Mafungu 7 (seven bunches) ya maua maarufu yajulikanayo kwa jina la Marie Claire Rose (pichani) yameibiwa kw a hila na ghilba katika ofisi za basi la Super Feo katika stendi kuu ya basi ya jijini Mbeya leo asubuhi jijini Mbeya.

Katika tukio hili la wizi wa mafungu saba yalitoweka katika ofisi za Super Feo bila maelezo yanayaoeleweka. Maua hayo yalitumwa kutoka kampuni ya Allure Flowers ya Njombe yakiwa yameandikwa jina la kiume la mtoto wa kiume wa bibi mmoja wa Tukuyu ambae leo (5 Juni 2012) anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa huko kijijini, wilayani Rungwe.

 Mtoto huyo wa kiume alifika stendi kuu ya Mbeya jana jioni (4 Juni 2012) kuyachukua maua hayo lakini alielezwa kwamba yalikuwa yamepakiwa kwenye gari inayofuata ambayo ingefika kati ya saa 12 na nusu jioni au saa 1 na nusu usiku huo.

Kwa kuzingatia muda huo na safari aliyokuwa nayo ya kurudi kijijini wilayani Rungwe, mtoto huyo wa bibi huyo alifanya mpango na bwana mmoja mlinzi wa maeneo ya jijini Mbeya, kumpokelea mzigo huo wa maua na kumpelekea kijijini Rungwe kesho yake asubuhi (yaani asubuhi ya leo 5 Juni 2012) mara mlinzi huyo atokapo lindoni.

Aidha aliwaarifu wafanyakazi wa Super Feo kuhusu mpango huo wa mzigo wake kuchukuliwa kwa niaba yake na kisha akaendelea na safari yake ya kurudi Rungwe.

Cha ajabu mlinzi huyo alipofika ofisi za Super Feo asubuhi ya leo (5 Juni 2012) alistaajabishwa na taarifa ya kwamba eti maua yale yamekwishachukuliwa na dada aitwae Sofia. Nae mtoto wa bibi aliyekuwa akiyasubiri maua hayo Rungwe aliamua kumpigia simu mlinzi huyo ilipofika saa 4 asubuhi bila maua hayo kuwasilishwa kijijini huko Rungwe. Mlinzi aliijibu simu hiyo na taarifa hizo za kusikitisha.

Wafanyakazi wa Super feo jijini Mbeya walishindwa kujieleza kwamba ilikuwaje walimpa ‘Sofia wa Songwe’ mzigo ambao uliandikwa jina la kiume na wakati mwenye mzigo alishafika ofisini kwao na kutoa maelezo ya kwamba mzigo ungechukuliwa na mwanaume kwa niaba yake? Aidha hata mtumaji, Allure Flowers wa Njombe, alikuwa ametoa maelezo yanayoshabihiana kwamba mzigo ungechukuliwa na mwanaume na mzigo ulikuwa umeandikwa jina la mpokeaji wa kiume.

Katika mazungumzo na majadiliano ya simu kati ya mlinzi Super Feo Mbeya na mwenye mzigo huko Rungwe namba ya simu ya huyo dada Sofia wa Songwe iliweza kupatikana. Alipopigiwa Sofia wa Songwe alidai yuko Songwe na yeye vilevile alikuwa ameagiza maua kama hayo.

Alipoulizwa je huo mzigo wa maua ulikuwa na jina lake alishindwa kutoa jibu. Aidha Allure Flowers walipopigiwa simu tena walikana kumfahamu Sofia na walikanusha kwamba alikuwa ameagiza maua ya aina yoyote kutoka kwao.

Mpaka sasa dada huyo anajivuta na kuchenga kuyarejesha maua hayo kwa kudai yuko mbali na anamtafuta kijana wa kumtuma, huku siku ya besdei ya bibi wa Rungwe ikiendelea kuyoyoma. Alipoelezwa kwamba hii inaelekea kuwa kesi ya wizi maana ilikwishathibitishwa kwamba hakuna oda yoyote ya maua kwa jina lake kwenye kampuni ya Allure Flowers na kwamba ni wazi mzigo huo wa maua uliandikwa jina la kiume na siyo ‘Sofia’ hivyo suala hili litafikishwa Polisi- Sofia alijibu kwamba kulipeleka suala hili Polisi hakutasaidia chochote; haikueleweka mara moja kwamba huyu ‘Sofia wa Songwe’ alikuwa na jeuri gani ya kusema hivyo na kukijusuru na kukichagiza chombo cha usalama ambacho wananchi wanakitegemea kwa ulinzi na usalama wao na wa mali zao.

Maua hayo yanasemekana kuwa maalum na yenye soko zuri kwa wapenda maua ndani na nje ya Tanzania. Ankal Michuzi tusaidie kumpata ‘Sofia wa Songwe’ na wakuu wa Super Feo ili maua yarejeshwe kwa mwenye nayo na ukweli upatikane kwamba imekuaje mzigo apewe mtu mwanamke ambae si wa kwake na mzigo ukiwa umeandikwa wazi jina la kiume na maelezo ya wazi ya mzigo kuchukuliwa yakiwa yametolewa na kurudiwa mara kadhaa. Je hii hii ni kawaida ya watoa huduma ya mabasi? Ni kawaida ya Super Feo kuwafanyia wateja hivi?

Tutafutie jibu pia Michuzi kwamba eti kweli haisadii kitu kutoa taarifa Jeshi la Polisi mali yako ikiibiwa??
Aidha SUMATRA inasemaje katika masuala kama haya? Haki ya mteja inalindwaje? Hatua dhidi ya msafirishaji ni zipi?

Tusaidie Ankal majibu na maua yapatikane!
Maua yangali yanasubiriwa na mwenye besdei leo!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2012

    Mwizi aliyekusudia ataacha namba zake za simu na contact zake halisi? Wakati mwingine muwe mnatumia common sense wandugu, Super feo wapo na wametoa ushirikiano mzuri kabisa, na wanaweka kumbukumbu zao vizuri. Aliyechukua maua anajulikana, mnawasiliana naye na mpaka sebuleni kwake mnaweza kufika. Mnataka Michuzi awasaidie nini tena?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2012

    Sasa Michuzi anahusikaje hapa? Si mkatoe ripoti polisi. Habari zingine bwana.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2012

    Huu ndo ulimbukeni wa watz.maua yanazidi kunyauka namba ya mwivi unayo unataka michuzi akufuatilie kvp hata namba ya simu ya mchukuzi wa mzigo hujaiweka!wajinga ndo waliwao

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2012

    Auncle mwaka huu unalo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2012

    Wenye basi wana makosa kwani unampaje mtu mzigo bila kuonyesha kitambulisho?

    Ila Wabongo wamezidi wizi yaani kila mahala ni wizi tu, bora hayo maua mimi nimesafirisha mizigo yangu kutoka UK mpaka Dar nimeilipia kodi huko TRA kisha sikupata hata box tupu. Mizigo imezuiliwa wee TRA ilivyotolewa wamempa mtu wanaemjua wao, laanakum, wizi mpaka vitu vya yatima na mzidi kulaaniwa!! Ukipewa mzigo wa mtu fikisha na kama kitu si chako usichukue!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2012

    Tz shughuli ipo Posta wezi, TRA wezi, Mabasi wezi,Mahakamani wezi wapi sasa tunaenda au ndo kiama? Hapa UK mara nyingi tu nimepoteza simu yangu mara niisahau kwa bus mara University ila naipata back kwani wakiokota wanapiga kwa marafiki zangu na naipata back. Acheni wizi mtapata laana bure hasa hawa Tra nyie ngojeni tu lazima nilipe kisasi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...