RUKIA ABDALLAH ni mtoto wa miaka miwili anayeishi Wilayani RUANGWA mkoani LINDI aliungua maji ya moto,akapelekwa hospitali ya wilaya RUANGWA ambako alipata huduma ya kwanza na kushauriwa aende NDANDA,NYANGAO au MUHIMBILI.

Wazazi wa RUKIA hawana uwezo kifedha wa kumfikisha mtoto wao katika hospitali hizo,wanaendelea kumuuguza mtoto huyo kienyeji nyumbani kwao na sasa mtoto huyo anatoa harufu kali kwenye kidonda hicho......

Kwa niaba ya Familia Mimi Abdulaziz Ahmeid wa Lindi Press Club na Mwandishi wa Channel ten Mkoa wa Lindi natumia fursa hii kumuombea mtoto huyu msaada ili asaidiwe kupatiwa Matibabu ya Haraka kunusuru Maisha yake.

kwa mawasiliano 

SIMU
O787176221/0716483532............

AU WASILIANA NA LINDI PRESS CLUB ILI KUMFIKIA KIJANA HUYO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2012

    Looh!..Ruangwa nilishafanya kazi miaka kadhaa iliyopita,mitaa ya Nambilanje,Namichiga,Namkonjera,Mkaranga,Mandawa,nk.Mimi nipo nje ya nchi lakini kama mzazi,nimeguswa na huyu mtoto.Bwana Abdul naomba tuwasiliane kwenye hii anuani ya barua pepe;.....'atyini@yahoo.com'

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2012

    Kama michuzi mnaweza irusha hii habari kwenye Television itakuwa vizuri sana ili watu wengi waione na tuweze kumsaidia mtoto huyu.Kama serikali waliweza kutoa MILIONI 10 Kwenye msiba wa msanii. Nadhani kwa huyu mtoto hatashidwa ili tunusuru maisha yake.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 03, 2012

    SERIKALI INAWEZA KUMSAIDIA MTOTO HUYU, JAMANI TUWE NA HURUMA, ILITAKIWA WATOE TU TAARIFA KWA VIONGOZI WA SERIKALI WALIOPO. SIO LAZIMA MPKA WATU WACHANGE. TUNAMTAKIA MTOTO APATE NAFUU MAPEMA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2012

    Watu tujifunze kwa wenzetu Wakenya kufa harambee, palepale kijijini na hilo linaweza kusimamiwa na balozi wa nyumba kumi kumi, badala ya kusubiri mpaka mtoto anuke na michuzi abahatishe kufika katika eneo lako akuone, kama ndo hivi basi tunaweza kupoteza maisha pasipo ulazima.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2012

    Habari Kaka Michuzi!

    Hivi sisi Watanzania tunaishi maisha ya namna gani? Hatujijali! Tunajali sifa na hasa kwenye misiba! watu wanashindana kuchangia misiba na kunywa pombe! Kujirusha kwingi! Jamani mambo mengine Serikali inapaswa kuyafanya bila kuambiwa! Hivi Huduma za Matibabu/Afya kwa mama na mtoto au kwa watu wasio na uwezo hazina kipaumbele kwenye nchi hii? Tunachangia rambirambi Milioni 10 tena Waziri wa Serikali ya Jamhuri anatoa ubani kwa bashasha! tunashindwa kumsaidia mtoto kama huyu mwenye tatizo la kuhitaji matibabu ya kina ili kuokoa maisha yake, siwalaumu hawa Lindi Press Club au Media yoyote ambayo inatoa habari kama hii ya kuhitaji msaada wa kutibiwa lakini Serikali hasa Wizara husika na Afya na Ustawi wa Jamii wako wapi? Au mpaka mtu akifa ndio mnapeleka rambirambi za watu kutumbua na kugombania urithi!!! Viongozi amkeni msingoje kila kitu Mshtuliwe na Vua Gamba Vaa Gwanda!! aibu!!!

    shark_ham@yahoo.co.uk

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...