Mmoja wa Makuli wa kupakia mifuko ya Saruji kwenye malori kutoka kiwanda cha saruji,Wazo jijini Dar akiwa ameuchapa usingizi mzito nyuma ya lori hilo lililokuwa linatembea katika barabara ya Sam Nujoma,Jijini Dar.Ulalaji wa namna hii ni hatari sana kwa maisha yake kwani linaweza tokea lolote kwake,japo hatuombei litokee.
Home
Unlabelled
Usingizi Mzito.....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
poa tu raha jipe mwenyewe au unataka alale kwenye mashangingi? kwani yeye mbunge?
ReplyDeletehuyo ni masikini mtaji nguvu zake ana raha gani ya kuishi? waache hao wabunge wale maisha na mafisadi lakini kina sisi hata tukifa hatuna neno.
Pole Bwana kaka na msukosuko wa wimbi la maisha!
ReplyDeleteHapa ndio yale mazingira Kibarua kinakuwa ni cha kufukuzia, huku ukipata inakuwa ni zamu za usiku tu hadi asubuhi!
Kwa mtaji huo sio ndio haya ya kulala juu ya gari tena?
Duhhh jamani kiumbe wa Mwenyezi Mungu anateseka na mshike mshike wa maisha Duniani!
ReplyDelete1.Hapo ndoto zake ktk usingizi huo juu ya Lori anaota ameshafariki yupo ndani ya kaburi!
2.Kama akiota yupo hai anaota anaanguka kutoka juu ya pango kwenda bondeni!
3.Kama akiota ana afadhali yupo ktk ndoto akiwa ktk kazi ngumu kama kubeba zege kwa kuwa yupo juu ya mavumbi ya simenti!
4.Akiota anajuta, atakuwa anajuta kwa nini hakuzaliwa Mbunge au Fisadi?
5.Akiota anakula, ni kuwa anakula mavumbi na mawe kwa vumbi la simenti linavyomwingia puani!
Ndio maana Bob Marley aliimba,,,
''So much trouble in the world X 3''
Ahhh maisha ya namna hii yana raha gani tena?
1.Kukosa usingizi sawasawa,
ReplyDelete2.Kazi ngumu na ya suluba,
3.Dishi la kubabaisha,
Kulingana na aina ya kazi kama hii maisha yake yanazidi kuwa mafupi kwa miaka zaidi ya 10 hivi!
Wasi wasi wako tuu mbona hamna shida hapo jamaa yupo makini kuliko unavyofikiria.
ReplyDelete