Waziri wa zamani wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akimkabidhi kitabu cha sheria na mwongozo wa utendaji kazi wa wizara hiyo Waziri Mpya  Dkt. Hussein Mwinyi.Makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye ukumbi wa wizara hiyo
 Waziri Dkt. Mwinyi akipokea kitabu cha utekelezaji wa majukumu ya wizara  hiyo ambapo ameahidi kuendeleza kutekeleza na kuendeleza majukumu yale aliyoyaacha ingawa anatambua changamoto kubwa ni kuboresha huduma ya afya upande wa tiba.
 Mawaziri hao wakipeana mkono mara baada ya makabidhiano hayo Dkt. Mponda amemtaka waziri Dkt. Mwinyi kufuatilia na kusimamia vyema  utekelezaji wa  mikakati ya sekta ya afya ili kuweza kuimarisha huduma ya afya kwa wananchi
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi aliyekaa katikati,Kulia ni waziri wa zamani Dkt. Hadji Mponda na Naibu Waziri Mpya Dkt. Seif Rashid aliyekaa kushoto, wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa wizara hiyo mara baada ya makabidhiano ya ofisi.(Picha na Catherine Sungura-Mohsw)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 16, 2012

    Pole Dr. Hadji Mponda.

    Inasikitisha sana lakini ndio ilivyo yameshakuwa!

    Anaonekana ni mtu mstaarabu sana, haya inabidi uyakubali mabadiliko na majaribu na sasa unarudi Darasani(Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili-MUHAS) kwenda kufundisha!

    -Unaweza kuwa na Mali ukafilisika,
    -Unaweza kumiliki kitu kikakutoka,
    -Unaweza kuwa na Madaraka yakatoweka,
    -Unaweza kuwa na mwana akaenda mbele za Haki!

    MWISHOWE UKABAKI UNALIA NA NAFSI!

    WAZARAMO WALISEMA 'MULUNGU CHIBIDU!'

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 16, 2012

    Pole Dr. Hadji Mponda!

    Wala usijali Mungu atakupa kingine.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 16, 2012

    Daktari Hadji Mponda,

    Unalo Genge?,
    Unamiliki mabasi ya Daladala,Teksi au Boda boda?
    Una mbuzi,kuku,bata na ng'ombe? au Shamba?

    Kama huna ni bora upande ndege wende zako Majuu ukafundishe Vyuo Vikuu huko!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 16, 2012

    Jamani tuwaonee huruma Mawaziri Waliotolewa !

    Hakuna kitu kinaumiza na kutia simanzi kama moja ya haya hapa matatu (5):

    1.Kufilisika kwa mali
    2.Kufiwa na mtu kipenzi wa karibu
    3.Kuanguka madaraka
    4.Kusalitiwa ktk Mapenzi
    5.KUBWA LAO (Kuthibitika iwe kwa matokeo ya Vipimo au kutambua ya kuwa sasa umeathirika kwa Ukimwi au Kansa)!

    YOTE TISA YANAUMA ILA MAUMIVU MAKALI ZAIDI YA NO.(5) NA NO.4 HAPO JUU (KUATHIRIKA,KUSALITIWA MAPENZI) INAUMA ZAIDI NI NAMBA TATU (3)...YAANI KUANGUKA KIHESHIMA NA MADARAKA!

    Dr.Hadji Mponda anajikaza kisabuni ila anatia huruma sana!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 16, 2012

    Madaraka na Mapenzi yana RAHA na KARAHA!

    1.MADARAKA:
    Kuchaguliwa kupata Madaraka KUTAMU KAMA ASALI!

    Kulega lega kwa Madaraka KUCHACHU KAMA LIMAO!(Kipindi cha migogoro ya Madakitari)

    Kuondolewa kutoka Madarakani KUCHUNGU KAMA SHUBIRI!

    2.MAPENZI:
    Kumpata mpenzi mpya au ndoa Changa KUTAMU KAMA ASALI!

    Kulega lega kwa Mapenzi au Ndoa KUCHACHU KAMA LIMAO!

    Kuvunjika kwa Penzi ama Ndoa KUCHUNGU KAMA SHUBIRI!

    EWE MOLA KWA MASAHIBU HAYO MAWILI HAPO JUU NO.1 NA NO.2 UTUPE SUBIRA!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 17, 2012

    Hivi hakuna njia ya Busara zaidi ya kuwatoa watu ktk kazi zaidi ya kuumbuana kama hivi?

    Inakuwa kama ndio basi tena na kuwa labda mtu huyo hana umuhimu kabisaaa, kitu ambacho sio kweli!

    Napendekeza wanaotolewa kazini waitwe kwanza kabla ya zoezi zifanyike hatua hizi:

    1-Waelezwe makosa yao,
    2-Wajiuzulu,
    3-Wakabidhi Ofisi (Kwa faragha/ siri) kwa Watumishi wapya,
    4-Halafu wasafirishwe nje ya nchi
    5-Na huku nyuma ndio itangazwe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...