Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam imeanza kuhakikisha Dar kuna maeneo ya kushangaa na kupigia picha! Hapa ni Round about ya Bridge/India/Makunganya ( Msikiti wa Ngazija) More to come, wanasema. 
Theme: utajiri wa maliasili Tanzania



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2012

    ujinga mtupu hivi huwa wanakosa vitu vya kupendezesha?

    waweke hata maua mazuri na maji yawe yanaruka juu huku yanamulikwa na taa za rangirangi kutapendeza hata usiku

    hapo usiku giza likiingia hakuna lolote wekeni mataa ya rangi na maji ya kuruka juu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2012

    safi... angalua ukimuelekeza mtu unamwambia... pale kwenye mduara wa mamba.. kata kulia.. tehe tehe

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2012

    Imependeza sana, sema tu hizi electric cables zilizohanikiza hewani ndio huwa zinaharibu mandhari.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2012

    Halahala biashara ya vyuma chakavu!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2012

    Hizi zitakawia kusombwa na wezi wa chuma chakavu kweli?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 13, 2012

    sasa inabidi walindwe na umeme hao twiga wa mabati maana waheshimiwa wa vyuma chakavu watakuja kuwafyagia muda si mrefu

    dula maandazi

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 13, 2012

    wasiwasi wangu juu ya mateja kuiba kama vifaa chakavu si unajua ankali?
    chokoraa ni chokoraa tuu,hebu tujaribu tuone ikipita mwezi bila kuhujumiwa basi tumefanikiwa

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 13, 2012

    wakishakula % zao wanazitelekeza hizo vitu, mpaka machizi wanapanda wanaharibu nobody cares!!
    huu ni mradi wa wajanja tuu. remember signs za barabarani katikati ya jiji? remember mbango ya no parking? kuna mwingine akaweka bango la usifanya biashara hapa, pale salender bridge ambapo hapajawahi kuwa na wafanya biashara.
    ufisadi mtupu!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 13, 2012

    hala hala.. ndugu zetu wa kununua vyuma chakavu wasije pitia malighafi hizi... tujifunze kutunza jiji letu na kuachana na mila potofu za kudharau na kutojali...

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 13, 2012

    Gharama zilizotumika hapo sijui dola ngapi?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 13, 2012

    mpaka hapo mmekwishatumia bilioni ngapi au tiliomi ngapi? na tuwaongeze ngapi kukamilisha mradi?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 13, 2012

    Leo nimepita nimeona kuna mtu anamwaga maji machafu, hayo mawe yameshageuka rangi na kuwa meusi, Kaka Michuzi hebu waambie waweke ilani watu wasimwage maji machafu, hivi wamehsindwa kuweka maua? na maji yanayoruka kama mdau wa juu alivosema , haya na waosha magari ndio sehemu yao ya kumwaga maji machafu wewe pita uone kaka Michuzi Tanzania bhhana ! ah

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 13, 2012

    Maji ya kuruka ndo umeona bomba sana ?? na huyo uliyemuona anamwaga maji taka pale ,wewe kama mzalendo ulimwambia nini ?? akili za wengine sijui vipi-mmekalia kulaumu tu kila kukicha -ningependa kuona unavyoishi ndugu yangu maana watu kama nyie ni mzigo tu wa taifa-lawama haziwaishi vinywani mwenu. kingine -hilo neno Fisadi litumieni vizuri-maana kila kitu sasa hivi ni Fisadi-get over with man. Zebedayo

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 13, 2012

    Hapo kwa kuwa zimetengenezwa kwa vyuma utaambiwa zimetumika BILIONI 100 !

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 13, 2012

    Hapo 'material' imechaguliwa iwe ni CHUMA ili wazito wakiongeza masifuri watu wasiulize!

    Mfano Ujenzi halisi ni Tsh,1,000,000 hapo kwa vile ni vyuma zinaongezeka koma koma (,) na sifuri tatu (3) mwisho na hiyo moja mwazo inafuatiwa na sifuri mbili (2).

    Mnafikiri gharama za maisha Mabosi wanazimudu vipi?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 13, 2012

    Kwa kuwa ni vyuma udhibiti ni rahisi tu ni kutegesha umeme!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 13, 2012

    TANZANIANS why cant you just appreciate things???Thats just BEAUTIFUL..Please tuleteeni pale kawe roundabout moja wapo. INAPENDEZA SANA!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 13, 2012

    We mchangiaji wa mwanzo kabisa kwako mapambo ni maji ya kuruka juu na maua tu basi? Mbona ubunifu huu unapendeza kabisa? Cha msingi ni ulinzi na matunzo ya hayo mapambo. Na sie pia tuache uchafu wetu,inawezekana kabisa jiji kuwa safi na kupendeza.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 13, 2012

    Mjomba ujuwe dunia inaendelea kwa watu kuwa wabunifu siyo kwa watu kuiga kila
    kitu maji yanayoruka tumesha ya zowea kama kunguru weusi
    watu waje na vitu vingine na siyo kisa maji yanaruka sehmu fulani nao waweke
    Me niwapongeze wawe wabunifu zaidi sd20k@yahoo.com

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 13, 2012

    hizo waya za umeme zinaharibu zingetolewa zipite pembeni ya magorofa sio katikati ya bara bara ukipiga picha mawaya yanaonekana. halafu walinzi wawe walio izunguka hilo duara yeyote atakae haribu chochote wanamkamata.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 13, 2012

    HAO WANYAMA WANGEWEKEWA MAJANI KUONYESHA UKIJANI NA MAUA, MAJI YA KURUKA KAMA WALIVYOSEMA WENGINE, VINAPENDEZESHA HATA MACHO KUONA. HAPO BADO NI KUISHIA VYUMA CHAKAVU TU.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 13, 2012

    Tumetumia ka milioni 700 tu.

    Shukran

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 13, 2012

    We mdau unayesema waweke maji ya kurukaruka.... kwani Dar au Tanzania kuna keep left moja tu? si viko vingi hivyo si vyote vifanane..

    hapo wameepuka gharama za maintanance... bustani na maji ya kurukaruka ni gharama kuzitunza

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 13, 2012

    Watanzania na wabongo wote hatujui mandari nzuri wala usafi. mzungu anajenga na kusafisha barabara ya Morogoro road pale Manzese usiku pamemwagwa marundo ya taka katika katika ya sehemu ambapo dongo la barabara limekwishawekwa sasa. Utamaduni wetu ni uchafu, nao ni ufisadi mkubwa.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 13, 2012

    Sio wabunifu ni cut and paste, nenda zambia (Lusaka) on the way to airport utaziona hizi kibao. Tembo, Nyati.... so there is not much of discovery, ila am proud of the guy who convinced these big guys to add some values

    great!!!!!

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 14, 2012

    Bora hata kama siku hizi wa TZ MNAJUA KUKOPI NA KUPEIST NI MAENDELEO MAKUBWA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...