Vikosi vya Taifa Stars na Ivory Coast vikiingia uwanjani kuanza pambano lao la kuwania tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika,uliochezwa jana jijini Abdjan,Ivory Coast.
Mbwana Samatta akiwania mpira na Alexander Igor Lolo wa Ivory Coast wakati wa mchezo ulichezwa jana jioni katika uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan,Ivory Coast.Taifa Stars ililala kwa Bao 2-0.
Mbwana Samatta wa Taifa Stars akiwania mpira na Salomon Kalou wa Ivory Coast.
Mshambuliaji Mrisho Ngassa (kushoto) wa Taifa Stars akiwania mpira na Kolo Toure wa Ivory Coast.
Beki Siaka Tiene (kulia) akimfanyia madhambi Mrisho Ngassa wa Taifa Stars wakati wa mechi hiyo iliyofanyika jana.
Wachezaji wa akiba wakifuatilia kwa makini wakati wa mechi dhidi ya Ivory Coast jana.
Sehemu ya washabiki wa Ivory Coast.
Kikosi cha Taifa Stars ambacho jana kilicheza na Ivory Coast hapa Abidjan na kupoteza kwa mabao 2-0 kinaendelea kujinoa kwa mechi ijayo dhidi ya Gambia itakayochezwa Jumapili (Juni 10 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi cha Taifa Stars ambacho jana kilicheza na Ivory Coast hapa Abidjan na kupoteza kwa mabao 2-0 kinaendelea kujinoa kwa mechi ijayo dhidi ya Gambia itakayochezwa Jumapili (Juni 10 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa programu ya Kocha Kim Poulsen, Taifa Stars imefanya mazoezi leo asubuhi kwenye uwanja wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Ivory Coast (FIF) ambao uko pembezoni mwa jiji la Abidjan.
Timu hiyo itafanya tena mazoezi kesho (Juni 4 mwaka huu) asubuhi kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani saa 1.30 usiku kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi ambapo itawasili Dar es Salaam, Juni 5 mwaka huu saa 1.40 asubuhi.
Kocha Kim ambaye amekuja na wachezaji wote hapa ukiondoa wanne ambao ni majeruhi (Thomas Ulimwengu, Nurdin Bakari, Haruna Moshi na Nassoro Masoud Cholo) amesema hivi sasa wameelekeza akili yao kwenye mechi ijayo dhidi ya Gambia.
“Safari ya kujenga timu ndiyo imeanza. Mechi dhidi ya Ivory Coast imepita na ninawashukuru wachezaji kwa kucheza kwa mujibu wa maelekezo na kujituma. Mpira ni mchezo wa makosa, tumefanya makosa yaliyosababisha tuwape Ivory Coast mabao mepesi.
“Lakini kama nilivyosema mechi hiyo imepita, hivi sasa tunaangalia mechi ijayo dhidi ya Gambia. Hatuna muda mwingine wa kujipanga na ndio maana niliamua kuja na wachezaji wote Abidjan,” amesema Kim.
Mechi dhidi ya Gambia itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni. Gambia ilitoka sare ya bao 1-1 na Morocco katika mechi iliyochezwa juzi jijini Banjul.
Hata hivyo, Taifa Stars haitakuwa na nahodha wake msaidizi Aggrey Morris ambaye alionesha kadi nyekundu dakika ya 65 baada ya kupata ya pili ya njano kwenye mechi dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan.
Vijana walijitahidi sana.Mashambulizi golini yanafika,umaliziaji bado ni kikwazo.Kuna mdau humu alisisitiza stars kufungwa 6-0!
ReplyDeleteDavid V
Hata hivyo stars wamejitahidi.Tungefungwa bao nyingi ingekuwa aibu kubwa.
ReplyDeleteni hayo tu. Kwa hiyo hongera stars kwa kujitahidi
Mr Nyamaimewahi Kunikabashingoni.
Hongereni kwakujitahidi kuzuia nakufungwa magoli kidogo.
ReplyDeletenilisema hii siyo timu ya kuifunga ivory coast wala Gambia. Kocha lazima arudishe wazoefu. hizi ni mechi kubwa asipofanya hivyo tutamaliza duru ya kwanza bila pointi. nawakilisha.
ReplyDeleteLazima ukweli usemwe, STARS wamejihadidi sana, wengi hatukutegemea matokeo hayo. japo tumefungwa
ReplyDeleteWell done Taifa stars!!!!. Naomba kocha aendelee kuimarisha team ktk idara zote husika. Ni muhimu kuelewa kuwa kuna mwanzo wa kila jambo..naamini kuna siku team itafanya kila ambacho watanzania tunakitarajia. Ahsante
ReplyDeleteushabiki wetu upo sana kwenye chadema na ccm mambo ya mpira tia kapuni watanzania viongozi wanawaza ikulu tu.
ReplyDelete