Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa hoteli ya Serena,Seraphin Lusala (kulia) akishirikiana na mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo,kufanya usafi pembezoni mwa barabara ya mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa ilifanyika Mkoani Kilimanjaro.
Meneja Mafunzo wa Hoteli ya Serena,Rhoda Kitilya akisaidiana na baadhi ya wafanyakazi wa hoteli hiyo,kufanya usafi pembezoni mwa barabara ya mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa ilifanyika Mkoani Kilimanjaro.
mbona hatuwaoni huku TANDALE wakifanya usafi?
ReplyDeleteHongera sana Wafanyakazi wa Serena Hoteli. Ingawa pia wapo waajiriwa maalum wa kazi hiyo ya usafi pembezoni mwa barabara, lakini hata hivyo ingependeza zaidi zoezi hilo likawa kama moja wapo ya desturi zetu za kila siku au mara kwa mara kujitolea na kufanya usafi wa aina hiyo humo pembezoni mwa barabara katika mitaa mbali mbali jijini na kwengineko nchini ili kuimarisha, kuboresha na kupendezesha mazingira yetu. Isiwe kungojea mpaka ifike hiyo siku ya maadhimisho ya mazingira ndio watu wazinduke.
ReplyDelete