Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mh Joel Bendera, akionesha aina ya vitabu vya masomo ya sekondari vilivyotolewa msaada na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Nkwamira Sustainable Life Trust ya Jijini Dar es Salaam ( kulia ) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo , Noreen Mazalla ,wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu hivyo Ofisini kwa Mkuu huyo wa Mkoa , Shule 10 za Wilaya ya Mvomero na Morogoro zimenufaoka na vitabu hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Nkwamira Sustainable Life Trust , Noreen Mazalla ( kulia) alikabidhi kitabu, Kaimu Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro,Salome Mwitumba ( kushoto) huku mwenzake wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, ikiwa ni ishara yakuwakabidhi shehena ya Vitabu vya masomo ya Sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi nne kwa Shule 10 za Wilaya ya Mvomero na Morogoro katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Mkurugenzi Mtendaji wa Nkwamira Sustainable Life Trust , Noreen Mazalla ( kati kati) akitoa maelezo ya mpango endelevu wa Taasisi yake katika kusaidia sekta ya elimu kwa Shule za Sekondari katika Mkoa wa Morogoro , ukianzia na vitabu vya masomo ya kidato cha kwanza hadi nne, shule 10 za Wilaya ya Morogoro na Mvomero, zimenufaoka kwa kusaidiwa vitabu vya Hisabati, English, Kiswahili, Civics, Jiongrafia na Historia, ( kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mh Joel Bendera akiwa Ofisini kwake. Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii, Mji Kasoro Bahari
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...