Mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya ya namtumbo mkoani Ruvuma Mussa Zunguza akiwa ameshika mwenge wa uhuru mpakakani mwa mikoa ya Ruvuma na Mtwara katika kijiji cha Lumesure wilayani Namnyumbu mara baada ya mwenge huo wa uhuru kumaliza mbio zake mkoani Ruvuma.
Katibu tawala wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,Joseph Kapinga kushoto,akikabidhi mwenge wa uhuru kwa katibu tawala wa wilaya ya namtumbo mkoani humo Ndaki Stephano mara baada ya mwenge wa uhuru kumaliza mbio zake wilayani Songea.
Katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Ndaki Stephano akimkabidhi mwenge wa uhuru kwa katibu tawala wa wilaya ya Tunduru Martin Mlyafu mpakani mwa wilaya hizo katika kiijiji cha Huria Tunduru.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kapt Honest Mwanossa akiweka jiwe la msingi katika zahanati ya kijiji cha mageuzi wilaya ya namtumbo.
Mbunge wa jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma Vita kawawa kushoto akifafanua mambo mbalimbali kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu kapt Honest Mwanossa katika kijiji cha mageuzi wilayani Namtumbo.PICHA NA MUHIDIN AMRI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...