Nampongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kwa kitendo chake cha Kijasiri cha kumkamatisha fedha za moto huyu Mbunge wa Bahi (CCM) ambaye awali alishatajwa kuwa ana kamchezo ka kuomba na kupokea rushwa na Mbunge machachari David Kafulila (NCCR-Mageuzi). 

Wengi walibisha wakati ule lakini kumbe Mwl Nyerere alizungumza ukweli kwamba ukizoea kula nyama ya mtu kuacha ni kazi ngumu. Nitoe wito kwa Watendaji wa Serikali katika ngazi zote kwamba utaratibu huu wa kuwaanika waomba rushwa kama huyu jamaa ukifanywa na kila mmoja wetu, utasaidia sana kupunguza tatizo la rushwa nchini. 

Rushwa ni Adui wa Haki Tushirikiane Kuitokomeza. EKN - 

Mdau toka Copenhagen - Denmark

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2012

    Ndugu wa Denmark,nashukuru kwa kuliona hilo la rushwa-yaani ,tumechoka nalo ile mbaya, na woga wetu ndiyo umetuponza kwa kuyaacha huru haya madudu kuendelea, kuna mhasibu Tannesco Ubungo ,jamani huyu naye angepewa pesa za moto. Kwa kweli huyu jamaa kabila msukuma ana nuka mavi ya rushwa. Asanteni wote mtakao jitolea kusafisha haya madudu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2012

    Wala Rushwa ni wengi tu wanajijua wenyewe na kufichiana siri,kuanzia ngazi za chini hadi juu,iliyobakia ni wananchi wenyewe wafanye kazi kubwa ya kukataa kununua haki zao!Mafisadi na wala rushwa ni wengi sana hasa kwenye sekta ya serikali,sababu ya ubinafsi wao na ndiyo maana wanafikiria matumbo yao tu!LOH ni aibu tupu!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2012

    Tatizo ni Takukuru wenyewe kwani wao ndio wanaongoza kwa rushwa zaidi hapa tanzania. Mawaziri na makatibu wakuu wengi tu serikalini ni wezi lakini mpaka leo hii, hakuna katibu mkuuu yeyote wala waziri aliyekamatwa. Tunalalamika hata kuandika barua za siri kwenye masanduku ya malalamiko makazini tunafanya, nothing happens. Utakuja kusikia tu mtu hata hafahamiki kakamatwa yule mnayempendekeza kwa malalamishi bado anapeta na anazidi kutukandamiza. Inakuwa kama anaambiwa na Takukuru kuwa jamaa zako wanataka uchukuliwe hatua maana wanakuwa na hasira sana na wafanyakazi wao. Takukuru ifutwe madaraka tupewe sie wenyenwe wananchi kama vile rwanda. There's no point of Takukuru being there wakati they are NOT doing their job properly. Kwa mtaji huu hatutafika kamwe.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2012

    Mchangiaji wa kwanza hii kazi ya kupambana na rushwa si ya akina fulani tu ni yetu sote. Hebu fanya bidii kamatisha pesa za moto huyo msukuma mwenzangu ili na wengine waogope. TANESCO wanatupa shida sana katika kupata huduma zao ikiwemo kuunganishiwa umeme. Tushirikiane sote tutokomeze rushwa.Inawezekana.
    Asante.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2012

    RUSHWA KUUWAWA:

    Ili kutoa mfano kwa vitendo huku watu wakipata Muamko wa kuwa Rushwa ni kitu kibaya sana kwetu kutukwamishia maendeleo, kunyima watu haki na upendeleo,kimetuumiza sana na cha kuepukwa ni muhimu ikafanyika 'FIRING SQUAD' yaani mauaji ya mpigo kwa watu wote waliothibitika ktk WIZI ,UFISADI na RUSHWA!!!

    Kwa kuwa Rushwa ni kitu kibaya sana hakuna jinsi inabidi angalau tuwe majasiri wa kuikataa kwa vitendo kwa kuwaweka wote waliothibitika 'kwa ushahidi na Court Ruling'

    Wawekwe MBELE YA MTUTU WA BUNDUKI NA KIPUGWA RISASI HADHARANI IKIWEZEKANA NDANI YA UWANJA MPYA WA TAIFA HUKU MAELFU YA WANANCHI WAKISHUHUDIA LIVE NA WENGINE MAMILINO WAKIONA TUKIO KWA NJIA YA RUNINGA YA TAIFA TBC !!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2012

    Watanzania wote ni watoaji na wapokeaji Rushwa, tena ni wazi kabisa. Kila ofisi unayokwenda rushwa ipo. Tena unatoa mwenyewe bila ya kuombwa. Kazi yako ikiwa nzuri basi hujali lolote. Ila vijana wetu wa siku hizi ndio walaji rushwa wakubwa. Evidence ni magari yaliyojaa mjini, mtu mshahara tuseme akali akali Millioni moja ananunua gari na kuigharamia mafuta kila siku, alipe chumba kodi, umeme, maji ale chakula milo mitatu na kunywa beer, aende kustarehe kila siku. Hebu fikiria hizo extra anazipata wapi? kama sio kuibia watu au kutoza kidogo soda.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...