Tangu wiki iliyopita tarehe 4/June nimekuwa nikihudhuria mahakamani katika kesi ya mauaji ya Swetu Ramadhani Fundikira mpaka jana tarehe 12/06 ilipofikia ukomo kwa siku ya hukumu kutajwa kuwa ni 30/10/2012. sio siri nimefumbuka mno na weledi unaotumika humo katika kuendesha kesi hasa ya mauaji. Lakini kuna suala moja linanitatiza nalo ni usalama wa wazee wa baraza, wamekuwa wakifika pale mahakamani kwa dala dala na wamekuwa wakiondoka hapo kwa daladala. Tujiulize watu wanaopewa jukumu kubwa la kutoa maoni yao katika kesi ya mauaji kupatikana kirahisi namna hiyo ni sawa? Nasikia wanalipwa sh 10,000/= kila siku watakayohudhuria mahakamani. Je ni sawa kuweka maisha ya mtu hatarini kwa kumlipa sh 10,000/= tu? Je tunawezaje kusema kuwa ndugu wa washtakiwa hawawezi kujaribu kuwarubuni wazee hawa? Nchi zilizopiga hatua wazee hao huwekwa kambini kwa kipindi chote cha kesi itakapokuwa ikiendelea, hivyo basi huwa salama na watatarajiwa watoe maamuzi yenye kuzingatia haki.
Kwa mtazamo wangu.
1.Ipo haja wazee hawa wafanyiwe mchujo ikiwezekana na wajaribiwe ili kujua uwezo wao wa uelewa na busara, kwani si kila Mzee ana busara.
2.Wawekwe kambini kwa siku zote watakazokuwa wakisikliza kesi kabla ya kutoa maoni.
3.Wafikishwe mahakamani kwa usafiri maalumu na warudishwe kambini na usafiri huo.
4. Waongezwe posho hata ifikie 50,000/= kwa siku.
| Ndugu wa marehemu Swetu Fundikira wakiwa nje ya mahakama jana |
| Ndugu wa marehemu mahakamani |
2.Wawekwe kambini kwa siku zote watakazokuwa wakisikliza kesi kabla ya kutoa maoni.
3.Wafikishwe mahakamani kwa usafiri maalumu na warudishwe kambini na usafiri huo.
4. Waongezwe posho hata ifikie 50,000/= kwa siku.


Kwa kuwa Umuhimu wa Wazee wa Baraza ni kukamilisha utendaji ktk uendeshaji wa kesi, licha ya kukaa hadi kesi iishe hakuna sababu kwa nini wasikae Kambini hadi kifo kabisa kikiwafikia.
ReplyDeleteInaonekana hujui bajeti ya mahakama ilivofinyu wewe. Pesa yote inaishia bungeni.
ReplyDeletendo bongo hiyo bongo bongo mambo yote kienyeji lakini mafisadi wanajua kuwa serious
ReplyDeleteSidhani kama kuna hatari yoyote kwani wao wanachotoa ni maoni tu ambayo hata wewe unaweza toa, na maoni yao si lazima Judge ayachukue kama yalivo kwani wao wanatoa busara zao tu then Judge anachambua na kuona kama kuna point muhimu then anarudi katika sheria inasemaje. Wa kupewa ulinzi ni Judge kwani ndo muandaa hukumu na kuisoma. Hao wengine labda ni sawa tu kuwaongezea posho lakini kwa ulinzi sidhani kama ni kiivooooo
ReplyDelete