Watukumiwa wa Mauaji ya mtoto wa Chifu Abdallah Fundikira,Marehemu Swetu Fundikira walipofikishwa Mahakamani Januari 27,2010 kusomewa mashtaka yao
========== ==========
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuanzia kesho Jumatatu Juni 4, 2012 itaanza kusikiliza kesi ya mauji ya mtoto wa Waziri wa zamani wa Sheria Hayati Chifu Abdallah Fundikira, Swetu Fundikira, inayowakabili MT 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi cha Mbweni na wenzake.
Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya uendeshaji wa kesi za Mahakama Kuu ambayo Ripota wa Globu ya Jamii ameiona nakala yake, kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na Jaji Zainabu Mruke na jumla ya mashahidi tisa wa upande wa jamhuri watatoa ushahidi katika kesi hiyo.
Washtakiwa wengine ni MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Kikosi cha Kunduchi na MT 85067 Koplo Mohamed Rashid wa JKT Mbweni.
Wakili wa serikali Mh. Dionisia Saiga awali alidai mahakamani hapo kuwa Januari 23, 2010 kuanzia majira ya saa 6 usiku, kuwa marehemu akiwa na wenzake wawili aliuawa na watuhumiwa hao wakati akijaribu kumuokoa dereva wake asipigwe na askari huyo.
Marehemu Swetu Fundikira enzi za Uhai wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...