Mhe Pinda akisoma hotuba hiyo.

UTANGULIZI


1.            Mheshimiwa Spika, naomba kutoa Hoja kwamba kutokana na Taarifa zilizowasilishwa leo ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala na Kamati ya Fedha na Uchumi zilizochambua Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge lako sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2011/2012 na Mwelekeo wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2012/2013. Vilevile, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Taasisi zilizo chini yake pamoja na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2012/2013.

2.            Mheshimiwa Spika, tangu tulipohaitimisha Mkutano wa Bajeti  wa  Bunge hili mwaka jana, Nchi yetu imekumbwa na  Majanga  na Matukio mbalimbali yaliyosababisha vifo na  uharibifu  wa  mali.  Nitumie  fursa  hii  kutoa  pole    kwa  wote  waliofiwa  na  Ndugu, Jamaa na Marafiki. Mungu  azilaze  Roho za  Marehemu mahali Pema Peponi. Kwa ndugu zetu walioumia na bado wanajiuguza, tumwombe Mwenyezi Mungu awasaidie kupona haraka na kurejea katika shughuli za ujenzi wa Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...