Naibu Katibu Mkuu Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimia na watanzania waliohudhuria hafla ya kusherehekea mafanikio yake katika kipindi cha Miaka Mitano na Nusu ambayo amekuwa Naibu Katibu Mkuu,Umoja wa Mataifa iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini New York,Marekani. Katika baadhi ya mambo aliyowasisitizia watanzania ni pamoja na kufanya kazi kwa nidhamu na kulinda, kuenzi na kudumisha amani, umoja na mshikamano.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Mwanaidi Maajar akiwakaribisha wageni pamoja na kutoa wasifu wa Mhe. Dkt. Asha- Rose Migiro , Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, wakati wa hafla ya kusherehekea mafanikio ya Dk. Migiro katika kipindi cha Miaka Mitano na Nusu ambayo amekuwa Naibu Katibu Mkuu.
Naibu Katibu Mkuu Asha- Rose Migiro na Balozi Maajar wakipakua chakula, kati ni Dada Rozi Mkapa akiwaelezea menu iliyokuwa imeandaliwa siku hiyo.
Naibu Katibu Mkuu akicheza muziki na mtoto Ronald Magoha.
Na mduara nao ulichezwa, Naibu Katibu Mkuu mwenye nguo nyekundu hakuwa nyuma katika kuucheza mduara.
Kaeni mkao wa picha, ndivyo anavyooneka kusema Bw. Saleh wakati wa upigaji picha ya wafanyakazi wa Ubalozi za Washngton na Umoja wa Mataifa wakiwa na Naibu Katibu Mkuu na Balozi Maajar na Balozi Manong.
Naibu Katibu Mkuu na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, na Balozi Tuvako Manongi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...