BAADHI YA WANANCHI WAKISHANGAA BAADA YA FAINES KUZINDULIWA NA MTOTO MWENYE MIAKA KUMI ALIYEKABIDHIWA MIKOBA NA MAMA YAKE
FAINES AKIPAKIWA KATIKA GARI YA POLISI
FAINES ZAWADI-BINTI ALIYEFARIKI KWA MUDA NA KUREJESHWA DUNIANI AKIWA AMESHIKILIWA NA NDUGU ZAK
MJUKUU BATROMEO BRUNO NA BIBI YAKE EVANIA SEPHANGA WAKISHUKA KATIKA GARI LA POLISI BAADA YA KUFIKISHWA KITUO CHA POLISI CHA KATI CHA KIGOMA
Na Pardon Mbwate na
Felister Chubwa, wa Polisi Kigoma
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limefanikiwa kuwaokoa watu watatu waliokuwa wamezingirwa na kundi la wananchi wakitaka kuwaua kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya ushirikina.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma SSP Joseph Konyo, aliwataja watu hao waliokolewa kuwa ni Evania Sephanga(50), mkazi wa wilaya ya Kibondo, Bruno January(46), mkazi wa kijiji cha Nyamhoza na mtoto mmoja mwenye umri wa miaka kumi na mkazi wa kijiji cha Nyamhoza Kigoma mjini ambaye jina lake linahifadhiwa.
Kamanda Konyo amesema kuwa wiki iliyopita majira ya saa tisa mchana, watu hao walizingirwa na kundi hilo kwa madai kuwa walimroga na kumuua msichana mmoja aitwaye Faines Zawadi(20) mkazi wa kijiji hicho cha Nyamhoza ambaye siku moja kabla ya kifo chake alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa na kuwa kama kichaa.
Alisema katika tukio hilo, bibi kizee mmoja ambaye alikuwa mshirika wa kundi la waliodaiwa kuwa wachawi, alifanikiwa kutoroka katika mazingira ya kutatanisha alipojifanya kuwa anakwenda kujisaidia.
Kamanda Konyo amemtaja bibi huyo aliyefanikiwa kutoroka kuwa ni Bibi Editha Dosiyo mkazi wa kijiji hicho ambaye baadaye alipatikana na kuhojiwa kabla ya kukabidhiwa kwa Idara ya ustawi wa jamii baada ya kuonekana kuwa maisha yake yangekuwa hatarini.
Amesema baada ya Polisi kupata taarifa za tukio hilo, walikimbia na kwenda kuwaokoa kutoka katika mikono ya kundi la wananchi lakini wakiwa wameshaadhibiwa kwa kupigwa kiasi.
Habari zinasema kuwa, baadhi ya wananchi walipata taarifa kutoka kwa mtoto aliyeokolewa akisema kuwa baadhi ya watoto waliofariki kijijini hapo, akiwataja (majina tunayahifadhi) alikuwa akiwaona nyumbani kwao nyakati za usiku wakiosha vyombo na baadaye kupewa chakula.
Siku ya tukio hilo, baadhi ya wananchi walisema kuwa kabla ya bibi huyo kutoweka alimnong’oneza jambo mjukuu wake ili amfanyie marehemu ikiwa ni pamoja na kumruka mara saba kisha bibi huyo alitoweka akijifanya anakwenda kujisaidia.
Walisema mara baada ya bibi huyo kutoweka, mtoto huyo wa kiume ambaye ni miongoni mwa waliozingirwa wakitaka kuuawa, alianza kutekeleza maagizo ya bibi huyo na alipomaliza kitendo cha kumruka kwa mara ya saba, msichana yuyo ambaye alikuwa 'mfu' alizinduka na kuomba uji.
Wamesema msichana huyo alipewa uji na kunywa kisha akapelekwa hospitalini ambako hadi sasa hali yake inasemekana kuwa inaendelea vizuri.
Hata hivyo Kamanda Konyo ametoa wito kwa wananchi kuacha kuchukua sheria mkononi na badala yake watoe taarifa Polisi kwa kila jambo wanaloliona kuwa linaweza kuleta uvunjifu wa amani ili hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya wahusika.
Mwezi uliopita watu wawili mke na mume, waliuawa na kundi la watu wenye hasira kisha miili yao kuchomwa kwa moto mkoani Kigoma baada wa kutuhumiwa kuwa walikuwa ni wachawi.



Duh! Hii nchi kwa mazingaombwe ndio yenyewe. Malaria imepanda kichwaani, ohh!kalogwa. Shauriyenu. endeleeni kung'ang'ani hizi imani zenu za karne ya 17. Hao wote wakipewa kazi tu na kuweza kuyamudu maisha yao, hizi imani potovu zitaingia mitini.
ReplyDeleteKazi ipo.
ReplyDeleteDavid V
unadhani kwamba uchawi haupo haata wakipewa kazi hawa ndugu na jamaa zetu za kufanya?
ReplyDeleteserikalini wanarogana kwenye vyama vya siasa wanarogana kwenye timu za mpira wa miguu wanarogan,mwanamke anatafuta mume anakwenda kwa mganga kuroga you name it kila mahali wanaroga unadhani utaisha uchawi.
michuzi naye kajizindika watu wasimlonge na waingi kwa wingi kweny ehii blog yake ha ha ha just kidding man
ninachotaka kusema msijidai wabi shororo bure,bab kubwa mkaona mila potofu hizi hata ulaya na marekani zipo na huko haiti ndo usiseme wee acha tuu
omba mungu yasikupate haya mazinga ombe ukiroka ukarogekwa ndo utakuja juu malaria imepanda kichwani au vipi usiombe mkuu yakufee shauri yako
Nakuunga mkono Anon Fri Jun 01, 10:25:00 PM 2012.
ReplyDeleteIla inasikitisha sana! hata ukisema elimu ndio itakomboa watu lakini wapi? tuzidi kuomba mungu tu yasikukute.
Ni mimi
Mr Nyamaimewahi Kunikabashingoni.
Haya mambo ya kuendekeza uchawi yanarudisha nyuma kila kitu kinachohusiana na maendeleo. Halafu nasikia na ndugu zetu wa ugaibuni nao wanaendekeza. Nasikia Belgium kuna wapopo na Holland kuna kibibi ambao ni the so called waganga. Jamani tutafika kweli? Hii ni karne nyingine hebu tuache hayo.
ReplyDeleteMkereketwa
WEWE UCHAWI UKO SANA TANZANIA, NA USISUBUTU NI NCHI YOTE NDIO UTAMADUNI. WABUNGE, MAWAZIRI , WANAWAKE NDIO USISEME NI SUMU HAO WANAWAROGA SANA WANAUME KWA AJILI YA KUFANIKISHA MAMBO YAO WALA HAWANA KIPIMO CHA KUROGA, NI KUMUOMBA MUNGU YASIKUKUTE WEE ACHA TU. HUKO WEST AFRIKA NCHI KAMA GHANA NA IVORY COAST, NIGERIA, MALI , SENEGAL. GAMBIA HIO YA TANZANIA CHA MTOTO. BASI NIKEKWISHA KUONEA MWANAMKE KAROGA NA KAOLEWA NA MZUNGU HUYO MAMA NI KIPOFU, WALA HAJUI KUSOMA WALA KUANDIKA, MZUNGU KAJIKUTA TU KAMUOA BILA YEYE KUJITAMBUA MPAKA LEO ANAHOJIWA KATIKA VITUO VYA TELEVION AMESHINDWA ELEWA ILIKUWA KAMUOA HUYO MWANAMKE TOKA BENIN
ReplyDeleteWEE ACHA TU.
MDAU EAST LONDON
Wacheza mpira wa kibongo ndio kiama hao bila kulala makaburini mechi haichezwi, hizo sio siri kwa mtanzania, wake wa mawaziri, wanawake wa pwani ndio usiseme balaa tupu.
ReplyDeleteUCHAWI UPO NA UTAENDELEA KUWEPO TU ; NA HAYO MAMBO YAKO KWENYE ASILI ZA KIFAMILIA KAMA MAMA YAKO AU BABA ALIWAHI FANYA USHIRIKINA NA WATOTO HUWA WANAFUATA NATURAL;
USIOMBE UKAKUTANA NAO NI HATARI WANATESA VIBAYA SANA
Michuzi katika mchakato wa kutoa maoni kuhusu KATIBA jamani hili swala la USHIRIKINA NA UCHAWI Liwakilisheni lijadiliwe na iundwe SHERIA KALI kwa wanao PRACTICE MAMBO YA UCHAWI , Nchi haiwezi kwenda kwa mtindo huu maana watu wanaogopa hata kujiletea maendeleo binafsi kisa kuwaogopa hao NYAMAFU VIGAGULA. SERIOUS MZEE na kama inawezekana weka humu KICHWA CHA HABARI WATU WATOE MAONI YAO KUHUSU NINI KIFANYIKE ILI KUPAMBANA NA ROHO INAYOTUMEZA YA MASWALA YA USHIRIKINA TANZANIA. So sad man karne ya 21 watu bado wanamambo yakishenzi namna hii!
ReplyDeleteDavid V toa hoja na wewe nyama imekukaba shingoni acha zako toa ponti. yangu ni haya ,kama kweli wachawi wapo- jamani mrogeni Mkulo arudishe pesa za umma, sasa nyie huo uchawi wenu ni wa kufuata watu masikini tu ??,sijasikia karogwa mhindi, marekani walitoa millioni 25 kwa mtu anayefahamu Saddam Hussein alipo, haya mbona huyo bibi kizee wa Kigoma hakujitokeza na ujinga wake wa so called Uchawi akawatonya Marekani na donge hilo likaenda Kigoma kuchimba visima vya maji. na nyie mnaosema uchawi upo,you are simply good for nothing. Polisi endesheni virungu tu wenyewe watazihama imani zao. Zebedayo mna nasa.
ReplyDeletekweli uchawi upo ila si jambo la kulichukulia uzito maana kwa watu wasio na busara linaweza kurudisha maendeleo nyuma sana hata kugharmiu maisha ya watu.
ReplyDeleteDawa yake ni kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (S.W), kama wewe ni Muumin wa Kiislam soma Alkal za asubuhi na Jioni, usilale mpaka uhakikishe umesoma dua za kulalia, usitoke nyumbani kwako bila kusoma dua ya kutokea nyumbani, usiiingie nyumbani kwako mpaka umesoma dua ya kuingilia ndani, fanya yale Mwenyezi Mungu (S.W) aliyekuamlisha, swali swala tano, usizini, kula vya halali yale yote Mwenyezi Mungu aliyekuambia usiyafanye yaache, udumu kuwa na udhu hiyo ndio tiba ya uchawi. Ukijikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (S.W) Shetani atakukimbia na akikukimbia Shetani Uchawi hautakupata, Inshaallah.
ReplyDeletehuyu anonymous wa sat jun ot at 3.50 am na muunga mkona kwa nini tusiroge watu matajiri lakin kumbuka human psychology huwa anayekukera pale wa karibu yako ndo unaye weza kumroga that how human psychology works upo mkuu ni kweli tusiuendekeze UCHAWI lakini pia tusiukatae kwa sababu serikali yetu yote imetawaliwa na imani hiyo, ukitaka ukuu wa nchi lazima upitiye kwa sangoma bwana wewe acha hizo
ReplyDeletenakuombe mungu yasikukute yakikukuta ndo utajua cha mtema kuni nini ehee, au omba leo waje wakuwangie katika nyumba yako hata ukisoma maandiko yako wanapasua ukuta wewe, usicheze nao lakin pia usiwe muoga sana
omba mungu mkuu wa sat jun 2 at 5;40 yasikukute shauri yako jefanye choka wenzako lami
mdau marekani
Pumba nyingi humu.. We nyamaza omba mungu wako na muamini kwa maana haya mambo yapo.
ReplyDelete