Mh. Alhaji. Adam Kimbisa
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wameapishwa rasmi kushika madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hilo.
Wabunge hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana Uchumi, Margareth Zziwa kuchukua nafasi hiyo.
Wabunge wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo hii leo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose Saddrudin Bhanji.
Wengine ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi Yahya,Mh.Nderkindo Perpetua Kessy, Dkt Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Mhe Bernard Musomi Murunyana Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta anaeingia kwa wadhifa wake wa Uwaziri.
Wabunge hao wameapishwa pamoja na wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Picha na FATHER KIDEVU BLOG
Mh. Samuel Sitta ni muwakilishi wa Tanzania
Mh. Abdullah Alli Hassan Mwinyi
Mh. Charles Makongoro Nyerere
Mh. Dkt. Twaha Issa Taslima
Mh. Nderkindo Perpetua Kessy
Mh. Bernard Musomi Murunyana
Hivi Mhe. Shyrose anaapa kwa kutumia kitabu gani maana naona ni tofauti na vingine walivyoshika waislamu na wakristo
ReplyDeleteQuran ile mheshimiwa au umeonaje?labda macho yangu huenda ikawa ni kitaku cha ujamaa ukoministi kisochoamini dini yeyote
ReplyDeleteSHY ROSE YEYE NDO KAONYESHA DHAHIRI SHAHIR (WAZI WAZI) KWAMBA NI MTOTO WA KIISLAMU KILA ALIYE NA MACHO KAIONA ILE QURAN YENYEWE SIYO WENZAKE WAMEIFICHA MKUU HAPO JUU ULIYETOA COMMENT HUONI BWANA
ReplyDeleteImani zipo nyingi....usikariri mdau
ReplyDeletemkuu unaesema kuwa shy rose ndio alieonyesha dhahir shahid,umeangalia kweli alichokishika? ameshika kitabu cha tafsiri ya Quran sio msahafu. Sisemi shy rose sio muislamu ila nasema alichoshika sio mshahafu mtukufu ila ameshika tafsiri ya mshahafu, kuna tafauti kubwa hapo.
ReplyDeleteHiyo Ni AL FURQAAN au QURAAN TAKATIFU:
ReplyDeleteInshallah Mwenyezi Mungu wa Rehma amzidishie!!!
Hakuna ubishi Shyrose Bhanji ni Binti wa Kiislamu!
Ile ni Quran,
ReplyDeleteShyrose ni Mwislamu, msije mkababaika na hiyo ROSE mwisho ktk jina lake!