Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limefanikiwa kupata taarifa za mtandao wa majambazi waliokuwa wakivamia na kuwapora vifaa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Johns wanaoishi nje ya chuo hicho mjini Dodoma.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma SACP Zerote Stiven, amesema kuwa kubainika kwa mtandao huo kunatokana na kukurupushwa na kushambuliwa vibaya kwa mmoja wa majambazi hayo aliyejulikana kw ajina la Amor Makanya au Mhiri.

Amesema Polisi alipofika eneo la tukio na kumhoji mtuhumiwa huyo, alitoa maelezo yaliyofanikisha kukamatwa kwa baadhi ya vifaa vya wanafunzi hao ambavyo viliibwa katika matukio tofauti na kukutwa katika nyumba ya kulala wageni walimokuwa wakiishi watuhumiwa hao huku wakiendeleza wimbi la wizi kwa wananchi mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa chuo hicho.

Amesema katika upekuzi katika vyumba vya watuhumiwa walikuta laptop kadhaa ambazo zilitambuliwa kuwa ni miongoni mwa mali zilizoibwa kutoka kwa wanafunzi wa chuo hicho.

Amesema pamoja na mali hizo, Polisi pia walibaini kuwepo kwa tiketi mbalimbali za mabasi ambazo zilitumika kwa safari za ndani na nje ya nchi na hivyo kuongeza shaka kuwa huenda mtandao huo una uhusiano na mitandao mingine ya kihalifu kutoka katika nchi nyingine jirani.

Hata hivyo Kamanda Zerote alisema mtuhumiwa huyo alifariki dunia akiwa katika hospital ya Mkoa Dodoma alikopelekwa kwa matibabu kutokana na kipigo cha wananchi.

Kamanda Zeropte amesema kuwa kwa siku za hivi karibuni yamekuwepo matukio kadhaa ya kuvamiwa kwa wanafunzi wa chuo hicho waliokuwa wakiishi nyumba za binafsi katika mitaa ya Kikuyu Kaskazini na Kusini mjini humo ambapo kuanzia Mei 26, mwaka huu matukio ya kuvamiwa kwa watuhumiwa hao yalishika kasi.

Amesema kuwa Makachero wake walikuwa wakifuatilia nyendo za watuhumiwa hao na ndipo mmoja wao aliposhambuliwa na wananchi usiku wa jana alipokuwa katika maeneo ya Kituo kikuu cha mabasi mjini Dodoma.

Vitu vingine vilivyopatikana katika nyumba hiyo ya kulala wageni ya Ukio ni pamoja na kadi za ATM za Mabenki ya Barclays, Kenya National Bank.

Amesema walipokagua kitabu cha Wageni katika nyumba hiyo makachero wa Polisi walipata majina ya watu wengine wawili ambao ni Sihoja Lutongisha ma Boaz Adhero ambao wamekimbia na Polisi inawataka wajisalimishe wenyewe kabla ya kutiwa nguvuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2012

    HONGEREN POLISI KWA KUPUNGUZA IDADI YA MAJAMBAZI DODOMA MAANA YANANYANYASA SANA RAIA WASIO NA HATIA. LAKIN HAMIENI NA KWA MAFISADI PIA MAANA HAO NDIO MAJAMBAZI WAKUMBWA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 02, 2012

    Wimbi la Majambazi Dodoma lina maana yake,

    Ni wazi ya kuwa watu wanaishi kwa Malengo na Mipango yenye akili, Majambazi wameona BAJETI kubwa ya matumizi inaelekezwa kwa Waheshimiwa hasa wakiwa huko Dodoma.

    Kama unavyoona imebidi wakae Gesti (Nyumba ya wageni kwa maana wametokea sehemu zingine na si wakazi wa kudumu huko Dodoma) hivyo nao wana Mtandao wa Majambazi wakaona wazifuate huko FEDHA !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...