Aliyekuwa mgombea ubunge kwa Tiketi ya CCM, Hawa Ng'umbi (pichani kulia) leo amewasilisha hati ya nia ya kukata rufaa katika mahakama ya Rufaa.
Kusudio hilo limewasilishwa leo na wakili wake Mh. Issa Maige baada ya Mahakama Kuu Kanda ya dar es Salaam kutupilia mbali kesi hiyo na kumpa ushindi mbunge wa jimbo hilo kupitia CHADEMA, Mh. John Mnyika (pichani kushoto).
Madai ya Ng'umbi yalikuwa ni kuwa uchaguzi wa Jimbo la Ubungo ulikuwa ni batili kwa sababu haukuwa huru na haki, mbali na hilo taratibu za uchaguzi zilikiukwa kuna baadhi ya fomu hazikujumlisha matokeo.
Alikuwa anadai Mh Mnyika aliingiza Laptop kwenye chumba cha kuhesabia kura na alizitumia laptop hizo kujiongezea kura, na kwamba Mnyika aliingiza watu watano katika chumba cha kujumlishia kura wakati watu hao walikuwa hawahusiki.
Madai mengine ni kuwa Mh. Mnyika alimtolea maneno ya kashfa kwa kumwita fisadi alipokuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake(CWT) Wilaya ya Kinondoni, na kuwa aliuza nyumba za jumuiya hiyo, na kwamba kuna kura zilizoongezeka.


Kweli asiyekubali kushindwa.......!
ReplyDeleteMheshimiwa Hawa anawapenda MNO, MNO MNO wananchi wa Ubungo!. Je, na nyie wananchi mnampenda vivyo hivyo?
ReplyDeleteHuo ni uongo mtupu kama anapendwa mbona asipite lol... huo ni unafiki acha vijana wajanja wachape kazi huyo ngumbi anatuletea nini kipya katika eneo letu la ubungo. Wewe tuliza ball kanda isonge mbele ha ha haaaa
ReplyDeleteMama Hawa kama una moyo wa kusaidia wananchi wa Ubungo bado una nafasi ya kufanya hivyo si lazima uwe mbunge. Hizi kesi zisizoisha hazina tija yoyote kwa sisi wananchi ni kupotezeana muda tu. Tuwaache majaji wafanye kazi nyingine zenye maslahi na taifa hili
ReplyDeleteIla tafadhali sana Hawa angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.
ReplyDeleteWewe Mama nenda kalime au omba mkopo Saccos ukaanzishe mradi huku ukisubiri chaguzi ujao 2015!
ReplyDeleteAcha kurudi Mahakamani kwa kuwa unaumbuka bure tena unaumbuliwa na dogo Mparare mwenzio John Mnyika!
Hii ndio Siasa ya tija kweli?
Tafadhali tafadhali tafadhali, serikali tunaomba utupilie mbali hii kesi, kwani ni upotezaji wa hela ya wananchi, tunajua kwamba hata uchaguzu urudiwe leo Mnyika atashinda tu.
ReplyDeleteSII UTULIE TU!!!!!!HOJA ZAKO HAZIKIDHI NDIO MAANA JAJI ALITUPILIA MBALI. TAFUTA KITU KINGINE CHA KUFANYE CHENYE KULETA MAENDELEO KULIKO KUANZA TENA KESI.
ReplyDeleteasiyekubali kushindwa si mshindani.. hajuikama siasa ni game,mbona mwenzake SHy rose amesota miaka mingapi mpaka saivi Mungu amemwona kwenye ubunge east Africa, huyu mama anabore.sio great thinker haoni hata kama atashinda kesi serikali itatoa tena fedha nyingine kwa ajili y a uchaguzi mwingine? tulia mama angalia fani nyingine usituletee kichefu chefu.
ReplyDeleteMambo ya Mgombe Ubunge kupeleka compyuta katika kituo cha kupigia kura nyie mnayaona sawa. Hivi vikifanya vyama vingine itakuwa sawa. Ubungo wengi ni wahamiaji.
ReplyDeleteHawa Ngumbi bado una nafasi ya kugombea tena 2015 jaribu bahati yako kipindi hicho kwani muda umebaki mchache kipyenga kipulizwe tena achana na makesi yasiyokuwa na faida kwa taifa.
ReplyDeleteBIASENESS IMEJAA ACHENI! ANA HAKI YAKE NA ANATUMIA UHURU WAKE MWACHENI AKISHINDWA NDIYO ATAJIFUNZA KAMA KWELI KAKOSEA.
ReplyDeleteHiyo ndiyo Demcrasia kuweni wavumilivu jamani!
Hakuna cha demokrasia wala nini mambo mengine ni kukubali tu yaishe we mwanamke mwenzetu maisha si ubunge tu kuna mambo mengi waweza kufanya hata bila kuwa mbunge na ukawapa faida wananchi kama ndo unalotaka lakini kwa mwendo huu nadhani utakuwa ulimwaga mihela mingi sasa unataka njia ya rahisi kuzirejesha ambayo ni bungeni tu ukapewe limkopo likubwaaaaa pole mama kubali tu kuwa ulishashindwa karibia tunaingia elfu mbili na 13 only 2yrs left utagombea tena kha hadi unaboa. Huyo wakili wako keshajipatia pa kumalizia mahitaji yake madogo acha ajiliage hela kwa kukudanganya kuwa utafanikiwa kama hutujui mawakili ndo ivo hata mimi ningekuchezesha hilo ligwaride tukate rufaaa hadi international court mi najilia hela tu nashida gani
ReplyDeleteKwani ni uongo nyumba si mliuza kweli.
ReplyDelete