Waheshimiwa Wanalibeneke,

Naomba kupitia blog zetu maarufu Tanzania naomba mniwasilishie swali langu kwa Watanzania wenzangu kusudi wachangie;

SWAHILI: “KITU GANI AMBACHO KAMA NCHI WATANZANIA TUNAFIKIRI HATUKIFANYI VIZURI?
NA KITU GANI WEWE BINAFSI UKIFANYI VIZURI?”

ENGLISH: “WHAT IS OUR MAJOR MALFUNCTION AS A NATION?”

Namba majibu yote yaelekezwe kwenye sehemu ya maoni. Tuanzie hapo kupata ufumbuzi wa kurekebisha mwelekeo wetu. Katika Tanzania ya sasa blogs zinaweza kuifahamisha, kuielimisha na kuikosoa jamii zaidi kuliko hata radio na TVs.

Mdau
Talent Network

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2012

    Pamoja na kwamba sina jibu kamili la upande wa mwanzo wa swali lako,(kitu tusichofanya kama nchi ) ila nina jibu la swali lako la pili(nisichokifanya mimi binafsi)
    Na kabla sijajibu napenda tu kukupongeza jinsi ulivyokaa na kulifikiria hili ulotuletea. Nakubaliana nawe kwa kupitia blogs na hasa blog hii inayotembelewa na wengi,tunaweza kuelimishana na hata pengine kusaidia kwa kiasi kikubwa kurekebisha mfumo wetu.
    Nikirudi katika kujibu upande wa pili wa swali lako mimi binafsi nisichokifanya ni NAJIKATISHA TAMAA NIONAPO WAKUU WENGI WANAIBA SANA MALI YA NCHI YETU NA NASHINDWA KUSIMAMA KIDETE KULIKEMEA NA KULIPIGIA KELELE KWANI NAJIONA KAMA SIWEZI KUBADILISHA LOLOTE NA HALI HII WANAYO WATANZANIA WENGI NA NI MAKOSA MAKUBWA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 16, 2012

    Simple. We are wasting a lot of our valuable time politing instead of doing productive activities and when i say productive i am not talking about petty shops you see mushrooming every morning or bongo flavor music which every energetic young man whant to do today or machinga business which assist some traders to avade paying taxes but i am talking about business which produce products. If we let politicians convince us that this country is wealthy and one day we will all be healthy without doing what i am saying here the next generation will see even more miserable old people living and dying very poor. Let everybody work and you will see the difference check any literature and you will not find a different answer

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2012

    Kama nchi kwanza nadhani kitu ambocho hatukifanyi vizuri, bado hatujaweza kutumia rasilimali/utajiri wetu vizuri kulijenga taifa letu. Pili tunashindwa kujali mambo si madogo tu bali makubwa pia, kifupi tunapenda kudharau mambo. Mfano mdogo ni ajali za barabarani zinazotokea siku hadi siku nk.

    Mimi kama mimi binafsi kitu ambocho sijaweza kukifanya vizuri ni kuoanisha shahada yangu ya Chuo Kikuu na maisha yangu alisi. Lakini bado naamini kujiajiri mwenyewe na kuwaajiri watanzania wenzangu ndiyo kitu ninachofanyia kazi hivi sasa. Mpaka kieleweke. Nitasema na mradi/biashara yangu iwe mjini au kijijini, hii ni siri yangu mpaka itakapoanza. Kazi kwenu wadau wa mijadala Michachu, safi sana.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 16, 2012

    Kwanza nikupongeze sana mdau kwa kuwa na wazo zuri ambalo kwa michango na mawazo ya wadau wengine itasaidia kujenga Nchi yetu. Mimi sina mengi ingawa nina mengi sana ambayo yananikwaza kila siku, kubwa zaidi ni swala la USHIRIKINA NA UCHAWI TANZANIA, kwa mtazamo wangu watanzania na serikali yetu tuliangalie hili swala kabla hatujapoteza mwelekeo, SHERIA KALI itungwe ili kuwadhibiti watu wanaopractice huo uupuuzi, Adhabu iwe kali sana kama si kunyongwa basi kifungo cha maisha jela. Lingine ni kuhusu madawa ya kulevya jamani yanaua nguvu kazi, SHERIA KALI itungwe na ikiwezekana hao wauzaji adhabu yake iwe jela maisha au kunyongwa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 16, 2012

    Mdau,
    Is this a test or well intended?

    Kwanini wewe usianze kutoa maoni yako kwanza. Twambie ni kitu "wewe" hukifanyi vizuri then tuendelee kutoka hapo.

    Vinginevyo inaonekana kama vile unaandika paper ya chuo kwahiyo unataka tu watu wakupe mawazo.

    Twambie unafikiri wapi tunakosea, au wewe unakosea arafu ndo tujue kinachofuata

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 16, 2012

    As Tanzanians we do not speak up. Even when we are given an opportunity to air our views we prefer to complain after the fact hiding behind others. We have the right of expression - but only a few make use of it.
    In Kiswahili - Watanzania hatusemi hata tunapopewa nafasi. tunapenda tu kulalamika kichini chini hatusimami tukasema pointi yangu hii hapa. Hata tunapoulizwa rasmi je maoni yako nini tuk tayari kukaa kimya halafu baadae, wakati tumeshachelewa tunaanza kulalamika pembeni.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 16, 2012

    Wa-Chinese hawoo wanapeleka Space Craft angani leo. Hatua nyingine ya uzalendo wao wa kupepea bendela yao na kuwaamasisha watoto wao.

    Watanzania kana kwamba atakuja Yesu au Mtume Mohamed ama nabii yeyote atucharaze viboko na kisha kuwasurutisha wabunge wetu waanze kuchangia hoja ya kuanza kujenga teknologia yetu wenyewe na kuanzisha bajeti yake. Yako wapi maendeleo ya gari la Nyumbu? Tuanzie hapa. Wakusanywe ma-engineer kutoka machuoni na mafundi machnics kutoka magereji ya mitaani waanze kazi ya kuifanyia utafiti wa hili gari. Mchanganyiko wa hawa wataalamu kitaeleweka sasa hivi. Hakuna watu smart duniani kama watanzaia, tukiamua tu kila kitu kitakua "bam".

    Mdau mimi binafsi kitu ambacho sikifanyi vizuri ni kwamba napenda mafanikio ya haraka ya kile ninachokifanya over night, I'm a termist I don't think much for long term goals and I think so does Tanzania as a nation. Congrats Mdau for this debate. Ankal please keep this article alive there will be so much to contribute and learn among Tanzanians not only here at home but I believe those who live abroad too.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 16, 2012

    Ankal Michuzi mjadala kama huu utawafikiaje Wabunge wetu Dodoma, wanatakiwa kusoma haya mawazo ya watanzania wanaowawakilisha. Kazi kwako chukua kompyuta yako na blog nzima wabwagie waheshimiwa pale Dodoma na kisha wambie "Kazi kwenu waheshimiwa mimi (wewe) simo". HIi mawazo itajalisha.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 17, 2012

    Kama taifa watanzania hatuthamini haki za wengine. Kuna ubabe na kumjua fulani zaidi ya haki na majukumu. Ukiwa mbabe, kiongozi au mwenye fedha unaweza ukavunja sheria unavyotaka, uko juu ya sheria nani akuguse.

    Mimi binafsi si mzuri katika kujifagilia. PR (too modest) Wenzangu wengi tu wana CV za kuunganisha (sio Watanzania) wanajifagilia utafikiri wameinvent jua. Nimekuwa back bencher kwenye mambo mengi ambayo yako ndani kabisa ya uwezo wangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...