Baadhi ya Wahariri wa Vyombo mbali mbali vya Habari hapa nchini wakijiandaa kushusha jeneza lenye mwili wa Mhariri wa Gazeti la Jambo Leo,Marehemu Willy Edward Ogunde aliefariki dunia mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro.Shughuli ya kuaga Mwili wa Marehemu Willy imefanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar na baadae ikafuatia safari ya kwenda Nyumbani kwao Mara kwa Mazishi.
Mchungaji akiongoza ibada ya Kuaga Mwili wa Marehemu Willy Edward leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Prof. Ibrahim Lipumba akitoa heshima zake za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Willy Edward ambaye alikuwa Mhariri wa Gazeti la Jambo Leo aliefariki ghafla huko mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.Hafla hii ya kuaga imefanyika mchana huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginald Mengi akitoa heshima zake za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Willy Edward ambaye alikuwa Mhariri wa Gazeti la Jambo Leo aliefariki ghafla huko mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM),Nape Nnaupe akitoa heshima zake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...