Hii imetokea Jana jumamosi asubuhi majira ya saa tatu asubuhi baada ya gari ya kampuni ya Kanji Ladji inayobeba bia iliokuwa inatokea Mbeya kwenda Sumbawanga ikiwa imesheheni vinywaji kupata ajali na kuanguka majira ya saa tatu asubuhi.
 
 Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi..... baada ya ajaali hiyo kutokea kijiji cha Mshani zipatazo km 19 kutoka Laela-Sumbawanga ilikuwa kama sherehe kwa wengine kwani wanakijiji walivamia gari na wakaruhusiwa kunywa watakavyo ila hakuna kuondoka na chupa..... asubuhi watu walikuwa wamelewa chakari...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 25, 2012

    I hope that the driver is OK, and no one was injured during this accident.
    Dr Gangwe Bitozi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 25, 2012

    Sumbawanga si mkoa, ila ni wilaya iliyo mkoani Rukwa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 25, 2012

    hahahaha daaah hii nimeipenda wadau eti "kunyweni hapa hapa ila msiondoke na chupa" daaah na wanakijiji walitii bila shaka thats very good.

    sasa ingetokea dar uone yani japokua utawaambia hivyo lakini watasepa na chupa na kreti vile vile.

    tuhurumie na hawa wanaopata ajali jamani, heri nusu hasara kuliko hasara kamili.

    --Mtoto wa kiswahili.!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 25, 2012

    Sumbawanga ni mji na Wilaya iliyo katika Mkoa wa Rukwa ,kama mdau hapo juu alivyoelezea,shukrani kwa taarifa Mkuu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 25, 2012

    afadhali maana pombe ni haramu jamani

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 25, 2012

    hehehehehe wacha walewe chakari ukute walizoea kunywa chimpumu sasa wameona bia za bure kwi kwi kwi kwi kwi kaaaaaazi kweli kweli

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 25, 2012

    watu walikuwa tilalila.....hahahaha! na sisi watanzania tunavyohusudu pombe, ilikuwa sherehe kabisa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...