Na Woinde Shizza,Arusha

MKUTANO wa benki ya maendeleo y Afrika, AFDB, ni changamoto kwa benki zetu hapa nchini katika swala zima la kuchangia kukua kwa uchumi na benki zenyewe kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko zilivyo sasa ili ziweze kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia inayotokea ulimwenguni na kuweza kuepuka kupata hasara kunapotokea mitikisiko ya kiuchumi

Hayo yameelezwa na Askofu Josephat Mwingira, alipokuwa akizungumza na Ripota wetu jijini hapa,anakohudhuria mkutano mkuu wa benki ya maendeleo ya Afrika ,na kusema kuwa kutokana na mkutano huo tunahitaji kufikiria upya juu ya mipango yetu kwa kushirikisha wadau wengi zaidi kuliko hali ilivyo sasa ili tuweze kupata maendeleo ya haraka na hivyo kushindana na mataifa yaliyoendelea.


Alisema Afrika sio maskini ila inakosa uongozi imara wenye dhamira nzuri ya kuwafungua macho wananchi waweze kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli ya kiuchumi na kupata maendeleo endelevu .

''unajua nchi yetu sio maskini ila tatizo ni kwamba inakosa viongozi wenye uwezo na ambao wanauchungu na nchi yao ,mbali na hao pia wanauchungu na wananchi wao''alisema Mwingira

Alibainisha kuwa amesikitishwa na idadi ndogo ya washiriki kutoka sekta binafsi nchini,huku washiriki wengi ni watumishi wa serikali na kutahadharisha kuwa iwapo hali hiyo haitarekebishwa siku zijazo taifa halitaweza kusonga mbele katika mabadiliko yanayotarajwa kwa sababu wadau ndio walengwa ila hawapewi nafasi ya kutosheleza kushiriki na kutoa mchango wao .

kuhusu,uwekezaji,askofu Mwingira amesema bado ni tatizo kutokana na jamii haijaelimishwa vya kutosha hivyo kushindwa kushiriki kikamilifu na kwa wingi katika shughuli zote ili iweze kuleta mabadiliko katika maisha yao na hatimae kuondokana na umaskini kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi na kuiendeleza.

Kwa upande wa wananchi,walifurahi na kusema kuwa mkutano huu umewaongezea kipato kwa kipindi kichache kwani wamekuwa wanafanya biashara sana na wamepata faida kubwa kutokana na wageni huku wakiisihi serikali kuendelea kuleta mikutano mikubwa kama hii jijini hapa kwani inawasaidia wananchi na kuongezea kipato jiji letu

''kwakweli nimefurahia mkutano huu kwani umetusaidia kuchangamsha mji na kutupa fedha nyingi,watu wamekuwa wakiuza vitu mbalimbali kwa ajili ya mkutano huu hivyo tunaomba serikali isitutupe bali ilete mikutano hii ili pato la jiji letu liendelee kukuwa"alisema Israel Mungure.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...