakiwa ndani ya suti......!!!!nani anamdanganya nani....!
ReplyDeleteAcheni kuchezea akili zetu na kufanya mambo kisiasa. Kufyeka na suti? Si mpange siku mje na mavazi sahihi. Haya mambo ya ajabu
ReplyDeleteNi safi kabisa kuweka utaratibu kama huu wa kufanya usafi. Lakini ni muhimu sana, OFISI ziwe na mabafu. Pia zinunue mavazi maalum ya kufanyia usafi, ili wafanyakazi waende tu na nguo zao nzuri, wakishafika ofisini, wabadili nguo zao hizo, wavae nguo za usafi. Baada ya kumaliza kufanya usafi, waoge, kisha wavae nguo zao nzuri za ofisini. Sasa hili kufanikisha hili, inatakiwa usafi ufanyike kwa awamu: Asubuhi, baada ya lunch, na baada ya kazi. Hapa mabafu machache yatatosha. Pia ofisi zote hazitafungwa kwa ajili ya usafi.
ReplyDeletejamani jamani hawa watu wanafikiri sisi wajinga nini???wanakata majani wamevaa suti na viatu virefu..wanaonekana kabisa hawako serious na wanachokifanya
ReplyDeleteMsiwafanye maofisa kama wako jeshini ajirini makampuni ya usafi katika majengo na kusimamia kwa karibu zaidi. Hii pia itawapa fursa wasio na ajira kuajiriwa.
ReplyDeleteMusiendeshe nchi kama hivi mukawafanya wafanyakazi kuichukia siku hii ya kila alhamisi na baadae kuja migogoro isiyokuwa ya lazima.
Sutiiiiiiiiiiiii!
ReplyDeleteSutiiiiiiiiiiiii!
Sutiiiiiiiiiiiii!
Sutiiiiiiiiiiiii!
Sutiiiiiiiiiiiii!
Sutiiiiiiiiiiiii!
Sutiiiiiiiiiiiii!
Sutiiiiiiiiiiiii!
Sutiiiiiiiiiiiii!
Sutiiiiiiiiiiiii!
Sutiiiiiiiiiiiii!
Sutiiiiiiiiiiiii!
Sutiiiiiiiiiiiii!
Sutiiiiiiiiiiiii!
TUSIDANGANYANE KUFYEKA NA SUTI,HUO NI UTANI!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteHii nayo ipo kwenye job description? Naona maagizo ya Mhe. ni kinyume na PPP,hizo kazi zinapaswa kufanywa na sekta binafsi.
ReplyDeleteSina shaka wengi ya hawa watumishi watakuwa wanajiuliza 'ni lini huyu mama ataondolewa hapa?anatufanyisha kazi na suti zetu?'
ReplyDeleteAkuna usafi hapo, hiyo ni kwa ajili ya kupiga picha tu na kuwadanganya watanzania kama kawaida yao, Usafi na Suti na Skuna wapi na wapi? Tujifunze jamani kuwa serious.
ReplyDeleteusafi ni kitu muhimu ktk mazingira yetu, sasa hao maofisa hawakujua kama wanakuja kufanya usafi, suti za nini tena? wangevaa traki suti lol
ReplyDeleteIt seems convincing that "the Vigogoz" are willing to lead by examples! I wonder why the cleaning is at their office environment only! Is it because they have failed to hold the cleaners responsible!!!!!!!! Is she campaigning for 2015? was this for media show?
ReplyDeleteThey should have cleaned the public places (along the streets, market places, bus stations, hospitals, etc.) of which I believe that is where we have challenges. Let us be serious with what we do as leaders and not foul the public.
Hivi Sera ya usafi Tanzania inasemaje (kama ipo)? Kwa nini halimashauri wasipitishe sheria inayombana kila mtanzania kuhakikisha usafi katika eneo lake mfano kila mwenye biashara ahusike kusimamia usafi wa eneo la biashara yake? Hebu angalia kariakoo kulivyojaa taka inayozalishwa maduka na hakuna anayejali!!! Kwenye Dalaldala kuwe na debe la taka "dustbin" n.k. Tena ikiwa watatozwa faini ikiwa eno lako litakutwa chafu, naamini kila mtu atakuwa polisi wa mwenzake. Makusanyo ya faini hizo yatatumika kununulia vifaa vya kukusanyia, kusafirisha/kuhamisha na kuteketeza taka kadiri inavyofaa! Inabidi tuamke jamani!!!!!!!!!!!
mbona mnamshikia bango mnene Mateni kufyeka akiwa amevaa Suti, Hamjamuona RC wake mbona na yeye anasawazisha maua akiwa na Vazi la Kitaifa, Wabongo bana
ReplyDeleteusafi na suti na kokoko wapi na wapi...kweli bongo tambarare kila kitu siasa.
ReplyDeleteHongera mama Manyanya kwa kuonyesha njia. Lengo lako tumelifahamu ni kuonyesha uwajibikaji kwa viongozi kwa kuonyesha mfano wao wenyewe kwa kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu ya kitaifa. Tuliona ulianza mitaani katika Mji wenu wa Sumbawanga kuwahamasisha wananchi, sasa umerudi katika Ofisi yako. Hao wanaosema kinegative na kawaida kwa waswahili
ReplyDeleteHongera mama tulikuona ulianzia mitaani kuhamasisha wananchi kwenye usafi sasa upo Ofisini kwako. Hao wanaosema negative ni kawaida ya wabongo kusema
ReplyDelete