Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamisi Kagasheki akiteta jambo na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,Mh. Lazaro Nyalandu.
Wizara ya Maliasili na Utalii inatoa taarifa kuwa hakuna ugomvi wowote kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamisi Suedi Kagasheki na Naibu Waziri Mhe. Lazaro Nyalandu. Mawaziri hao wanafanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu na hakuna mgogoro wowote kati yao.
Tarifa hii imetolewa kutokana ma habari iliyoandikwa na gazeti moja la kila wiki nchini ambalo katika toleo lake la tarehe 19/06/2012 lililoandika: “MAWAZIRI WAGOMBANA”.
Habari hiyo inataja kuwa Naibu Waziri alizungumza na baadhi ya watendaji wa TANAPA na kusema kuwa “Waziri alikurupuka’’ pale alipowasimamisha kazi baadhi ya watumishi waliotuhumiwa kuhusika na mauaji ya faru. Habari hiyo inataja pia kuwa Mhe Nyalandu aliyasema hayo kwenye kikao cha kusuluhisha mgogoro kati ya TANAPA na Kampuni ya Otterlo Business Corporation Ltd. (OBC).
Wizara inakanusha habari hizo na kusisitiza kuwa hakuna ukweli wowote katika habari hiyo na kuwa haina msingi.
Mheshimiwa Nyalandu hajawahi kufanya kikao na TANAPA kusuluhisha mgogoro kati ya Shirika hilo na Kampuni ya OBC kama gazeti lilivyoandika. Aidha kampuni ya OBC haina mgogoro wowote na TANAPA wala shughuli zake hazihusiani na zile za TANAPA.
Vilevile Naibu Waziri hajawahi kutamka wakati wowote kuwa “Waziri alikurupuka” na hata mwandishi wa habari hiyo alimnukuu Mhe. Nyalandu akikanusha kusema hivyo.
Izingatiwe kuwa Mhe. Nyalandu hajawahi kugombana na Mhe. Kagasheki na kuwa taarifa hiyo ya uzushi haitasababisha ugomvi kati yao.
Michuzi umeanza kuuza chai? Hii taarifa ni nyepesi mno,tofauti na ile ya gazetini. Haijatosheleza kujibu maswali yaliyoletwa na taarifa ya gazeti. Hivyo walete maelezo zaidi ya kutosheleza.
ReplyDelete