Naibu Waziri Goodluck Medeye akielezea jambo wakati wa mazungumzo yake na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, muda mfupi kabla ya kuungana na wajumbe wengine na kufanya nao mazungumzo ya jumla ambapo walibadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na mkutano wa 22 wa nchi zilizoridhia mkataba wa sheria ya bahari ya umoja wa mataifa, maandalizi ya mkutano wa kimataifa wa maendeleo endelevu na mazingira maarufu kama RIO+ 20 utakaofanyika Rio de Jenairo, Brazil mwezi huu , pamoja na maandalizi ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuja kutetea Andiko la kutaka kuongezewa eneo la ziada la bahari nje ya mail 200 za ukanda kiuchumi wa Bahari. Tanzania imepangiwa kulitetea Andiko hilo mbele ya Makamishna wa kamisheni ya Umoja wa Mataifa inayohusika na mipaka ya Bahari mwezi Agosti mwaka huu.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Asha-Rose Migiro akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye wakati yeye na ujumbe wake walipokaribishwa Ofisini kwa Naibu Katibu Mkuu, Naibu Waziri yuko hapa Umoja wa Mataifa, akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 22 wa Nchi zilizoridhia Mkataba wa Sheria ya Bahari ya Umoja wa Mataifa.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 22 wa Nchi Zilizoridhia Mkataba wa Sheria ya Bahari ya Umoja wa Mataifa ukiwa katika picha ya Pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Asha-Rose Migiro. kutoka kushoto ni Dkt. Justin Seruhere, Kaimu Balozi, Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Bw. Omary Mtunguja, Geophysicist kutoka TPDC, Bw. Abdon Makishe, Hydrophysicist kutoka TPDC, Naibu Waziri, Goodluck Medeye, Naibu Katibu Mkuu wa UM, Asha- Rose Migiro na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi Maria Bilia. Wengine kutoka kulia ni Bw. Kelvin Komba, Geophysicist kutoka TPDC, Bw. Omar Zuber Kaimu Mkurugenzi wa Nishati kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Justo Lyamuya, Hydrographer kutoka Wizara ya Ardhi, Bw. Richard Maridadi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bi. Verediana Mashingia kutoka Wizara ya Ardhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...