Kocha wa timu ya Mpira wa Kikapu ya vijana chini ya Miaka 17,Greg Brittenham kutoka nchini Marekani (kushoto) akitoa maelekezo wa vijana wake wakati wa kufunga Mafinzo ya vijana wa chini ya miaka 17 yaliyofanyika jijini Arusha tarehe 10, Juni 2012.
Kocha wa timu ya Mpira wa Kikapu ya vijana chini ya Miaka 17,Greg Brittenham akionyesha mfano kwa vijana wake.
Viongozi wa Mpira wa Kikapu nchini pamoja na mgeni rasmi wakiwa kwenye picha ya pamoja na timu.

Katika nasaha zake za kufunga Clinic hii Mhe Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela aliwashukuru wote waliofanikisha ikiwemo watu wa Marekani, Cocacola , Kocha Greg na wengine wote.

Mhe. Mkuu wa wilaya alisema aliposikia Kocha Greg amekuja hakuamini kwa sababu sio kitu rahisi na ni bahati ya pekee kwa vijana wa kitanzania kupata kufundishwa na kocha aliyefundisha NBA.

Mhe. Mongella aliwaambia vijana hawa kuwa yeye pia ni mpezni wa kikapu na aliwahi kuishi New York siku za nyuma, hivyo anajua umuhimu wa kocha huyu

Hivyo aliwaomba vijana hawa wazingatie mafunzo waliyoyapata na aksema hii ni historia katika maisha yao, kwani wako vijana wengine wako Marekani lakini hawapati bahati kama waliyopata hawa vijana wa Arusha.

Mkuu wa Wilaya alikiri tatizo kubwa la viwanja na kuahidi kulifanyia kazi, pia alisema atajaribu kushirikiana na wadau wote walioko Arusha ili wasaidie kuinua mchezo wa kikapu.

Mkuu wa wilaya aliahidi kusaidia timu zote za Arusha pale zitakapokuwa zinatakiwa kushirikia mashindano ya Kitaifa.

Mhe. Mkuu wa wilaya alihimiza michezo mashuleni na kuomba walimu wawape nafasi vijana ili waonyeshe vipaji vyao mashuleni ikiwa ni pamoja na kuhimiza kila shule iwe na viwanja na walimu wa michezo.

Pia mkuu wa wilaya aliwaasa vijana wazingatie masomo darasani, michezo viwanjani na kudumisha nidhamu muda wote.

Mhe. Mongella alimuomba Kocha Greg aje tena Arusha na akaitangaze vyema Tanzania ili tuweze kuvutia watalii wengi zaidi.

Na mwisho alitamka kuafunga rasmi mafunzo haya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...