Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud Mohamed akifafanua jambo alipozungumza na Maaskofu mbalimbali kufuatia kwa matatizo yaliotokezea Zanzibar ya kuchomwa Moto kwa Makanisa mbalimbali,huko katika Ukumbi wa Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Askofu Mkuu wa Anglican Tanzania Dk Valontine Mukiwa wakwanza kulia akizungumzia kuhusiana na matatizo yaliotokezea Zanzibar ya kuchomwa Moto kwa Makanisa mbalimbali,huko katika Ukumbi wa Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar walipokutana Maaskofu mbalimbali na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud Mohd.
Askofu Mkuu wa Anglican Tanzania Dk Valentine Mokiwa akifanya mahojiano na Muandishi wa BBC kuhusiana na matatizo yaliotokezea Zanzibar ya kuchomwa Moto kwa Makanisa mbalimbali,huko katika Ukumbi wa Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Na Miza Chande-Maelezo Zanzibar
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohammed Aboud Mohammed ameuhakikishia umoja wa Mapadri nchini kuwa malamiko ambayo wameyatoa kwa Serikali atayawasilisha kwa maandiko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohammed Shein.
Malalamiko hayo yanatokana na vurugu ambazo zilitokea mwishoni mwa wiki katika maeneo ya mji wa Zanzibar ambapo Makanisa matatu yalichomwa moto na kusababisha uharibifu wa mali mbali mbali za Makanisa.
Waziri Aboud ameyasema hayo alipokutana na Ujumbe wa umoja wa Makanisa Tanzania ulioongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Dk. Valontine Mokiwa katika Afisi ya Waziri huyo Mjini Zanzibar.
Amesema Serikali na kila mwananchi mpenda amani amehuzunishwa sana na fujo zilizotokea na kuahidi kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kufanya kazi yake ya kuwatafuta wale wote waliohusika na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Waziri Aboud amesema amefurahishwa na subra ambayo Wakristo hao wameichukua bila ya kulipiza kisasi jambo ambalo linawajengea heshima kubwa kwa jamii.
Amezisisitiza Taasisi za dini kuendelea kuhubiri amani kama lengo la taasisi hizo linavyosema na kuongeza kuwa kama kuna mambo ambayo yanafaa kuzungumzwa ni suala la ukosefu wa ajira na umasikini nchini.
Amesema Viongozi wa Dini wanapaswa kuwa na mipaka,busara na elimu wa yale wanayoyahubiri na kuwataka wananchi kuweza kuchambua juu ya viongozi ambao wanafaa kusikilizwa na wale ambao hawafai kusikilizwa.
Aidha amewahakikishia Viongozi hao wa dini kuwa na amani na kwamba ulinzi umeimarishwa katika Sehemu zao za ibada ili kuweza kuzuia watu ambao hawaitakii mema Zanzibar.
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Dk. Valontine Mokiwa amesema kuwa matukio ambayo yamekuwa yakifanyika yamepindukia mpaka Zanzibar lakini Serikali ya Mapinduzi imekuwa imeonekana kuwa na imani kubwa wakati hali inakuwa mbaya.
Amdai kuwa Makanisa 25 katika Visiwa vya Unguja na Pemba tokea mwaka 2001 yameshambuliwa lakini hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa kwa wahalifu hao jambo ambalo linawapa shaka.
Mokiwa amesema Jamii ya Wakristo nchini ina hamu ya kujua nani kahusika na kuchukuliwa hatua za kisheria na siyo tu kuishia kuambiwa Jeshi la Polisi linaendelea kuwatafuta wahalifu hao.


Askofu Dr. Mokiwa Umeongea vizuri sana kwa niaba ya wakristo wote.
ReplyDeleteInakuwaje hakuna aliyeshitakiwa kwa kuchoma makanisa?
Wakumbuke kuwa nyakati zimebadilika. Usipokamatwa kipindi cha serikali hii utakamatwa tu hata miaka kumi imepita na utahukumiwa wa makosa uliyoyafanya.
Wanaowakumbatia wachoma makanisa watapita uongozi wao.
Hatutasahau
Mh Abood tunashukuru kutambua kuwa wakristo wana busara zaidi kwani nina hakika kitendo kilichofanywa kuchoma makanisa ingekuwa ni misikiti nchi nzima ingerindima. Mtetezi wetu yu hai ngoja tusubiri tuone mtafanya nini ama ndo kutuliza watu na kuwaacha hao wahuni kuendelea kuumiza watu bila hatia
ReplyDeleteInakuaje pia hakuna aliyeshitakiwa kwa kuchoma kiwanda cha vitabu vya dini ya kiislamu pale mwenge? Waumini wa kikristo EPHATHA waliohamasishwa na mchungaji wao huku wakikaidi amri ya jeshi la police...mnadekeshwa eeeh watu huwa kuna wakati wanachoshwa pia.
ReplyDeleteASKOFU DR. MOKIWA UMEWAAMBIA UKWELI KABISA. SISI WAKRISTU NI WATU WENYE HOFU YA MUNGU HATULIPIZI VISASI.TUNATAKA KUONA MWISHO WAKE KWA AMANI. HATUTACHOMA MISIKITI KAMA WAO.
ReplyDeletePoleni na Pongezi kwa wale woote waliodhurika na fujo za Zanzibar. Vyombo vya habari kama nyenzo muhimu ya mawasiliano Muwawekee wahuni hao Hotuba ya Mwl Nyerere iliyoelimisha juu ya dhambi ya ubaguzi. Yawezekana Hawajui walintendalo! Elimu Elimu Elimu. Ni dawa idumuyo bila kujali dini, kabila, jinsi, rangi nk nk nk.
ReplyDeleteOk licha yakuwa mimi ni Muislam sijafurahiswa na vitendo vya kuchoma makanisa na huenda ni propaganda za watu wenye yao zamani wanataka kuchukulia kisingizio cha UAMSHO kuchoma makanisa wakati nia ilikua zamani.
ReplyDeletePili kuhusu kushitakiwa kuchoma kanisha je Nyie mnaotoa maoni mnaweza kumkamata mtu kumpeleka mbele ya sheria au kumpoint mtu? Sheria si upenzi waliokamatwa wamekamatwa ndani ya matukio mengine na sio katika kuchoma makanisa mkumbuke wekeni akili zenu sawa sio umkamate mtu kwenye maandamano umpe kesi ya kuchoma kanisa,kumbukeni mkutano na Saidi mwema unatokea kumbe watu wanachoma makanisa wakati huo huo na hapo watu walikua washakamatwa.
Akitokea shahidi kusema wameona watu basi watakamatwa tuwe na busara vile vile.
Mwisho haya yote - yanasababishwa na serikali ya CCM kwa nini watu wanataka uhuru wao wa maoni hawawapi uhuru? jazba ndio inayopelekea yote huko.
one day else kitaeleweka...tunajua sisi tuna subira kuliko wenzetu ukweli ni kwamba hayo ni mafundisho mnayofundishwa msikitini, hata ukiangalia clip za viongozi wenu zinahamasisha hayo, unafiki ndio unaowaongoza...eti mnasema hamuhusiki. hayo makanisa 25 mliyoyachoma toka 2001 je?? kwanini hamchomi temple za wahindi???
ReplyDelete