Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB,Dk Charles Kimei akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya mambo mbalimbali na mkutano wa wana hisa utakaofanyika jumamosi ya wiki hii mjini Arusha.
BENKI ya crdb inatarajia kutoa gawio la shilingi bilioni 19 kwa wanahisa wa benki hiyo kwa kipindi cha mwaka 2011- 2012 kama sehemu ya faida ya shilingi milioni 37 ambazo benki hiyo imepata kwa kipindi hicho.
Mkurugenzi mtendaji wa benki ya CRDB dakta Charles Kimei alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha alipokuwa akitoa taarifa za awali kuhusu mkutano mkuu wa17 wa wanahisa wa benki hiyo tangu kubinafsishwa toka mikononi mwa serikali mwaka 1996.
Dk Kimei aliongeza kuwa mkutano huo pia utafanya uchaguzi wa wakurugenzi watatu wapya baada ya wale wa zamani kumaliza muda wao wakurugenzi mbao wanapaswa kuchaguliwa na wanahisa hao.
Dkt Kimei alisema mkutano huu waCRDB utafanyika kwa mujibu wa sheria ya makapuni sehemu ya 133 na kwamba mkutano huu ni muhimu sana ambao wanahisa wote wanatakiwa kuhudhuria ili kuja jinsi hisa zinavyotunzwa .
Aliongeza kuwa pamoja na masuala mengine wanahisa watapewa taarifa ya mahesabu ya biashara ya mwaka uliyopita unaoishia 2011 na kuwapa taarifa za maendeleo ya benki hiyo.
Dakta Kimei alifafanua kuwa benki hiyo inakila sababu ya kutoa sehemu ya faida kwawanahisa wake kwakuwa mtaji wa benki hiyo umepanda na CRDB ndiyo benki yenye mtaji mkubwa kuliko benki nyingine za hapa mjini.
Aidha aliwataka watanzania kutambua umuhimu wa kuwa na hisa kwani wengi wameonekana kukosa mwamko na nafasi yao kuchukuliwa na watu wa nje baada ya watanzania kuonekana kuwa hawatambui muhimu wa kumiliki hisa.
“Watu wengi wamekuwa wakiuza hisa mtaani kwa bei ya hasara jambo ambalo linasababisha kushuka kwa thamani za hisa na kutofikia malengo waliojiwekea wakati wakinunua hisa”alisema Dakta Kimei.
Aliongeza kuwa mkutano huo utafuatiwa semina ya kwa waandishi wa habari ambayo itafanyika jijini Dar-es-salaam yenye lengo la kuwapa ufahamu wanatahaluma hao ili kutambua kazi za benki hiyo na namna inavyotoa huduma kwa wateja wake wayoiwezesha benki kufikisha mtaji wa zaidi ya shilingi bilioni 250 hadi sasa.
Watanzania Muamko wa Kifedha vipi?
ReplyDeleteCRDB hapa inawashukia Jamvini kwa Mipango ya Hisa na Uwekezaji.
Mara nyingi nimeona Makala zinazohusu masuala ya Mipango ya Uchumi na Fedha watu hawana mwamko wa kufuatilia kabisa wala kuhoji?
Au ndio tuseme athari za Mtikisiko wa Kiuchumi na Kifedha Nchini Tanzania?