Mrusi wa Matumla amemkimbia baada ya kuona rekodi yake ni kali. Wawili hao walikuwa wacheze katika mpambano uliopewa jina la “The Rumble on the Mountain” na ulikuwa ushuhudiwe na mcheza sinema maarufu kutoka nchini Marekani Deidre Lorenz ambaye atakuwa anashiriki mbio za Mount Kilimanjaro marathon mjini Moshi tarehe 24 Juni mwaka huu.

Deidre Lorenz anajulikana sana kwa sinema nyingi mojawapo zikiwa The Santorini Blue, Perfect Strangers, The Big Fight na nyingine nyingi. Hata hivyo Deidre Lorenz ataingia mjini Moshi akitokea nyumbani kwake New York , Marekani terehe 21 Juni tayari kikimbia mbio hizo za Mt. Kilimanjaro Marathon.

Bondia huyo wa Urusi Vitaly Shemetov ambaye anajulikana kama “Siberian Tiger” aliingia mitini kiaina baada ya kupelekewa tiketi za ndege ya shirika la Kirusi la Aeroflot yeye na kocha wake. Hii ni mara ya kwanza kwa mpambano wa kimataifa ulioandaliwa kwa pesa nyingi kutofanyika baada ya bondia mmojawapo kuingia mitini kwa woga.

Bondia Rashid Matumla anayejulikana kama Snake Boy ana rekodi ambayo mpaka sasa hakuna bondia yeyote wa Kitanzania aliyeweza kuifikia.

Matumla ameshawahi kuwa bingwa wa Taifa, Afrika Mashariki na Kati, Bara la Afrika, Mabara na Dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi Duniani (WBU). Akiwa chini ja DJB Promotions bondia Rashid Matumla ambaye kwa sasa ndiye Kamishna wa TPBC kanda maalum ya Dar-Es-Salaam alionyesha ubingwa wa hali ya juu.

Hata hivyo Rashid Matumla amepangiwa kupigana na bondia mwingine siku za usoni ili kupooza machungu ya kukimbiwa na Mrusi huyo!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2012

    Tatizo sio kuingia mitini pesa alizo garamiwa zipo wapi? MZ

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 16, 2012

    with all respect to rashid nadhani huyu mrusi alikuwa sio bondia.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2012

    TANZANIA NA ULIMWENGU WA MICHEZO:

    Ni wazi kabisa ya kuwa tuko vizuri katika Masumbwi kuliko Soka!

    Sioni ni kwa sababu gani tunapoteza muda ktk Soka wakati mtaji tunao kama hivi mnaona Matumla anakimbiwa na wapinzani!

    Rashid Matumla 'Jembe' a.k.a 'snake boy' ifanyike jitihada Mrusi asakwe aliko kama ana Mikanda yeyote anyang'anywe na kupewa Snake boy,

    Au siyo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 16, 2012

    Afadhali yake Mrusi amekimbia,

    Dona na Maharage ya Tanzania mchezo?

    Bondia wa Bongo anaandaliwa ugali uliopikwa katika nusu pipa na debe moja la maharage kabla ya kula anapiga pushapu 1,000 kwanza!

    Kamasi zingemtoka baada ya kukumbana na 'ngumi jiwe'

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 17, 2012

    Kama mzungu tu kaangalia record hapo amekosea maanake hiyo ni record ya zamani. Rashid sasa amekwisha na anatakiwa astaafu, hamna lolote tena hapo. Alikuwaga mzuri sana alipokuwa bado kijana lakini sasa sio wakati wake tena

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...