BAADHI ya abiria wakidandia lori likiwa katika mwendo katika kijiji Muze,barabara ya Sumbawanga - Mtowisa. barabara hii pamoja na kwamba inapita katika vijiji vilivyopo katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga maarufu kwa kilimo cha mpunga, ufuta na mahindi lakini wakazi wake wanalazimika kusafiri katika magari ya mizigo kwa kuwa hakuna mabasi yanayopita huko kutokana na mindombinu ya barabara kuwa mibovu.
Magari mawili madogo yakipishana kwa taabu sana leo, katika njia panda ya kwenda uwanja wa ndege wa Sumbawanga na kitongoji cha Sumbawanga Asilia katika Manispaa ya Sumbawanga , kipande hiki cha barabara kimechimbika na kufanya 'mabwawa' ya maji ambayo hayajafanyiwa ukarabati kwa muda mrefu hiyo kuhatarisha maisha ya watumiaji wa barabara.
AKINA mama wakiwa wametanda viazi na maboga kando ya barabara ya Sumbawanga - Muze kijijini Muze katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga.
WATOTO wanaosoma Shule ya Awali iliyopo katika Shule ya Msingi Mwenge 'A' mjini Sumbawanga wakinywa uji.chakula mashuleni inasemekana huboresha mahudhurio na uelewa kwa wanafunzi (Picha na Mdau Peti Siyame wa Globu ya Jamii -Sumbawanga.)
Kumbe Sumbawanga kuna maisha bora namna hii? CCM walijitahidi sana. CHADEMA muache kejeli.
ReplyDelete