Dotto Mbwana, mfanyakazi wa NMB Muhimbili akigawa vijarida vya NMB Financial Fitness kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili mpango huo ni kwa ajili ya kuwaandaa wanafuzi kupata uelewa wa masuala ya kibenki mashuleni
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtibwa wakijisomea kijarida cha NMB Financial Fitness wakati wafanyakazi wa NMB Turiani walipotembelea shule yao
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili wakisoma kijarida cha NMB Financial Fitness
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili wakisoma kijarida cha NMB Financial Fitness
Meneja wa NMB Muhimbili Janeth Shango akiwasisitizia wanafunzi juu wa kuweka fedha wakiwa na umri mdogo
good job!
ReplyDeleteWatoto kufunzwa kuweka akiba:
ReplyDeleteSasa kwa malezi ya watoto ktk umri mdogo kama huu hatuwezi kuchochoe maadili na tabia mbaya ya udokozi,wizi na tamaa kwa watoto?
Ninachojua ni kuwa kumpatia mtoto Akiba ya baadae ni wajibu kwa wazazi na haki yao watoto kimsingi.
Isipokuwa ktk suala la kuweka akiba ya Mtoto Mzazi anatakiwa ashirikishwe mfano mchakato wa kufungua Akaunti mzazi anahitajika hatua kwa hatua kwa vile Sheria hairuhusu mtoto peke yake amiliki Akaunti isipokuwa namikliki Akaunti chini ya usimamizi wa Mzazi.
Itafaa Vijarida vitolewe kwa minajili ya kuwahamasisha watoto wapeleke Wazazi Majumbani ili kukwahimiza wawawekee akiba kwa kuwafungulia Akaunti.
Ni kazi nzuri isipokuwa kanuni zizingatiwe na badala yake tuamshe mwamko wa Akiba badala ya kuvunja maadili kwa watoto na kuonegeza idadi ya watoto vibaka majumbani.
Nawakilisha!