Wilfred Moshi amekuwa Mtanzania wa Kwanza katika historia ya Dunia,kupanda Mlima Mrefu kuliko yote Duniani,Mlima Everest uliopo kule nchini China.Pichani ni Mtanzania Wilfred Moshi akiwa kileleni kabisa mwa Mlima huo huku akiipeperusha vilivyo Bendera yetu ya Taifa.

kwa kusoma zaidi juu safari nzima ya Mtanzania Mwenzetu,Wilfred Moshi kwenda huko mlimani.
AU 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2012

    Mlima Everest upo NEPAL siyo China. Kwanini usihakiki unachokisema jamani?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2012

    Hongera sana Wilfred.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2012

    Nadhani kwa mtazamo wangu mimi huu mlima uko border ya nepals/Tibet china in southern asia

    na unaweza kidogo kuufananisha na huu wetu hapa kilimanjaro yule alomjanja ndie anaeutangazia kuwa uko kwake

    kwani hata huu kilimanjaro unaujuwa wewe kuwa uko tanzania ila wazungu wengi wanajuwa uko KENYA, kwani jirani zetu wao wanaupigia debe sana kuwa uko kwao na sisi watanzania kimya

    kwahio ukisema uko nepal ni sawa ila hao wajanja wengine wanaupigia debe kuvutia utalii kwao na ndio ukaona hata huyu aloandika hii habari HAJUI KITU

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2012

    utapandaje mlima everest huna gloves mikononi si vidole vitaganda with in minutes.... hiyo picture sio

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2012

    Mchagga wa kwanza kufika summit ya mt. Everest!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 19, 2012

    NDUGU YETU WOLFRED MOSHI HONGERA SANA KUFIKIA KILELE CHA EVEREST.

    UMEONYESHA NIA DHAHIRI NA UJASIRI USIO KIFANI KUUKWEA MLIMA NA BENDERA YETU YA TANZANIA.

    KHERI UISIMIKE KILELENI HUKO KAMA ISHARA YA UZALENDO (NA UGUNDUZI WETU WA MLIMA EVEREST).

    MAINA OWINO
    UK

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 19, 2012

    mwambie mwambie huyo, sana sana asome vitabu siyo kutizama sinema tu za wanaigeria

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 20, 2012

    Hongera sana Wilfred Moshi....! Umeweka historia mplya kwa wa TZ. Ila naomba kujuzwa, huu mlima una vilele vingapi? au ulipiga picha hii wakati umeisha anza kushuka...maana naona kwenye background kama kuna kaji kilele kengine? ( Msinishambulie wadau, nataka kujua zaidi).

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2012

    ...ummm... this picture looks... sijui! ... kama vile... studio maybe? ... :-)

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 20, 2012

    Hongera sana Fred... Kaka Michuzi tunaomba na yeye aalikwe Ikulu jamani kama akina Hasheem Thabit au unashauri vipi? Maana kafanya jambo jema.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 20, 2012

    Huyu jamaa amefika kwenye summit na sio Peak,ndio maana mnaona bado kuna kuna peak nyingine!
    Nakuhusu gloves unazoea tu, ukizidi kukaa kwenye baridi, na pale juu jua ni kali hata watu wanaweza kukaa bila ya nguo na hugandi!
    hii ni video, jamaa wapo Alps Switzerland
    http://youtu.be/9Jhs8yExFNs
    picha hizi hapa
    http://www.google.ru/search?q=%D0%BC%D0%BE%D1%80%D0%B6%D0%B8%20%D0%BB%D1%8E%D0%B4%D0%B8&um=1&hl=en&biw=1366&bih=667&ie=UTF-8&sa=N&tab=Ti&tbm=isch&source=og

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 20, 2012

    Hongera sana Fred, Kwa wadau mnaopenda kuongea bila kufanya utafiti, Fred ni mzoefu ni kupanda mila, Kilimanjaro ndio ofisi yake, so kuvua glove for a picture its possible again kaka umeonyesha mfano kwa wapambanaji wengine wa mlima kilimanjaro hongera sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...