Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa wa Mkataba wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC),Bi. Christiana Figeres akifungua mkutano wa kimataifa wa sayansi na taaluma wa mabadiliko ya tabia nchi, Mjini Bonn nchini Ujerumani.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira Ya Ofisi wa Makamu wa Rais,Bw Richard Muyungi ambae Pia ni mwenyekiti wa Dunia wa kamati ya sayansi na Taaluma ya Mabadiliko ya Tabia Nchi (kulia) akiwa pamoja na washiriki wengine katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya Tabia nchi unaoendela mjini Bonn njini Ujerumani.
Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais,Bw. Alfonce Bikulamchi (mbele kulia) pamoja na wadau wengine wakifuatilia kwa umakini ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Sayansi na Taaluma wa masuala ya mabadiliko ya Tabia Nchi unaondelea Mjini Bonn,nchini Ujerumani.Picha na Evelyn Mkokoi.
Mdau asante kwa kutuhabarisha!!Kazi njema!
ReplyDeleteSUALA LA MABADILIKO YA TABIA NCHI:
ReplyDeleteMchawi wa kumbebesha mzigo ni Mabepari wa Dunia wenye viwanda na wapanga sera wa mashirikisho kama WTO(World Trade Organisation),WTC(World Trade Center) na wengineo.
Mfano,
1.Mabepari wenye viwanda,
Wao wapo ktk kukuza faida na kupanua wigo wa biashara tu.
2.Mashirikisho kama WTO ,WTC na mengineo Wadau wake wakuu ndio hao hao Mabwenyenye ambao wanajilindia maslahi yao na kuweka sera za kukuza bishara zao tu.
Hawa No.1 na No.2 ni kuwa MIKUTANO KAMA HUU WA HUKO UJERUMANI NDIO YA KUAMUA KUWATOZA KODI KUBWA KABISA YA UHARIBIFU WA MAZINGIRA NA UTE WA GAMBA LA DUNIA 'OZONE LAYER' KUTOKANA NA MOSHI WA VIWANDA NA MADHARA YA KIFIZIKIA, KIKEMIKALI NA KIBAOLOJIA INAYOLETA HAYO MABADILIKO YA TABIA NCHI YANAYOWEKEWA KIKAO HICHO.