Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu , Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Aggrey Mwanri akijibu maswali mbalimbali yaliulizwa na Wabunge katika kipindi cha maswali na majibu leo mjini Dodoma.
Naibu wa Mambo ya Ndani ya Nchi Pereira Ame Silima akijibu maswali mbalimbali yaliulizwa na Wabunge katika kipindi cha maswali na majibu leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA na Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe akimuuliza Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda maswali ya papo kwa papo leo mjini Dodoma katika kikao cha tatu cha mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu ) Stephen Wasira akiwasilisha Bungeni leo mjini Dodoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011 na mwelekeo wa mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2012/13.
Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda (kulia) akimsikiliza kwa makini Waziri ujenzi Dkt Jojn Pombe Magufuli(kushoto) leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao cha tatu cha mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoendelea mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akisikiliza kwa makini taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011 na mwelekeo wa mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2012/13 iliwasilishwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira.
Mwanasheria Mkuu wa serikali Jaji Fredrick Werema (kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi(kushoto) wakijadiliana jambo leo mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Emmanuel Nchimbi (katikati) , Mbunge wa Afrika Mashariki Shyrose Bhanji (kulia) na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Esther Bulaya(kushoto) wakibadishana mawazo leo mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 15, 2012

    nataka kuliza swali hivi cuf zanzibar haipo kwa sababu maalim ndo yupo katika serikali ya mseto na wakati huku namuona ibrahim lipumba bado yuko bechini si ndo chama walichokuwa wanakipigania wote sasa yeye mbona yupo benchini

    nijibuni wadau wenzangu ili nitoe utata huu tafadhalini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...