KAMATI ya Bunge ya Miundombinu imeipitisha bajeti ya Wizara ya Miundombinu, ambayo ni Sh1,023,033,626,000.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba, alisema kipaumbele cha wizara katika bajeti hiyo ni kuhakikisha barabara zote nchini zinaunganishwa kwa kiwango cha lami.
Juzi, Waziri wa Fedha na Uchumi, William Mgimwa, alisema bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13 inatarajiwa kuwa Sh15 trilioni katika vipaumbele saba. Bajeti inayomalizika ilikuwa Sh13.5 trilioni.
Serukamba alisema katika miradi ya maendeleo, fedha za ndani ni Sh296,896,892,000 na fedha za nje ni Sh397,051,380,000 na kwamba, jumla ni Sh693,948,272,000.
“Mishahara ya wizara na taasisi ni Sh21,340,508,000, mfuko wa barabara Sh300,764,800,000, matumizi mengine ni Sh6,980,046,000 na jumla yake ni Sh329,085,354,000,” alisema Serukamba.
Alisema bajeti hiyo imepita kwa urahisi kwa sababu fedha nyingi zimepelekwa katika miradi ya maendeleo.
“Serikali imeshapata fedha kwa ajili ya kulipa madeni yote ya wizara ambayo mpaka mwishoni mwa Juni mwaka huu yatakuwa yamelipwa. Ila tumewataka kuhakikisha msongamano wa magari Mwanza, Dar es Salaam na Arusha unakwishwa,” alisema Serukamba.
Alisema barabara zote za Dar es Salaam zimechukuliwa na Wakala wa Barabara (Tanroads) na zitajengwa kwa kiwango cha lami.
Vipaumbele katika bajeti hiyo ni miundombinu ambayo ina vipengele vinne; umeme, usafirishaji na uchukuzi, mawasiliano na maji salama.
Vipaumbele vingine ni kilimo, viwanda, rasilimali watu na huduma za jamii, utalii, biashara za ndani na n je na huduma za fedha.
Sasa uangalie uwezekano wa kupunguza msongamano Dar na Arusha.
ReplyDeleteMuheshimiwa Dr. Magufuli, tunakuomba ile barabara ya Mombasa-Mazizini-Moshi Bar UKONGA ifanyiwe kazi, ina magari mengi wakazi wengi sana, shughuli nyingi sana za kibiashara lakini barabara imekuwa ni tatizo kubwa SANA NA MATESO MAKUBWA. Naomba hili tatizo uliweke kwenye faili lako mkuu. I salute you!
ReplyDeleteMhe. punguza miradi ya mjini na utukumbuke sisi wa vijijini katika mikoa iliyoko nyuma kimaendeleo
ReplyDeleteTunakuomba jaribu kuijenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka kimara kupitia chuo kikuu pia waombwe jeshi letu watoe njia kutoka goba kuingilia chuo kikuu ni laisi sana kuingia mjini
ReplyDeleteMheshimiwa daraja la kinyerezi limeterekezwa baada ya kubakwa na mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa mwaka jana. Pia lile daraja lingepeza likinyanyuliwa juu zaidi kwani pale ni bondeni likinyanyuka litapunguza mlima uliopo na litakuwa limeweka uwazi wa kutosha kiasi kwamba maji yatakuwa hayawezi tena kuliharibu
ReplyDeletesasa barabara ya kigoma-kasulu-kibondo .paka kahama ndio lami yake iliisha liwa au ilikuwa ni propaganda za kupatia uongozi mbona wewe magufuli hueleweki?
ReplyDeleteTukumbukeni watu wa kigoma sio hivyo na usafiri wa reli upewe kipau mbele
Mheshimiwa Magufuli Pombe, wewe ni kidume kweli, tengeneza barabara baba, tunakufagilia, ila na sisi wenyeji wa Kimara King'ongo mpaka kwa Komba, hebu tuangalia kibarabara chetu, ili mradi japo kiwe katika hali nzuri hata kama siyo rami, maana tunapata shida sana tunapokuwa na wagonjwa au wajawazito, Mh. Chonde chonde baba, tunajua unaweza, ni hayo tu.
ReplyDelete