nilikuwa ni mmojawapo wa abiria tuliopanda Ndege ya Auric air toka Mwanza kwenda Bukoba saa 05.45 kwa flight Na. 104 tukiwa abiria takriban 10, tuliondoka salama Mwanza na Pilot alitutangazia kwamba tutapitia kisiwa cha Rubondo ili kuchukua abiria wawili, tulitua salama Rubondo mnamo saa 12 jioni ina kuwachukua abiria na kabla ya kuanza safari Pilot alitutangazia tena kwamba tutachelewa kufika Bukoba ila atajitahidi kuongeza mwendo ili tufike mapema.
Mmojawapo wa abiria mwenzetu alitoa angalizo kwamba mbona muda umekwenda sana si tutafika Bukoba giza na airport ya Bukoba anavyoijua haina taa… hakuna aliyemjibu yaani kwa sisi abiria maana wengi nadhani tulikuwa wageni na uwanja ule, hivyo pilot alianza safari, tulienda vizuri tu ila tulipoanza kukaribia Bukoba kweli giza lilishaanza kuingia, na hatukupewa tangazo lolote la kujiandaa na kutua badala yake tulianza kushuka kama kawaida ila tulishangaa kuona pilot haongei chochote nasisi na tunazidi kushuka chini baada ya hapo kilichotokea siwezi kusema ila tulichosikia baada ya kuzunguka sana ni kishindo kikubwa kwamba tumefika ardhini na tukakwama kwenye matope makubwa yaani tulitua out of run way na Pilot alijitahidi sana kuikwamua ndege kwenye matope bila mafanikio, Ni mungu tu alitunusuru… kupata ajali mbaya sana
Baada ya purukushani kubwa sana Pilot alifungua mlango akatoka nje kisha akarudi ndani akatwambia mungu ametusaidia tuko salama, baada ya dakika kadhaa tuliona pikipiki ikija kwa kasi pale tulipokuwa toka pale airport hapo abiria tunagombania kutoka kwenye ndege, akaja mtu akatuuliza tuko salama… nadhani pilot ndo alimjibu kwa kweli ni ngumu kusimulia kwa kirefu kilichotokea. baada ya muda zilianza kuja gari nyingi toka airport kwa ajili labda ya kutuokoa au vinginevyo kwani hakuna gari la fire lililofika sehemu ile ya tukio,
badala yake ni wafanyakazi wa TAA walikuwa wanawasiliana na Mwanza wanawalalamikia kwa nini wameruhusu ndege ije bukoba usiku huku wakijua Bukoba hakuna taa airport! Na maneno mengi ya kuwalalamikia kwamba ni Tabia ya Auric air kujiamulia wanavyotaka… akawaambia kabisa KWA NINI MNATAKA KUUA WATU ONA SASA NDEGE IMEANGUKA…..
Inasikitisha sana kwa taarifa tulizokuwa nazo ni kwamba kiwanja cha Bukoba kimefanyiwa ukarabati, sasa iweje kiwanja hakina taa, pia hakuna mawasiliano na mwanza kwamba kuna ndege inakuja etc… kwa kweli hali haikuwa nzuri na ndugu na jamaa zetu waliokuwa wametusubiri airport ni mashahidi waliona jinsi pilot alivyohangaika na walishajua tunakufa walikuwa wanasubiri kuona ndege itaangukia wapi waje waokote
kitakachobaki.
Ninachosikitika baada yahaya yote kutokea Asante mungu hatukujeruhiwa licha ya majeraha madogo madogo tuliopata, hakuna Staff yeyote wa Auric aliyekuja hata kutwambia pole badala yake ni wafanayakazi
wa TAA nadhani ndio walitupakia kwenye gari na kutuleta airport wakatwambia tusubiri mizigo wakaileta wakaishia zao, hivi kweli huu ndio utaratibu wa airlines……….. au kwa sababu ni bukoba????
Ninaandika haya kwa masikitiko makubwa sana na imebidi niandike kwa maana ningekufa hakuna ambaye angefahamu haya…. Nimeambatanisha picha japo ni giza nilifanikiwa kuipiga baada ya kupata fahamu, tunaiomba serikali na vyombo husika tupatiwe taarifa kamili ya tukio hili na kibaya inaonekana imefichwa kwani hakuna chombo chochote cha habari kilichoripoti licha ya wakazi wa bukoba kuona hili tukio baya sana la kuhatarisha maisha ya watu lakini ingekuwa tukio lingine lingesambaa tena kwa breaking news!!!!!!!!!!!!!!
Kama airport ya Bukoba haina kiwango ni bora ifungwe tujue hakuna usafiri wa anga…. Pia tunaomba wahusika wawajibishwe mara moja na hasa wafanyakazi wa TAA, Auric Mwanza na mtu au kampuni yeyote iliyohusika na kuruhusu ndege hii 104 kupaaa na kuzua safari ya kwenda Rubondo bila mpangilio kama inavyotakiwa kwani tungekwenda moja kwa moja Bukoba kama inavyoonyesha kwenye ticket tusingechelewa kufika Bukoba ambako inasemekana inajulikana ndege hazitui Bukoba zaidi ya saa 12
jioni, hapa mzembe ajulikane na achukuliwe hatua.
Nimeandika haya kwa masikitiko makubwa sana najua na wenzangu tuliohusika mtakuwa mashahidi wangu katika hili.
Serikali,Watanzania, Wawekezaji na wafanyabiashara tujali maisha ya wengine, HAIWEZEKANI MTALII MMOJA SIJUI ANALIPA KIASI GANI AKAWASHAWISHI AFUATWE RUBONDO!!!! hii kamppuni ya Auric inachezea maisha ya watanzania na kwa maelezo ya mfanyakazi wa TAA Bukoba inaonekana ni tabia yao maana alisema sio mara ya kwanza tunawaambia msilete ndege usiku hamsikii.
Kipekee tunawapongeza sana Precision air kwa huduma nzuri kwa sisi wakazi wa Kanda ya ziwa, na tetesi ni kwamba wao wamesitisha trip za bukoba kutokana na hali ya uwanja, tunaiomba serikali kulichunguzana kulifanyia kazi suala hili kwa umakini na watanzania wapate taarifa nini kimetekelezwa,
Wasalaam!


Pole sana kaka na abiria wote mlionusurika,wahusika nafikiri watachukua hatua madhubuti kwa waliohusika na uzembe huu!
ReplyDeletekwanza nikupe pole wewe uliyetuletea hii habari.. Mimi natokea Kagera, nimepita saana bkb ni kweli ka uwanja kamechoka na nafikiri tatizo sio airline, tatizo ni serikali zetu zisizokuwa na maana.
ReplyDeleteUsalama wa airport unatakiwa kukaguliwa na serikali na hivyo kutoa ok kama unaweza kutumika au hapana. Inatia sana tena saaana hasira. Hata mimi mwaka 2008 nilienda na precision air, ila ilikuwa ni kuomba kama tungevuka ziwa make hakuna instructions zozote. Mizigo imezagaa zagaa kila mahara kwenye ndege.
Mungu tu ndo anatulinda, pole sana
Kwanza pole na hayo yaliyokukuta. Tunashukuru umepona kuhadithia. Pili, wewe ni mlipa kodi kwa mantiki hiyo wewe ndio mwenye huo uwanja wa Bukoba, ni mali yako. Waulize waheshimiwa kuanzia mzee wa nyumba kumi, diwani, mbunge na raisi inakuaje unalipa kodi alaf uwanja unakarabatiwa bila kuweka taa? Na kama wakisema taa zipo tatizo umeme, waulize kwani huo umeme si wa Tanesco ambalo ni mali yako (umma), iweje wasilete umeme Bukoba? Kwani huko hamna wenyenchi? Sasa ni wakati wa kuuliza maswali magumu.
ReplyDeletePoleni sana, abiria wote na tunamshukuru Mungu na tutaendela kumshukuru kwa kuwanusuru.
ReplyDeleteKabla sijaenda mbali, mimi ni abiria mzoefu na usafiri wa anga (kitaifa na kimataifa) na najua nitakachokiongea
Huu ni uzembe wa hali ya juu kabisa na tunaomba wote waliohusika wachukuliwe hatua kali. kwa haraka nashauri hili shirika linyanganywe leseni na rubani afungiwe maisha kurusha ndege. Kwanini? Huu usafiri wa anga unahitaji umakini wa hali ya juu na sio ubabaishaji kama huu. Kama shirika na Rubani watafikia kujiendesha na kurusha ndege kama madereva wa vipanya basi hii ni hatari kubwa. Kwa kifupi sekta ya anga imevamiwa nchini.
Pia naomba abiria wote tangazeni uzembe huu kwa nguvu zote na vyombo vya habari viandike kwa nguvu ili abiria wajue nini kinaendelea kwenye shirika ili na marubani wake wababishaji.
Lakini kama ni kawaida yao, jamani kwanini mnapanda ndege za hilo shirika?? Tunajua haya mashirika mengine yanaingia kirushwa rushwa ndio maana hawaogopi na kujali roho za watu sasa mi nashauri njia ni moja tu, nayo ni kutopanda ndege zao kabisa ili wajue umuhimu wa roho za watu. Heri kupanda mabasi ingawa na yenyewe sio salama kwa namna hiyo.
Naomba nieleweke, natoa maoni based kwenye tukio na sio mpinzani wao wa kibiashara, maana nchi yetu kuna tabia ukiongea ukweli au kutoa maoni yako haukawii kusikia umetumwa au una masilahi binafsi. sijatumwa wala sina masilahi binafsi, watu wasusie shirika hili na hao marubani wao wababishaji.Nashauri pia hawa marubani waliohusika, wakaombe kazi ya kupiga debe kweny vipanya maana hawastahili hata kuwa madereva wa vipanya hivyo.
Mwisho ndugu mdau, tunaomba majina ya marubani hao ili ijulikane ni watu hatari kazini na kupanda ndege zao ni hatari pia. Inaonekana sasa tunataka kuzoesha watanzania ajali za anga.
Poleni sana abiria mlionusurika na Mungu ashukuriwe.
Ni mimi mdau nilyefedheheshwa na uzembe wa huu. Auric kitu gani bwana?? Fungieni hawa.
Nashukuru kwa hizi taarifa,nikiwa nami ni mmoja wa wazawa wa mkoa wa kagera.
ReplyDeleteMimi kwetu ni karibu sana na uwanja wa ndege,lakini inasikitisha kuona kazi inayofanyika pale ili kuboresha uwanja ni zero.
Kazi kubwa ya kupasua miamba halafu uwanja hauna lami na kazi hiyo imechukuwa miaka hivi sasa.
Tunaomba wahusika watembelee huo uwanja mimi naamini kuwa kuna mambo ambayo si ya kawaida yaani niubadhirifu mtupu.
Nchi hii ni yetu na haya tunayaona na yanatuumiza kwani hizi nikodi zetu zinachezewa.
Aisee poleni sana na Mungu ni mwema sana amewanusuru maana navojua airport ya bukoba ipo close na ziwa mgeweza hata kutua ziwani na ndo kwisha. Serikali inatakiwa ifuatilie hili jambo tunahitaji usafiri wa uhakika bukoba na hata karagwe sikujua kama precision nao wamesitisha huduma so sad. Hongereni kwa kusalimika Mungu azidi kuwalinda
ReplyDeleteJamani poleni sana sana,,Ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa mmesalimika,,
ReplyDeleteKuhusu maswala ya Bukoba,,Mimi huwa nasema ni kama sio part ya Tanzania,,Bora mngemuachia Idd Amin ikawa ya Uganda,pengine waingeshughulikia huwo mkoa,na sasa hivi ungekuwa mbali,,Kusema ule ukweli,,Bukoba imesahaulika kwa kila kitu,,kuanzia uhuru,kuzama meli mpaka kesho,,Tanzania haina habari na mkoa huwo,,
Muhaya wa Canada
Duh poleni sana...GOD MUST BE CRAZY!
ReplyDeletepoleni sana wote mlionusurika na ajali hiyo.
ReplyDeleteila napenda kutoa angalizo, uwanja unapokarabatiwa haimaanishi ni lazima uwekwe taa.
pili ni kazi ya rubani na wahusika wa ndege hiyo kujua kwamba airport anayokwenda kama kuna taa na kama hakuna taa night inaanza saa ngapi!!!
Pole sana ndg yangu kwanza tushukuru Mungu umepona, ila kusema ukweli stori inatakiwa kuwa front page ya magazeti ya nyumbani ili ku-raise awareness na uzembe kama huu.
ReplyDeleteNaungana kabisa na mdau mmoja hapo juu kwamba shirika la ndege linatakiwa kufungiwa kwa muda wakati uchunguzi unafanyika na rubani atupwe mbali. Huu ni uzembe mkubwa SAAANA. Tanzania tu ndo tunaona maisha yatu hayana thamani, kwanini lakini?????
Nasisi wabongo tumezidi kuwa wapole, ingekuwa nchi nyingine esp west hapo ni keleleeee...
Yaani nimeachwa na butwaa....
ReplyDeleteHaiyumkiniki rubani aliye funzwa kwa kiwango cha kimataifa, anyedhibitiwa kwa kiwango hichohicho akafanya uamuzi wa kizembe na hatari namna hiyo.
Katika fani hii, uamuzi wa mwisho anao RUBANI, full stop.
Nikiwa mdau mwenye uzowefu wa miaka kadhaa katika fani hii nje ya nchi, nakuhakikishieni rubani kama huyo hiyo ingekuwa ndiyo flight yake ya mwisho katika anga za nchi.
Nitasubiri kwa hamu uamuzi wa TAA, hapo ndipo tutakapojuwa kama kuna upumbavu mwingine au la. Maana TAA inahitajika kutumia nguvu zake zote za dola kumdhibiti huyu rubani. Baadae na kampuni pia ichunguzwe jinsi inavyo endeshwa na kuangalia kanuni zao za flight operations.
Inasikitisha kuwa rubani anaweza kufanya jambo la hatari bila kujali hata maisha yake mwenyewe.
Cha kusikitisha ni kua labda anfanya hivyo kwa kujiamini hakuna lolote litakalo mkuta kisheria na vinginevyo!
Wizara ya Mh. Omar Nundu yahitajika kutoa meno yake hapa....tena makali.
Poleni wanachi kwa kuponyoka toka mdomoni mwa kifo.
Poleni sana na Mungu ashukuliwe hakuna aliyepoteza maisha, ila kwa ushauri wangu mambo kama haya yasitokee tena ni vyema mkawasiliana na wanasheria na kuwafungulia mashitaka kwanza wahusika wa ndege, pili mamlaka ya ndege na selikari kwa ujumla. lazima mtakuwa mmeadhilika kwa namna moja au nyingine, pia kisakolojia mnahitaji fidia.
ReplyDeleteMimi nashauri habari hii ipelekwe kwenye magazeti na pia auric air waandikiwe malalamiko rasmi kwa kutochukua tahadhari.Pole sana kwa mkasa huu
ReplyDeletepole sana ndugu. nakushauri mutafute list ya abiria wenzako na mulifungulie mashtaka shirika hili pamoja na wahusika wote kama wafuatao:
ReplyDelete1. pilot
2. shirika la ndege
3. safety officer wa mwanza
4. safety officer wa bukoba
Mimi nilishaaapa sitapanda tena hako kandege cha AURIC maana nilishawahi kukapanda kufika angani hali ya hewa ikawa mbaya sana cha ajabu pilot hakusema chochote wakati abiria wote mule ndani presha zilipanda, ila tunashukuru tulitua salama. Pole mdau
ReplyDeleteWanasubiri mfe ndo waanze kuchukua hatua si tumezoea kuchukua tahadhari baada ya tukio.
ReplyDeleteMdau Fidel
Contacts zao ni hizi:
ReplyDeleteMwanza Office
Auric Air Services Ltd
P.O.Box 336
Mwanza Tanzania.
Tel: 255 28 2561286
Cell: 255 783 233334
255 736 200849
255 736 200853
Email : reservations@auricair.com
auric@auricair.com
Dar-Es-Salaam Office
Auric Air Services Ltd.
Tancot House Sokoine Drive
P.O Box 9771
Dar-es-Salaam
Tanzania .
Tel: 255 22 2126043
255 22 2126044
Cell: 255 784 749769
Email : reservations@auricair.com
auric@auricair.com
It is sad to hear for Auric Air. I have been using their service for quite sometime. To my surprise, the person who has written this article did not know that Auric Air always fly via Rubondo. I have flown with them to Rubondo also. I have been using their service for myself and my group of missionaries from U.S. I have also had a bad experience with Precision Air as we had the same kind of Landing with Precision Air when I went to Bukoba in October. We were lucky to be safe as the pilot made a hard landing. My only suggestion is if something has to be done with the Bukoba Airport. We have seen no changes.
ReplyDeleteDale Mitchell & Duanne Morris.
+1 617 444 8480