Ndugu wa marehemu Swetu Fundikira

Na Keronyingi Blog
Tangu wiki iliyopita tarehe 4/June nimekuwa nikihudhuria mahakamani katika kesi ya mauaji ya Swetu Ramadhani Fundikira mpaka jana tarehe 12/06 ilipofikia ukomo kwa siku ya hukumu kutajwa kuwa ni 30/10/2012. sio siri nimefumbuka mno na weledi unaotumika humo katika kuendesha kesi hasa ya mauaji. Lakini kuna suala moja linanitatiza nalo ni usalama wa wazee wa baraza, wamekuwa wakifika pale mahakamani kwa dala dala na wamekuwa wakiondoka hapo kwa daladala. Tujiulize watu wanaopewa jukumu kubwa la kutoa maoni yao katika kesi ya mauaji kupatikana kirahisi namna hiyo ni sawa? Nasikia wanalipwa sh 10,000/= kila siku watakayohudhuria mahakamani. Je ni sawa kuweka maisha ya mtu hatarini kwa kumlipa sh 10,000/= tu? Je tunawezaje kusema kuwa ndugu wa washtakiwa hawawezi kujaribu kuwarubuni wazee hawa? Nchi zilizopiga hatua wazee hao huwekwa kambini kwa kipindi chote cha kesi itakapokuwa ikiendelea, hivyo basi huwa salama na watatarajiwa watoe maamuzi yenye kuzingatia haki. 
Kwa mtazamo wangu. 
 
Ndugu wa marehemu Swetu Fundikira wakiwa nje ya mahakama jana

 
Ndugu wa marehemu mahakamani
  1.Ipo haja wazee hawa wafanyiwe mchujo ikiwezekana na wajaribiwe ili kujua uwezo wao wa uelewa na busara, kwani si kila Mzee ana busara.
2.Wawekwe kambini kwa siku zote watakazokuwa wakisikliza kesi kabla ya kutoa maoni.
3.Wafikishwe mahakamani kwa usafiri maalumu na warudishwe kambini na usafiri huo.
4. Waongezwe posho hata ifikie 50,000/= kwa siku. 
Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2012

    Kwa kuwa Umuhimu wa Wazee wa Baraza ni kukamilisha utendaji ktk uendeshaji wa kesi, licha ya kukaa hadi kesi iishe hakuna sababu kwa nini wasikae Kambini hadi kifo kabisa kikiwafikia.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2012

    Inaonekana hujui bajeti ya mahakama ilivofinyu wewe. Pesa yote inaishia bungeni.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2012

    ndo bongo hiyo bongo bongo mambo yote kienyeji lakini mafisadi wanajua kuwa serious

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 14, 2012

    Sidhani kama kuna hatari yoyote kwani wao wanachotoa ni maoni tu ambayo hata wewe unaweza toa, na maoni yao si lazima Judge ayachukue kama yalivo kwani wao wanatoa busara zao tu then Judge anachambua na kuona kama kuna point muhimu then anarudi katika sheria inasemaje. Wa kupewa ulinzi ni Judge kwani ndo muandaa hukumu na kuisoma. Hao wengine labda ni sawa tu kuwaongezea posho lakini kwa ulinzi sidhani kama ni kiivooooo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...