Anko Michuzi,

Kwanza nakushukuru kwa kutokuwa na ubaguzi wa dini wala kabila katika kurusha hoja za wadau.

Naomba unirushie kwenye blogu yako hoja yangu kuhusu swala la dini kwenye sensa ya taifa. 

Nionavyo mimi jukumu la serikali ni kujua idadi ya watu wake kwa ajili ya mipango na mikakati ya nchi, kama afya, elimu, ajira,taaluma, makazi n.k. 

Si jukumu la serikali kujua waumini wa dini fulani wako kiasi kadhaa. Kama kuna dini yoyote yenye mashaka na idadi ya waumini wake basi waitishe sensa ndani ya nyumba hizo tukufu za imani na kuhesabu waumini wao. 
 
Kwa mfano tukijua kuna waumini kadhaa wa dini fulani mwaka 2012, Je tuna uhakika gani kwamba namba hiyo haitabadilika baada ya mwaka au miaka kadhaa? Inajulikana kwamba watu hubadili imani zao  za dini na ni kwa sababu hiyo basi ni rahisi zaidi kujua idadi ya waumini waliopo kwa kuwahesabu ndani ya nyumba za kuabudu kuliko kutegemea serikali kufanya hivyo.

Serikali ikianza kuweka kipengele cha dini kwenye mambo ya sensa  basi wapo wale watakaohitaji makabila pia yajulikane mwisho ni yale yalee ya kubaguana kikabila na kidini.

Mimi binafsi napinga ubaguzi wa aina yoyote ile, iwe ni wa dini, kabila, jinsia au rangi, kipato au elimu.

Familia za kitanzania zimechangayika dini tofauti makabila tofauti, hesabu hizi za kidini zinaweza kuvunja familia. Ni watanzania wangapi wanaweza kusema ukoo mzima wanaimani moja ya dini? Je ukihesabu wakristo kwa mfano utawagawanya kwa makanisa? Na waislamu je? Wahindu? Wasabato? Jehova witnesses? Na wengineo wengi. Kazi ipo! 

Kwangu mimi dini ni imani ya mtu binafsi. Ni mahusiano kati ya mwanadamu na muumba wake. Serikali haina nafasi katika hili. Na yeyote mwenye mawazo mazuri na mipango ya kuimarisha waumini wa dini fulani basi aielekeze kwenye nyumba za ibada za dini hiyo, mashule, vyuo n.k, hili limekuwepo miaka mingi tu.  Ukitaka kujua waumini wa kweli wa dini fulani basi wasiliana na viongozi wa dini hiyo au nenda kwenye nyumba ya ibada. 
 
Dini moja isiruhusiwe kutoa takwimu za dini zingine kwani hiyo si kazi yao.

Viongozi wa nchi wachaguliwe na kuteuliwa kwa CV zao na sio imani za dini.

Nawasilisha
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 15, 2012

    halafu kuna watu ni wakristo au waislam lakini hawaendi kanisani wala msikitini, sasa itasaidia nini kusema nina waumini 200 while wanaokuja au mnaojumuika kuabudu ni 10? mimi nimeona kanisa katoliki wanahesabu waumini wao kupitia jumuiya, kigango , parokia jimbo hadi taifani kwa ajili ya matumizi ya kanisa pekee na si mahitaji ya kisiasa, kiuchumi, au kijamii. kwa hiyo sidhani kama kipengele cha dini kwenye sensa ni muhimu kwa sababu lengo la sensa ni kujua watu wako wangapi kwa ajili ya kuboresha huduma za jamii lakini pia kwa maswala mengine ya kitaifa na kiuchumi pia. Hakuna sehemu itakuja kutokea eti kuna wakatoliki kumi wanahitaji huduma za afya pale, bali itakuwa mtaa fulani unahitaji huduma fulani.
    Halafu wale wapagani inakuwaje kwenye hili? ujue haya maswala ya dini haya yanaweza hata kuleta unyanyapaa kwa kunyoosheana vidole yule mpagani etc.
    Ni hayo tu naunga hoja ya mdau sina nia ya kumkwaza mtu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 15, 2012

    Unacho kinena kizuri mtoa mada.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 15, 2012

    Mtoa hoja uko sahihi kabisa. Binafsi nimesikitishwa sana na hoja ya Bakwata. Inaonekana wanaweka mbele zaidi uislamu bila kuangalia athari za hicho wanachokitaka.

    Hivi ukishajua dini fulani ndo wako wengi zaidi nchini, inakusaidia nini ktk maendeleo ya nchi yako? au wanataka wapate point ya kuombea misaada?

    Jamani Bakwata acheni hoja zisijo na tija ktka maendeleo ya taifa letu. Kwa kila hoja tuwe tunazingatia kwanza umoja na mshikamano wa kitaifa tulionao ktk nchi yetu. Maslahi binafsi tuweke pembeni, chonde chonde!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 15, 2012

    Nchi ya Tanzania ni ya Watanzania wote hili halina mjadala.Na matatizo yeyote ya nchi yanatatuliwa kwa kuangalia uhalisia, ikimaanisha jamii inataka nini.Kuna taasisi nyingi tu zimetajwa na wadau waliochangia mada hii ya sensa kuweka kipengele cha dini kwamba wanatumia takwimu kuonyesha Watanzania wapo kiasi gani kulingana na imani (dini) zao. Zilizotajwa ni za serikali na za watu binafsi. Ngoja nikukumbushe kwa kunakili kutoka kwa wachangiaji waliopita, waliweka taarifa hii iliyotolewa kwenye gazeti la HabariLeo:


    "Na mfano halisi uliotolewa na Shehe Ponda akinukuu vyombo vilivyotoa takwimu hizo ni tovuti ya Wakatoliki inayoonesha kuwa mwaka 2008 Waislamu walikuwa asilimia 34, Wakristo asilimia 44 na Wapagani asilimia 22
    Aidha, akaitaja Televisheni ya Taifa (TBC) ambayo hivi karibuni iliripoti kuwa Waislamu ni asilimia 32, Wakristo asilimia 52 na Wapagani asilimia 16 wakati Idara ya Uhamiaji ikionesha kuwa mwaka 2010 Waislamu walikuwa asilimia 35, Wakristo asilimia 32 na Wapagani asilimia 33.Pamoja na hayo, alisema pia chapisho la Serikali la Ramani ya Taifa linaonesha kuwa mwaka 2011 Waislamu walikuwa asilimia 35, Wakristo asilimia 45 na Wapagani asilimia 20."

    Nami nikaingia kwenye tovuti ya habari leo nikaona hiyo habari. Unaweza kuingia kwenye hii tovuti ya habarileo:

    http://www.habarileo.co.tz/index.php/wazo-langu/711-sakata-la-sensa-lishughulikiwe-kwa-busara

    Kwa mwenye akili atajua kwamba jamii ya Kitanzania inahitaji kujua idadi ya watu kulingana na dini zao pia. Kama wasingetaka tusingeona taasisi za serikali zikitumia takwimu zisizo rasmi ilhali wanafahamu hakuna sensa rasmi iliyofanyika.

    Kwa haraka haraka utajua kuwa hawa watu wametoa tarakimu za mwanzo ili kuweza kutafuta tarakimu yenyewe iliyokuwa ya ukweli. Nafikiri kama umepitia chuo kikuu na ukasoma hesabu zinazoitwa "Numerical Methods" mfano "Point Gauss-Seidel Method", utaona inafana na jinsi taasisi hizo zilivyofanya, yani unaanza na tarakimu ya mwanzo isiyokuwa ya kweli unaingiza kwenye kanuni na baada ya marudio kadhaa unakuwa umefikiwa kwenye tarakimu ya ukweli ambayo inamapungu machache (MINIMUM ERROR).

    Kwa hiyo basi, ili tuweze kupata jibu la uhakika ni lazima tuweke kipengele cha dini kwenye sensa hii.Haina gharama yeyote, ni kuweka tu sentensi na sehemu ya kujaza (mstari mmoja unatosha).

    Na nilifuatitilia mchangiaji mwingine alitaja kwamba serikali imeanzisha vitambulisho vya taifa na kila Mtanzania atawekewa kila linalomhusu yeye. Ameoa wapi, anafanya kazi gani, alimaliza shule wapi, ana dini gani, n.k., na hili zoezi kwa mbeleni litafanyika kwa kila kichanga kitakacho zaliwa. Manake ni kwamba serikali haitafanya sensa YA "MANUAL" tena, itakuwa kwa kheri. Nafikiri kama upo Tanzania unaona juhudi ya serikali kutandaza mkonga wa taifa ufike kila wilaya na ikibidi vijijini. Manake taarifa zetu zote zitawekwa kwenye SERVER na zitakuwa UP-TO-DATE.

    Sasa kama huko huko mbeleni kwa kutumia vitambulisho vya taifa kipengele hicho cha dini hakitakwepeka kwa nini tusiwe na kipengele cha dini sasa hivi pia??? Tatizo liko wapi??? Tusiwe na mawazo ya kizamani ya kudhania dhania, inabidi tufanye kisayansi.

    Kama kweli tunataka nchi hii iendelee tuache kudhania dhania. Mfano, kuna mchangiaji aligusia kuhusu ujaji wa vyama vingi vya siasa. Wakawa wanasema kutatokea vita kama vyama vingi vya siasa vikiruhusiwa. Ile ilikuwa dhana tu, siyo "SCIENTIFIC FACT". Tunamshukuru Muumba kwa hilo haijatokea na tuendelee kuliombea Taifa letu liendelee kuwa na amani, cha msingi tu haki itendeke kwa kila raia.

    Kwa hiyo suala la sensa liwe pia na kipengele cha dini, hakuna sabubu za msingi za kisayansi ya hicho kipengele kutowepo. Wengi wanadhania tu, hawaendi kisayansi kabisaaa.

    Naomba niishie hapo, nitaelezea zaidi kadri nitakavyoona wachangiaji wengine.Manake watu wanasema kumwelimisha mtu inachukua muda mpaka akaelewa.Manake wengine wanang'ang'ania kitu kwa ajili ya nafsi yao tu si kwa kuangalia uhalisia wa jambo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 15, 2012

    hoja yako kidogo ni nyepesi wala haina uzito wowote..tunachosema ni kwamaba hawa wanaojiita wakristo wanaumoja na serikali na wanapewa upendeleo maalum kisa wao ni wengi na wanataka kile wanachokipenda wao ndio serikali ikifanye..tunataka usawa kwa kila idara serikalini, sio makanisa wanapewa fungu waislam hawapati..tujue waislamu wako wangapi na wakristo wangapi halafu serikali kama itagawa mafungu kulingana na imani basi kuwe na usawa na pia ikiamua kutogawa hayo mafungu itakuwa sio mbaya sana...nakuuliza wewe uliyetoa hoja, hivi wakristo kwa nini mnaogopa sana na kupinga kila kinachotakiwa na waislamu?..mnawaogopea nini?..mahakama ya khadhi inawahusu?,mbona mlipinga sana isiwepo kwa nn?...kulikoni nyie makafiri!..
    hebu waacheni waislamu wapumue kwa kuondoshewa yale mnayowadhulumu kupitia mgongo wa serikali..na hata hivyo dawa yenu inachemka sana sana sasa hivi,karibuni mtainywa...

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 15, 2012

    Usijidanganye ndugu,kila kinachofanywa Tz kilishawahi fanywa nchi nyingine,sio kwamba ndio kinaanza hapo, utaratibu huu upo Dunia nzima wacha uoga wa kijinga na mlolongo mreefu come on!!!!Ni utaratibu wa kila mahari huu usijali hata wakiisabu hisabu zitawekwa sawa kama unavotaka ok? what about if i tell you waislam na wakristo wapo idadi sawa won't you be happy then?

    ReplyDelete
  7. Tukipata watu wenye busara na hekima kama wewe tutafika mbali kimaendeleo....
    Matabaka na kujigawa kwa aina yoyote ni kujijengea chuki katika nchi yetu.Mungu atulinde kwa mabaya na tupendane bila kubaguana.
    Maganga One.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 15, 2012

    HOJA DHAIFU KABISA: KUJUA WATU WA DINI FULANI NI WANGAPI KUNAONDOAJE MSHIKAMANO? MBONA UKIULIZWA WEWE NI MME/MKE KATIKA HISABU YA DINI UTASEMA KIPENGELE HICHO KINAVUNJA JINSIA ZA WATU COZ WATU WAMECHANGANYIKANA KTK JINSIA TOFAUTI???
    JAMBO LA MUHIMU KTKT HOJA HII NI KWAMBA KWAMBA KWA NINI TAASISI NYINGINE ZINARUHUSIWA KUTOA MATAMKO YA IDADI ZA WATU? BILA YA SERIKALI KUTOA TAMKO LOLOTE LA KUKEMEA MATAMKO HAYO PAMOJA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI VYA SERIKALI KAMA TBC1. HIYO NDIO SABABU ILIYOFANYA WATU WADI KIPENGELE HICHO

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 15, 2012

    Mwandishi:

    Unadumisha fikra halafu unajidai eti uonavyo, huna mboni wewe, umeonewa. utetezi kwamba serikali haijengi miskiti au makanisa ni hoja ya Mwl. Nyerere, lete yako nawe tukusikie. Elimu za kudesa.

    Kama idadi ya imani hubadilika kwa kubadili, mbona isiyo ya imani hubadilika kwa kufa na kuzaliwa, na uhamiaji, hivyo hamna haja ya kuhesabu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 15, 2012

    Kama kweli we ni mpinzani wa ubaguzi, umeshatoa maoni kwamba ubaguzi utambuliwe kisheria kuwa ni jinai na wabaguzi wafungwe au laa.

    Kama hutoi maoni basi we ni wale waso vitendo kwani hata katiba yetu inalaani tuu lakini haizuii mtu yeyote kubagua kwani si jinai.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 15, 2012

    Kisheri:

    Ubaguzi si jinai ila ni kitu kibaya kwani huleta madhara. Si jinai kwa sababu sheria zetu hazina procedure wala adhabu ya kushughulikia wabaguzi, inalaani tuu, helplessly.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 15, 2012

    Yaani nchi yetu ni ya utawala wa sheria lakini hakuna sheria ya kuwabana wabaguzi, inaishia kulaani tuu, laana hazisaidii, vitendo ndo muhimu.

    maneno matupu (laana) hazivunji mfupa.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 15, 2012

    SERIKALI INA NAFASI KATIKA DINI.

    Mfano:
    1. Wimbo wa taifa ni sala. Mungu ibariki.......

    2. Bunge lina sala


    3. Viongozi wa dini huitwa kufanya sala kwenye sherehe za serikali kama ya mashujaa nk.


    Nashangaa huo usekyula uko wapi.

    we jamaa ni mfuasi wa fikra, we si kiongozi.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 15, 2012

    Hapa uk katika form za sensa ipo sehemu ya dini na hata una asili gani? nafikiri kwa vile haya mambo yameanzia na hawa jamaa ndio maana na sisi tunawafuata wao .Pia ukijua idadi ya watu fulani au dini gani basi hata huduma utajua ni watu gani wanahitaji kiasi gani.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 15, 2012

    fresh sana ujumbe wako umefika na ni wa busara sana lakini kumbuka kuna dini fulani ambaya imebaguliwa toka long long time ago ndo maana wafuasi wake wakaamua wakataka sensa ingizwe dini kwa sababu dini inginewe ilikuwa inakataza isichanganye siasa na dini wakati wakati walikuwa wao wanafanya hivyo huku wakiwafanya wenzao bum bumbu na wenzao hivi sasa wameamka.

    ni kweli dini ni imani ya mtu binafsi kati ya yeye na muumba wake na muuba wako ndo atakaye ku charge siku ya siku lakini watu siku hizi hawataki KUZULUMIWA WALA KUONEWA NA KUBURUZWA OVYOO KAMA WATOTO MAYATIMA

    nchi hii imesema haina dini ila watu/raia wake ndo wenye dini but ukichunguza utaona udini upo so tuache longa longa na kiini macho

    kwa kifupi nakubalia na wewe watu hubadilisha dini zao katika familia kuna wanafamilia wenye dini zaidi ya mmoja lakini hii pia hana maana tuupuze kwamba wanaozulumiwa daima wasifanye kampeni ya kutaka dini iwepo kwenye sensa

    shukran mdau kwa mada yako lakin geuze shilingi upande wa pili na jaribu ku feel wale upande wa pili wa shilingi

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 15, 2012

    Ni kweli serikali haina dini. Lakini dini mbalimbali zina mahitaji tofauti, hivyo suala la dini ni muhimu kuwekwa kwenye sensa. Zoezi la sensa ni kujua idadi ya watu na sifa zao mbalimbali ili kuweza kufanya mipango ya baadae.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 15, 2012

    Hongera sana mdau kwa 'Article' yako ya ukweli! na iliyojaa busara.

    Kwa kweli tusipokua makini suala la dini litaitafuna TZA.

    Imekua jambo la kawaida kwa watu wenye 'elements' za udini kutoa takwimu juu ya waumini wa dini ipi ni wengi na wepi ni wachache.

    Madhara ya jambo hili ni kusababisha mashindano ya kuoa na kuzaa ktk nchi ambayo tayari inazidiwa na watu.

    Wengine wamekua wakihusisha imani zao na elimu, ajira na umiliki wa mali.

    Madhara ya majigambo haya ni kuwafanya wafuasi wa baadhi ya imani waone wanatengwa na kubaguliwa na serikali yao huku ikwapendelea wezao jambo ambalo si kweli!

    Kwa kweli suala la dini TZA kwa sasa ni nyeti kuliko wakati wowote uliopita.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 15, 2012

    Nakubaliana na wewe asilimia 200% Sensa ni kitu sensitive sana; hata huko US inazua debate jinsi wanavyo group watu kwenye sensa zao. Govt shoud be very careful

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 15, 2012

    SERIKALI ISIRUHUSU KABISA MAMBO YA DINI KTK SENSA, KAMA ALIVYOSEMA MWALIMU ANAETAKA KUJUA IDADI YA WAUMINI WAKE ATAFUTE KWENYE MAJUMBA YA IBADA.

    TATIZO KUBWA LA UDINI KTK NCHI YETU LINACHANGIWA NA WATUMISHI WALIOSOMA KTK SHULE ZA KIDINI.

    MIMI NADHANI WAKATI UMEFIKA KWA VIJANA WANAOSOMA KTK SHULE HIZO KUANDALIWA ILI WAMTUMIKIE MUNGU.

    NA WALE WALIOSOMA KTK SECULAR SCHOOLS NDIO WAWE WATUMISHI WA UMMA. MIMI NAAMINI KIJANA ALIE PIKIKA SEMINARY HAWEZI KUWAHUDUMIA WATZA BILA KUTANGULIZA MASLAHI YA DINI YAKE HATA KUWE NA SHERIA ZA AINA GANI!!.

    MIMI MWENYEWE NIMESOMEA HUKO NIMEYAONA KWA SASA SIKO INTERESTED KABISA NA MAMBO HAYO, ANAEPENDA DINI AFANYE KWENYE MAJUMBA YA IBADA AU NYUMBANI KWAKWE SIO MAOFISINI AU KWENYE MAENEO YA WAZI!!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 15, 2012

    Mawili, ama UMELALA au UNAJUA kila kitu isipokuwa unataka tu KUPUMBAZA watu.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 16, 2012

    Uingereza ni nchi ya Kikristo kwa katiba, bendera yao ina Msalaba, Mkuu wa Nchi(Malkia/Mfalme) ni Mkuu wa Kanisa lao (Church of England) na watu wa dini nyingine mbali ya uchache ( Hindu, Uislamu,Mayahudi n.k)ni wa rangi nyingine si weupe kama Waingereza asilia ndiyo maana wanataka kuwatambua hao watu wa dini nyingine (wa rangi nyingine).

    Idadi ya watu weupe Uingereza ni zaidi ya Asilimia 90 ya watu wakaazi ya Uingereza na wana nasaba na tabia za Kikristo hata kama hawaendi makanisani.

    Kwa Tanzania sote asilimia 99 ni weusi(Wakristo/Waislamu/Wapagani) sasa tunataka kujuana dini zetu kwa ajili ya nini?! wakati wote ni weusi asilimia 99?????????????!!!!

    Tusipende kuiga kila kitu kwa vile tu nchi fulani wao kipengele cha dini kimo, kuna mambo mengi yamejificha nyuma ya pazia kama huko Uingereza n.k.

    Mdau
    Jijini London

    ReplyDelete
  22. Kuna upotoshaji unafanyika katika kujadili hili. Waislam wametoa options mbili, lakini mijadala yote inajadili option moja tu. Hii si sahihi. Waislam wanasema 1. Kipengele cha dini kiwekwe 2. Iwapo hakiwekwi, basi serikali ipige marufuku matumizi ya takwimu zisizo rasmi. Mbona kwa kutumia akili kidogo tu inaonekana kuwa wanachokisema ni SAHIHI. Hizo takwimu tunazozitumia zimetoka wapi? kwa sababu kama kuhesabu watu na dini zao ni kutenganisha watanzania basi hao wenye hizo takwimu wanatenganisha watanzania kwa hiyo wapigwe marufuku kutumia hizo takwimu! Mbona jambo jepesi tunataka kulipa uzito usiostahili? hii ni dalili ya kutokuwa na malengo mazuri.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 16, 2012

    nashukuru kwa maoni wadau, lakini ninachoona hapa wachangiaji hawasukumwi na hoja bali wengi wnasusukumwa na udini zaidi. Mimi sioni ubaya wa kujua idadi ya aina ya waumini waliopo nchini. Serikali imekuwa ikisema haina dini lakini ukienda kwenye huduma za kijamii utakuta kipengele cha dini, mfano ukiomba paspoti lazima ujaze kipengele hicho. Nilifikiri wadau wangeanza kupinga matumizi ya Biblia na Qur an kwenye uapishaji wa viongozi kwa sababu serikali haina udini, tutumie katiba kuapa.
    Serikali kupitia vyombo vyake kama TBC visingetoa takwim za wananchi kulingana na dini zao. Kwa nini hizi takwimu zipo nafikiri zina maana kubwa kwa taifa, kwani kama kweli kutatokea hilo tatizo la udini kama wanavyosema wadau serikali itajua wapi pa kuanzia kurekebisha na wapi pa kumalizia.
    Mdau amesema watu wanabadili dini kila siku kwa hiyo takwimu hazitakuwa sahihi, je idadi ya watu nayo si sahihi kwani baada ya sensa watu wanendelea kuzaliwa na kufa.
    Serikali inawategemea sana viongozi wa dini kujenga maadili ya wananchi, wapeni nafasi viongozi wa dini wajue ni kwa kiasi gani wanachangia au wanatakiwa kuchangia kujenga maadili kwa wananchi.
    Naomba kuwasilisha kwa sasa

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 16, 2012

    Umenena mdau wa Uingereza.NI KWANINI TUNAHITAJI TAKWIMU HIZI ZA DINI ZA WATANZANIA? NA JE NI WAUMINI WOTE WANATAKA KUSHIRIKI KWENYE HILI? AU NI YALE YALEE YA WACHACHE KUUSEMEA UMMA? JE NIKIAMUA NISIJIBU SWALI LA DINI NITAKAPOULIZWA, KUNA LAZIMA GANI YA KUJIBU? KUNA UBAGUZI NA UNYANYASAJI WA WAZI UNAFANYIKA TANZANIA KILA SIKU, WA JINSIA, WANAOSHUKIWA UCHAWI, WALEMAVU, [MAALBINO KUUWAWA] WATOTO YATIMA, WAJANE, N.K. KWANINI TUSIELEKEZE NGUVU ZETU KUPAMBANA NA HAYA AMBAYO HAYANA DINI WALA KABILA?

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 17, 2012

    SIKU HIZI NI JAMBO LA KAWAIDA KUONA WAUMINI NI DINI MOJA WANAWATUKANA WAUMINI WA DINI AU DHEHEBU LINGINE HADHARANI, HATA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI KAMA RADIO, TV NA MAGAZET, BLOG NK.

    VIOGOZI WETU WA SERKALI NA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA WANAONA, WANSIKIA, SHERIA ZIPO LAKINI HAKUNA HATUA INACHUKULIWA. UOVU MWINGI TU UNFANYIKA LAKINI KIMYA KAMA VILE HAKUNA MAMLAKA WALA VYOMBO HUSIKA.

    HILI JAMBO LIKIENDELEA LITATUFIKISHA PABAYA SANA. INGAWA SERIKALI HAINA DINI LAKINI KUNA HAJA YA KUWA SHERIA ZA KUDHIBITI VITENDO NA MILOPOKO YA WAUMINI NA VIONGOZI WA DINI.
    MIMI NI MKRISTO LAKINI SIPENDEZWI KABISA NA VITENDO VYA BAADHI YA MADHEHEBU YA KIKRISTO KUTOA WARAKA KWA UMMA WA WATANZANIA, KUTOA TAKWIMU AMBAZO HAZWAHUSU, KUONGEA KAULI ZENYE KUJENGA CHUKI NA FITINA.

    KUHUSU KUWEKA AU KUTOWEKA KIPENGELE CHA DINI KWENYE SENSA, INAGEMEA NA MALENGO YA SENSA, NA UMHIMU WA KIPENGELE CHENYEWE KWENYE MAENDELEO NA MSTAKABALI WA TAIFA.

    JAMBO LA MSINGI KWANZA TUJUE KWA NINI VIPENGELE MBALIMBALI VINAWEKWA KWENYE SENSA eg Majina, jinsia, mkoa, wilaya kata, baloz, elimu, etc. kwa nini vingine haviwekwi? na kwa nini tunafikiri kuna haja ya kuongeza vipengele vingine? Je ni kwa kiasi gani kipengele cha dini kitalisaidia taifa letu. Serikali ikujua islamu wapo 30, wapgani wapo 10, whaindu 12 itasaidia nini? Isipojua hiyo j]kuna hasara gani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...