Na Ripota Wetu
KITUO cha Utamaduni cha Jamhuri ya Irani leo kimewasarifisha vijana wawili wa Kitanzania kwenda nchini Iran kwa ajili ya Mashindano ya Kimataifa ya Kusoma Kuruan yatakayoshirikisha nchi 40.
Akizungumza wakati wa kuaga vijana hao, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema vijana hao wanapaswa kuwa makini katika mashindano hayo kwani wamebeba bebndera ya nchi.
Alisema safari hiyo imegharimiwa na nchi ya Iran ambapo vijana hao wakati wakiwa nchini humo kwa muda wa juma zima huduma zote za kijamii zitakuwa juu yao.
Alhad Salum aliwataja vijana hao kuwa ni Saidi Idd Saidi na Omar Salumu ambapo Saidi anatarajiwa kushiriki katika shindano la kusoma ,Tajuwid’ huku Salumu akishiriki katika kosoma Kuruan ambapo shindano hilo litafanyika juma lijalo.
Alisema vijana hao walipata fursa hiyo baada ya kushinda katika shindano lililoandaliwa kwa kuwakutanisha na wenzao kutoka vyuo na taasisi mbalimbali hapa nchini.
“Leo tunawaaga vijana hawa na tunaamini kuwa wataenda kufanya vizuri na watarudi wanang’ara kwa kupata ushindi”alisema Salum.
Alhad Salum anatarajia kuwa safari hii vijana hao watarudi na ushindi wakwanza ukilinganisha na ule wa mwaka jana, Tanzania ilishika nafasi ya pili.
Aidha, alisema anakishukuru kituo hicho cha Utamaduni kwa kuandaa mashindano hayo kila mwaka ambapo ni jambo zuri katika kuwajenga vijana katika maadili mema yatakayowakinga na vitendo viovu duniani.
Alisema kwa kila mwenye kuifahamu kuruan anapaswa kumfundisha mwingine kitendo ambacho ndicho kinachofanywa na nchi hiyo ya Irani.
Naye Mkurugenzi wa Kituo hicho Morteza Sabouri aliwaasa vijana hao kwenda kufanya kile kinachowapeleka huko kwani watambuwe nafasi hizo ni adimu ukichukulia wapo vijana wengi wenye uwezo kama wao hapa nchini.


Ankal Please we ni muislam mambo ya kutuandikia Kuruan hatujui ni kitabu gani kinaitwa kuruan. Hakuna kitabu kinaitwa kuruani katika dini ya kiislam jina ni Qur'an. Please hakuna K ni Q so tunaomba sana utoe tanbihi kwa watu wako wanapoandika jina la kitabu kitakatifu narudia tena ni Qur'an na sio Kuruani.
ReplyDeleteNawasilisha
mashallah Allah akujaliyeni kila la kheri hapa duniani na kesho akhera mambo kama haya ndo tunayotakaa sio leo hii tukiyafanya sisi tunaonekana wadini wakati wenzeetu wameyafanya na wanayaendeleza kuyafanya long time mpaka kuote mizizi ndani ya serikali
ReplyDeleteMASHA ALLAH! Mwenyenyez Mungu awazidishie elimu yenu na kuwaruzuku faham zenu. Pia awapeleke na kuwarejesha salama salimini. Awafanyie wepesi kwa hilo mnaloliendea. Awajaaliye kila lenye kheri na barka tele, awanusurishe na shari zote - AMEEN. Mkaisome "WARAT'TILI-L-QUR'ANA TARTILA" (Kwa utaratibu na utungo). Mwende na mrudi salama INSHA ALLAH.
ReplyDeleteMashaallah, nawakabidhi kwa Mwenyezi Mungu, Mungu ambaye amana anayokabidhiwa huwa haipotei, namuomba awapeleke salama na awarudishe salama, na awajaalie kushika nafasi ya kwanza, Inshaallah.
ReplyDelete