Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar amezindua rasmi programu ya kiswahili inayofundishwa na Chuo Kikuu cha Indiana. Porgramu hii (ya kufundisha Kiswahili)ni ya kwanza nchini Marekani ambapo wanafunzi wanaosoma Kiswahili wanapata ufadhili kutoka Serikali Kuu ya Marekani. Wanafunzi hao pia watapata fursa ya kusoma Chuo Kikuu cha Zanzibar kwa mwaka mmoja kama sehemu ya programu hiyo.


Pichani Balozi Maajar akipongezwa  mara baada ya kumaliza hotuba yake iliyoelezea historia ya Kiswahili nchini Tanzania na kazi kubwa iliyofanyika ya kukuza Kiswahili na kuunganisha Taifa. Hotuba hii ilipokelewa vizuri sana ambapo pia ilielezea pia ilielezea umuhimu wa wanafunzi wa Kimarekani kujifunza Kiswahili. Pichani umati wa wageni wakimsindikiza Balozi Maajar kwa makofi huku wamesimama. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2012

    HII nimeipenda, huyu mama aendelee na kuchapa kazi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2012

    Mwenye enzi akuzidishie ndugu yangu Alwiya oh. I mean Prof. congratulations

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2012

    Safi sana. Hii ina maana sasa Kiswahili kinafundishwa katika vyo vikuu zaidi ya 400 duniani na kutangazwa na vituo vya redio zaidi ya 70 nje ya TZ (vikiwemo VOA, BBC, FRI, Deutschewelle, All India Radio, Radio Misri, China, Urusi, Kongo, Kenya, n.k.). Shaaban Robert alisema "Titi la mama tamu, lingine haliishi hamu". Pia pongezi kwa Balozi Mwanaidi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2012

    Nini faida lakini ya kueneza Kiswahili? Uchumi wa nchi yetu waweza kukua kwa kufanikiwa kupata vyuo vingi kunakofundishwa Kiswahili, au vituo vya habari kunakotangazwa Kiswahili? Mimi nadhani Kiswahili kinaweza kutusaidia kuinua uchumi wetu kama tutafundisha wanafunzi wetu kwa kutumia Kiswahili, ili wanafunzi waelewe masomo yao vizuri, na waweze kuwa wabunifu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2012

    Chuo kinachofundisha Kiswahili ni Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 04, 2012

    sisi wenyewe tukikandia kiswahili hao wanatakakukifundisha safi sana tubadirike tupende vyakwetu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...