Gari ndogo aina ya Land Rover Freelander lenye nambari za usajiri T 365 ATN likiteketea kwa moto mchana huu katika barabara ya Mtaa wa Lumumba jijini Dar.chanzo cha moto huo ambao umeiteketeza kabisa gari hiyo upande wa injini ambao moto huo ulianzia bado hakijafahamika mpaka sasa.hakuna aliedhurika waka kujeruhiwa katika ajali hiyo.
Wasamalia Mbali mbali wakijitosa kusaidia kuuzima moto huo ambao ulikuwa ukiwaka kwa kasi sana. 
 Wasamalia wakiisukuma gari hiyo ili ikae katika sehemu ambayo hakuna magari mengine wakati ikiendelea kuwaka moto kabla ya gari la zima moto kutoka manispaa ya Ilala kufika.
 Juhudi za kuuzima moto huo zikiendelea.
 Mashuhuda wakiangalia gari hiyo wakati inateketea kwa moto mchana huu,huku gari ya zima moto kutoka manispaa ya Ilala ikiwa imewasili tayari kwa kuuzima moto huo.
 Sehemu ya Injini ya Gari hiyo ikiwa imeteketea kabisa.
  Wakiisukuma ili kuitoa katikati ya Barabara.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa mchana huu katika barabara ya Mtaa wa Lumunda,Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam baada kufanikiwa kuuzima moto uliokuwa ukiwaka kwenye gari hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Mungu wangu, pole yao waliopatwa haya

    ReplyDelete
  2. bongo bwana!! watu hawana kazi watuwote hao wanashangaa gari inaunguwa do!!!,hii inaamanisha watu wengi huzurura mjini bila kazi,ni wingi wao ni vibakatu,serikali tafutieni watu ajiraaaa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2012

    Mjapani na used cars zake atatutoa roho na kutufilisi kimaisha!

    Ndio maana nchi zingine magari ya mitumba hayatakiwi kabisa kwa sababu ya mambo kama haya.

    Kama mtu atachagua kumiliki gari anatakiwa liwe jipya liwe ktk guarrantee na aweze kulipia full coverage insurance.

    Kwa hulka zetu za kibongo za ''magari, magari'' bila mipango unaweza kukuta mtu hata Kiwanja cha kupimiwa kwa hatua za miguu hana lakini hela puuu Milioni 10 anapata kwa bahati, anawahi Yadi kuchagua gari!, unakuta mtu anarukia kumiliki gari wakati mipango wala njia za kipato hana!,

    Bora kuwa na Genge la bamia na dagaa linalozungusha vizuri mauzo la thamani ya Tshs. 2 Milioni kuliko umiliki wa gari la Tsh. 10 Milioni lakini bila mipango endelevu ya kipato cha pesa!

    Sasa ili kulipata hilo gari 'used' huenda jamaa,

    1.Amekopa Saccos kununua gari au,

    2.Labda ni hela ya kudunduliza ktk biashara zetu ngumu za kufilisika kirahisi au,

    3.Labda ni hela yake ya mwisho ya mafao baada ya kupunguzwa kazini.

    Hivi kwa mazingira hayo matatu (3) hapo juu jamaa atakuwa mgeni wa nani Duniani hapa?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 14, 2012

    Uchakachuaji wa TBS - Haya ndio matokeo yake.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 14, 2012

    Haya ni madhara ya gereji mchangani kwa fundi Rama. Tunadhani ni rahisi lakini kutokana na ufundi wa kubahatisha utakuwa wiring ya kuungaunga ndio imeleta ajali hiyo. Tuombe mungu insurance yake iwe comprehensive.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 14, 2012

    hii ni njamaa wamemchomea ebwana eeh bongo bongo ukiwafichua mafisadi wanakuchomea kagari kako halafu mnawasingizia majapani, mjapan anatengezena kitu bongo kuliko mchina na hata kama ni mtumba wee acha hizo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 14, 2012

    unamuonea hilo gari si la kijapani. hapo tatizo ni ufundi. hatuna mafundi umeme gari waliobobea ndio mara nyingi magari yanayo ingua. ni tatizo la wiring. mpe pole mwinzio it can happen to anyone hata gari jipya hali chakai?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 14, 2012

    Mchangia hoja wa tatu, naomba nikurekebishe. Freelander ni gari ya kampuni ya landrover. Original ni muingereza.
    Pia kuhusu suala la kiwanja au gari kipi kianze itategemea na priority ya mtu mwenyewe na plans zako.
    Mwingine anapata pesa ananunua gari nalo linamragisishia maisha na kupata kiwanja hadi nyumba.

    Tukumbuke kwamba dunia tunayoishi sasa gari imeishakuwa kitendea kazi ktk maisha ya kilasiku na sio luxury kamailivyokua zamani.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 14, 2012

    Nafikiria kwa vile hajaja kwako kuomba chumvi au nauli basi muache tu hata kama kakopa makato ni yeye anarejesha, kama kadunduliza fine ni yeye,na kama aliamua kuwa na gari badala ya kiwanja ni sawa tu make halali kwako. Tatizo letu watanzania tunajua kujadili plan za watu unaona ana gari unampangia why asingejenga nyumba kwani nyumba haiwezi kuungua? mara ngapi tumeona nyumba zikiwaka na kuteketea ni yale yale tu eidha alikopa akajenga, ama alidunduliza ama mafao ajali ni ajali yaweza kukupata haijalishi ulikopa ama ulitoa malimbikizo ya miaka kadhaa. Tusikae na kupangia watu kitu gani waprioritize katika maisha hasa pale wahusika wanapokuwa hawajaja kwako kukuomba msaada. Hata iwe mpya au used yaweza teketea tu usiishie kusonga watu na maneno mazito ivo wakati mwenzio yuko katika masikitiko.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 14, 2012

    Anonymous 02:50:00. "Hivi kwa mazingira hayo matatu (3) hapo juu jamaa atakuwa mgeni wa nani Duniani hapa?" Mgeni wa Mungu.Nyumba, Nyumba mbona waHindi hawajajenga 'TZ'Bongo wanaishi Neshino House mpaka kufa na wajukuu na vitukuu. we uko Bongo au Mwenelumango?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 14, 2012

    We mdau wa "Thu Jun 14, 02:50:00 PM 2012" ebu acha ushabiki, ajali ni ajali inaweza kukukuta hata wewe usiye na gari! Kwani kuwa na gari unaona ni tatizo? Ngoja nikuulize hivi umesoma kweli? kama jibu ni ndiyo, je unajua maana ya priorities? Kama hujui jibu lake nenda katafute, then ukae kimya. Kila anachokifanya muhusika anajua umuhimu na ubaya wake. Ni sawa na wewe leo ukiulizwa huyo mke wa pili uliyenae ni wa nini wakati gharama ya kuendesha famila mbili ungeweza ku-invest na kupata faida! Acha mitazamo ya chuki na wivu! Jaribu ku-analyse mambo kwenye angles zote!Upo? Mdau uliyeunguliwa na gari, pole sana, mshukuru Mungu kwamba hukupatwa na madhara

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 14, 2012

    Ongea vitu vya maana wewe mdau hapo juu, ndio maana ikaitwa ajali. Una uhakika gani kama hiyo gari ni 2nd hand au unaonge tuu. watu wengine bwana

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 14, 2012

    hiyo gari ni lAAND LOVER FREELANDER YA KIINGEREZA. HIZO MODEL ZOTE ZA HAYO MAGARI ZINA FAULTY ENGINE NA MECHANISM NZIMA KUTOKA KIWANDANI. NA SABABU KUBWA, ZILITENGEZWA ENGINE NA MG-ROVER NA SIO JAGUAR-LANDROVER WANAOTENGENEZA LANDOROVERS NYINGINE. NI SAWA NA KUNUNUA MERCEDES BENZ A-CLASS. NI MBOVU FROM NEW PIA. HIYO GARI SIO YA KIJAPANI. KATIKA GARI ZILIZOKO RELIABLE DUNIANI, MJAPANI NDO ANAONGOZA!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 15, 2012

    Freelander zina matatizo sana hizi gari. Hii ni ya pili sasa naona inaungua katika miaka ya karibuni,

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 15, 2012

    Kumuunga mkono Mtoa Maoni wa tatu (3) Anonymous wa Thu Jun 14, 02:50:00 PM 2012

    Utafiti unaonyesha Mtanzania ni mtu anayependa sana 'ujiko' na sifa na ndio maana idadi kubwa ya wanaojaza mabara bara kwa magari hawana uwezo huo ila wana jilazimisha ili kupata 'ujiko' na ndio sababu watu wengi hawana uwezo wala jeuri ya kununua magari mapya wanategemea Ukombozi wa magari ya Mitumba!

    Zaidi ya hapo hata kama ni Landrover UK made kwa taarifa yenu idadi kubwa ya magari 'used' licha ya origin kuwa yaneundiwa Europe yanatokea Japani!

    Kwa kuwa Mjapani ameshaona Mtanzania na baadhi ya nchi masikini ni makuku ya kisasa ya kukusanya na kuzamisha ktk magunia kirahisi!

    Serikali inawatoa kamasi kwa Kodi ya uchakavu 45% ili mkome kuagiza mitumba na badala yake mfikiri vitu endelevu zaidi kama Kilimo, na kuuza Magenge ya Bamia na Dagaa!

    Kama mfano aliotoa Mdau mtu anatumia hela yake ya 'bahati' aliyoipata kwa mazingira ya tundu ya sindano matatu (3) anatumia Tsh. 10 Milioni kununua gari 'mtumba' halina uhakika 'guarrantee' ni akili kweli hiyo?

    Wacha yeye alivyosema ni bora kuwa na Genge la Bamia na Dagaa linalozungusha mauzo na faida nzuri la Tshs. 2 Milioni badala ya gari ya Tsh.10 isiyoingiza kitu huku mtu hana kipato cha uhakika,,,wacha Tsh. 2 Milioni huko ni mbali sana, sema ni bora kuwa na Genge la thamani ya Tsh. 200,000/= (SHILINGI LAKI MBILI) linaloingiza kuliko umiliki wa gari bila Mipango!!!

    TUPIGE HESABU:

    1.GARI YA TSHS. 10 Milioni BILA MIPANGO YA KUPATA PESA:
    Mtu anaamka asubuhi anajaza mafuta Tshs. 10,000/= anatekenya ufunguo anaelekea Mjini anafika anapaki anatoa gharama ya maegesho kwa siku Tshs. 1,000/= anafanya matumizi yake anashinda ktk Mgahawa kutwa akinywa chai na Juisi (mfano anakula Tsh. 5,000/=hajaingiza kitu JUMLA TSHS. 16,000/= gharama kwa siku.

    2.MWENYE GENGE LA BAMIA NA DAGAA LA TSHS. 200,000/=:

    Muuza Genge anapanga fungu zake za bamia na dagaa ANATUMIA THS. 200,000/= KUTOKA TSHS. 10 MILIONI ALIZOPATA KWA BAHATI KTK MAZINGIRA YALE MATATU (3) PALE JUU (TSH.10,000,000-TSHS.200,000/=) ANAWEKA BENKI TSHS. 9,800,000/= Anatumia TSHS. 200,000/= anaingiza TSHS. 40,000/= FAIDA kwa siku.

    SASA JE NANI MJANJA NA MWENYE AKILI NZURI KATI YA MMILIKI GARI ASIYE NA MIPANGO YA KUINGIZA FEDHA AU MWENYE MIPANGO MUUZA GENGE?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 15, 2012

    KIAMA KINGINE CHA WENGI WA WAMILIKI WA MAGARI 'USED'

    Ni muhimu kufanya mambo kwa mpangilio na 'priorities' kama zinavyostahili badala ya 'ujiko' na misifa!

    Ni dalili ya wazi ya kuwa kitendo cha kumiliki gari used ni kuwa huna uwezo wa kununua gari jipya!

    NI JAMBO LA KAWAIDA KWA MMILIKI WA GARI ZAIDI AKIWA MTANZANIA KTK TANZANIA AKISHIKILIA USUKANI HUKU MFUKONI AKIWA HANA AKIBA!

    MKUBALI MKATAE, WAPO WENGI TU HATA ULE UWEZO WA KUJAZA MAFUTA YA GARI LAKE ANALOLIMILIKI HANA, ANAJAZA MAFUTA KWA PESA YA KUBAHATISHA!

    NILISHUHUDIA JIJINI DAR POSTA MJINI MTU MMILIKI WA GARI AKISHINDWA KULIPA SHS. 300/= (MIA TATU) YA GHARAMA ZA MAEGESHO!

    UNAKUTA WENGI WA WATU WANAMILIKI MAGARI YA TSHS. 10 MILIONI HAWANA HATA AKIBA YA SHS. LAKI MOJA!!!

    MNABISHA?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 15, 2012

    Mdau wa tatu (3) juu Anonym Thu Jun 14, 02:50:00 PM 2012

    Ametoa msaada kwa watu kuwa msikurupukie umiliki wa magari ktk mazingira hatarishi bila 'priorities' za kweli kama wanavyodai watu,

    Kwa kununua gari la mtumba ina maana huna pesa ya kutosha kupata jipya, ni bora ungefikiri vitu vya maana zaidi maishani kuliko kuiweka rehani akiba yako ya mwisho maishani kwa kufungua Genge badala ya 'ujiko' wa umiliki wa gari bila mipango!

    Mpo hapo?

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 15, 2012

    Ujumbe kamili:

    Msitegemee kitu kinachoitwa 'used' kwa kuwa nacho ni kama umebeba maiti muda wote inaweza kuoza na hakuna 'guarrantee' !

    Hilo ndio somo kamili sio kumchamalia jamaa Mdau wa 3 hapo juu kwa kuhusisha masuala ya nyumba,viwanja na Japan,,,

    Watanzanie tuamke, mara zote watu hatufanyi mambo na maamuzi kwa tija, tumeegemea zaidi kwenye kijiko na sifa za muonekano tu.

    Kama kununua gari nunua lenye angalau uhakika sio kubeba maiti ama time bomb kama huo mkenge alioingia ndugu yetu wa Landrover Freelander.

    Je mfano badala ya kununua hilo kopo angetumia pesa hizo kununua Hisa ktk soko la Hisa la Dar angekosa kitu?

    Imebaki akafugie kuku sasa hilo kopo!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 15, 2012

    Anonymous,
    sema wewe bana mbona wengi hatutoi maoni kwa kutokuwa biased!!
    Ajali kweli ina kinga, sivyo kama tulivyozoea kwamba ajali haina kinga, lakini tusitoe maoni ambayo yanapelekea kuponda wengine, hali zatofautiana na kwa hali ya hapa tz, tujaribu kueneza tamaduni za kufanya matengenezo mara kwa mara!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 15, 2012

    Bajaji 'mpya' nayo ni usafiri:

    Ya nini tabu kununua gari 'second hand' wakati kama kigezo ni usafiri kama mnavyo toa ubishani ni bora mtu ukanunua Bajaji lakini mpya!

    Inaonekana suala la umiliki wa gari lipo 'kiujiko' zaidi kuliko dhana nzima ya usafiri!

    Ni vile pana kale kamtazamo kuwa Babaji ni usafiri usio na heshima au kijiko fulani hivi.

    Leo unakuja kuwauwa watoto na familia kwa njaa na kuwazamisha ktk lindi la umasikini kwa kung'ang'ania kununua gari mtumba eti oooh 'priorities' za maisha, hivyo ni vipaumbele kweli au ujiko tu?

    Kama suala ni usafiri badala ya kununua gari la mtumba lisilo na uhakika kwa nini usinunue Bajaji mpya?

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 15, 2012

    $$$$$

    Jamaa atakuwa ametugharimu Tanzania fedha nyingi za kigeni kwa kuagiza gari mshipa!

    Wandugu kama mnavyoona hali ya uchumi ilivyo tete nchini na duniani, manunuzi ya vitu kutoka nje hata kama utaagiza nywele bandia, au makalio nandia kutoka China elewa utalipia huko kwa US$$$$ sasa muelewe kuungua kwa gari hiyo mumeihgarimu nchi fedha za KIGENI ZAIDI YA HASARA ALIYOIPATA MWENYE GARI HILO.

    MBISHANE KWA VIGEZO HUKU MKIANGALIA HALI HALISI DUNIANI NA NCHINI TANZANIA.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 15, 2012

    Tatizo umiliki wa magari watu wana fosi hadi haya mamitumba !

    Ni vile umiliki wa magari watu wengi wanatafuta ujiko na ushawishi wa ngono badala ya dhana nzima ya mahitaji ya usafiri!

    mpo hapo?

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 15, 2012

    Wewe Bwege Anonymous wa Thu Jun 14, 08:30:00 PM 2012

    Unafikiri Anonymous wa tatu (3) hapo juu Thu Jun 14, 02:50:00 PM 2012

    Eti nini?...wewe usiye na gari?

    KWA TAARIFA YAKO KAMA ULIVYOSIKIA KTK HOTUBA YA BAJETI INAYOENDELEA BUNGENI DODOMA KUHUSU USAJILI WA NAMBA ZA MAGARI KWA MAJINA YA WATU JAMAA NAMBA YAKE ANAYO TAYARI NDIO WATU WA KWANZA KUPATA INGIA TRA SITE TATUFA UONE NAMBA YA GARI HAPA CHINI:

    TDAR ERIC MUSHI

    MSIFIKIRI KILA ANAYETOA COMMENT ZA KUKOSOA WATU HUMU NAE NI MASIKINI SIYO HIVYO!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 15, 2012

    Puuu hela ya bahati Mil. 15 mkononi unawahi ktk Mtandao au Yadi kuchagua gari!

    Kwala kacha unauparamia mtumba mbovu unawaka moto kama hivi.

    Mmeona matokeo yake?

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 15, 2012

    Tutakatae tusikatae Wabongo tuna 'aleji' ya kupenda magari!

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 15, 2012

    Thamani ya gari bora angenunua shamba !

    Mola amsaidie awe na Bima ya maana labda atapona kama sivyo akiwa na Bima za 'nusu andazi' asalaleee atalipwa Laki 2 presha itampanda!

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 15, 2012

    Pana watu majasiri sana kwa kuendesha magari bila bima kabisa au bima kiduchu au muda wake umekwisha!

    Hivi ktk mazingira kama haya inakuwaje?

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 15, 2012

    Ninyi wote mnaobisha hapo juu ndio hamkustahili kuwa na 'priority' za kununua magari 'used' badala ya mapya mli fosi king !,

    Ninyi wooote wabishi hapo juu ndio mlistahili 'priority' ya kwanza kufungua Magenge ya Dagaa na Bamia kwa (Laki mbili) mlipopata kwa mara ya kwanza Mil. 10 ya bahati mbakishe Mil. 9.8, badala ya kukurupukia kununua magari 'used'

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 15, 2012

    Duhhh ni kipande cha Mkaa!

    Bosi ndio amekwisha ukalia!

    Si ndio awasiliane na Wakala wake alikonunua?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...