

Hii imetokea Jana jumamosi asubuhi majira ya saa tatu asubuhi baada ya gari ya kampuni ya Kanji Ladji inayobeba bia iliokuwa inatokea Mbeya kwenda Sumbawanga ikiwa imesheheni vinywaji kupata ajali na kuanguka majira ya saa tatu asubuhi.
Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi..... baada ya ajaali hiyo kutokea kijiji cha Mshani zipatazo km 19 kutoka Laela-Sumbawanga ilikuwa kama sherehe kwa wengine kwani wanakijiji walivamia gari na wakaruhusiwa kunywa watakavyo ila hakuna kuondoka na chupa..... asubuhi watu walikuwa wamelewa chakari...


I hope that the driver is OK, and no one was injured during this accident.
ReplyDeleteDr Gangwe Bitozi.
Sumbawanga si mkoa, ila ni wilaya iliyo mkoani Rukwa
ReplyDeletehahahaha daaah hii nimeipenda wadau eti "kunyweni hapa hapa ila msiondoke na chupa" daaah na wanakijiji walitii bila shaka thats very good.
ReplyDeletesasa ingetokea dar uone yani japokua utawaambia hivyo lakini watasepa na chupa na kreti vile vile.
tuhurumie na hawa wanaopata ajali jamani, heri nusu hasara kuliko hasara kamili.
--Mtoto wa kiswahili.!!
Sumbawanga ni mji na Wilaya iliyo katika Mkoa wa Rukwa ,kama mdau hapo juu alivyoelezea,shukrani kwa taarifa Mkuu
ReplyDeleteafadhali maana pombe ni haramu jamani
ReplyDeletehehehehehe wacha walewe chakari ukute walizoea kunywa chimpumu sasa wameona bia za bure kwi kwi kwi kwi kwi kaaaaaazi kweli kweli
ReplyDeletewatu walikuwa tilalila.....hahahaha! na sisi watanzania tunavyohusudu pombe, ilikuwa sherehe kabisa
ReplyDelete