Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kapteni Honest Mwanossa akichanganya mbolea wakati wa uzinduzi wa shamba la michungwa  kwa kutumia  mbolea vunde kwa kuongeza ubora wa mazao na hifadhi ya mazingira katika kijiji cha Msindo wilaya ya Namtumbo.Shamba hilo lenye ukubwa wa hekari mbili na nusu linamilikiwa na Mzee Venant Haule (mwenye fulana nyekundu).
 

Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa kuingia katika wilaya ya Namtumbo kuanza kazi ya kuhamasisha shughuli za maendeleo ukitokea wilaya ya Songea.Jumla ya miradi  11 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 400 imezinduliwa,imewekewa mawe ya msingi na kufunguliwa. Picha na  Revocatus A.Kassimba - Afisa Habari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2012

    Jamani hii picha ya chini,jamaa alevaa kofia nyekundu sio Ras Makunja huyo? kwani naye kateuliwa katika msafara wa mbio za mwenge?
    Sasa muziki atatupigia nani?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2012

    HUU MWENGE MIMI NILIFIKIRI UMESHAKUFA KUMBE BADO UPO,MWENGE WA OLYMPIC UNAKIMBIZWA UINGEREZA KWA SASA KATIKA MICHEZO HAYA MAMBO YANAELEWEKA KATIKA KULETA MAENDELEO HUU NI UKOMINISTI AMBAO UMEFELI KIASI FULANI SASA IKIWA CCM WANAHITAJI MAGEUZI BASI KWA KUUTUMIA MWENGE HUU NI TATIZO.

    NINA USHAURI WA BURE KWAO NI VIZURI WAKAUPUMZISHA MADHARA YA MWENGE HUU NDIO YANAYOTUSUMBUA SISI WAZEE WA LEO KWANI TULIPOKUWA VIJANA TULIJAZWA ITIKADI ZA KISOSHALISTI NA UKOMUNISTI NDIO MAANA KILA KIONGOZI UNAEMVUMBUA KATIKA CCM LEO MWENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA 40 HUWA HAFAI SASA TUNAWATIA KASUMBA UPYA WATOTO WETU ILI WAENDELEE KUAMINI ITIKADI ZILE ZILE DUNIA YA LEO NI YENYE KUHITAJI MAGEUZI YA KIUCHUMI NA FIKRA ZENYE KUENDELEA 'PROGRESSIVE MIND SET' SAMAHANINI VINGINE VIACHENI VI-EXPIRE.

    MDAU.

    KARIAKOO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...