Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiwa na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Lu Youqing (katikati) na Afisa kutoka Ubalozi wa China Bw. Ouyang Zhibing (kulia) wakati Balozi huyo wa China alipomtembelea Waziri Magufuli ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiwa na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Lu Youqing (katikati) na Afisa kutoka Ubalozi wa China Bw. Ouyang Zhibing (kulia) wakati Balozi huyo wa China alipomtembelea Waziri Magufuli ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiwa na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Lu Youqing (katikati) na Afisa kutoka Ubalozi wa China Bw. Ouyang Zhibing (kulia) wakati Balozi huyo wa China alipomtembelea Waziri Magufuli ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli leo amekutana na Balozi wa Jamhuri wa Watu wa China hapa nchini Mheshimiwa Lu Youqing wakati balozi huyo alipotembelea Wizara ya Ujenzi hapa jijini Dar es Salaam.

Katika mazunguzo baina yao Mheshimiwa Lu Youqing alisisitiza dhamira ya nchi yake kuendeleza ushirikiano na Tanzania kutokana na historia ndefu ya ushirikiano huo ambao ameuelezea kuwa ni wa damu hasa kutokana matukio yaliyojitokeza wakati wa ujenzi wa reli ya TAZARA ambapo baadhi ya wafanyakazi wa Kichina waliofariki wakiwa kazini walizikwa hapa hapa Tanzania.

Mheshimiwa Magufuli kwa upande wake alimshukuru Balozi huyo kwa kufika ofisini kwake na kumhakikishia kuwa Wizara ya Ujenzi itaendelea kuenzi mahusiano hayo mazuri ikiwa ni pamoja na kuyapa ushirikiano makampuni ya Kichina yanayotekeleza shughuli za ujenzi hapa nchini.

Waziri Magufuli alimwelezea Balozi huyo kuwa kwa hivi sasa Wizara ya Ujenzi iko katika mkakati wa kukabiliana na ongezeko la msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam na pia katika barabara inayounganisha Bandari ya Dar es Salaam na nchi zinazopakana na Tanzania kwa upande wa Magharibi. Mheshimiwa Magufuli alibainisha kuwa tayari taratibu za awali zimeanza za kutafuta wawekezaji wa kujenga barabara mbadala katika sehemu inayounganisha jiji la Dar es salaam kupitia Chalinze hadi Morogoro.

‘Hii ni fursa nzuri kwa makampuni ya Kichina kuona namna ya kushiriki katika mchakato huo ambao unakusudia kutumia utaratibu wa kushirikisha sekta binafsi katika uwekezaji huo’ alibainisha Waziri Magufuli.

Naye Balozi Youqing alimfahamisha Waziri Magufuli kuwa China iko tayari kuanzisha mpango wa pamoja wa kubadilishana wataalam ili kuongeza ujuzi katika sekta hii ya ujenzi na kwamba kwa sasa hivi yapo makampuni ambayo yako tayari kuingia ubia na makampuni ya Kitanzania kwa ajili ya kutekeleza kazi za ujenzi.

Ubalozi wa China pia unakamilisha maandalizi ya kufanyika kwa mkutano utakaokutanisha makampuni yote ya Kichina yanayotekeleza kazi za ujenzi hapa nchini ili kukutana na Wizara ya Ujenzi kwa lengo la kupata tathmini ya utendaji wao kwa upande wa ubora wa kazi na mikakati ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa kizalendo wanaoajiriwa na makampuni hayo.

Waziri Magufuli alihitimisha kwa kumhakikishia balozi huyo kwamba Serikali tayari imekwishatenga kiasi cha Shilingi bilioni 335 kwa ajili ya kulipa madeni ya makandarasi wanaodai hadi sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2012

    Daraja la kigamboni ujenzi wake umefikia wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...