Ndugu Watanzania na Marafiki,

Familia ya Mung'ong'o ya Palos Hills, Illinois, USA inasikitishwa kutangaza kifo cha mpendwa wao, mume, baba, babu, binamu na mjomba, Gendelimage George Mung'ong'o (pichani), kilitochotokea Jumatano Mei 23, 2012 katika Hospitali ya John Stroger Jr, Chicago, IL.

Mzee Mungongo alipigana vita njema ya imani wakati akipata matibabu ya saratani mpaka kifo chake. Alimjua Yesu na alikuwa rafiki wa Yesu katika maisha yake yote. Furaha yake ya kuambukiza ya Bwana, iliwagusa watu wengi na wengi wao walikuja kumjua Yesu kupitia yeye. Watu wengi walitiwa moyo na waliongozwa katika mambo ya Mungu. Utukufu kwa Mungu.

Mzee Mungongo ameacha mke Martina, watoto wanne, (Lusungu, Kangalage (KCG), Sylvia na Rainald,) wajukuu (Malikia, Myles na Elijah) na wapwa wengi, mama yake (Rosina), dada wawili (Margreth, na Theckla) na kaka mmoja (Patrick).

Mipango ya mazishi imekamilika na Mzee Mung'ong'o atawekwa katika nyumba yake ya milele Jumamosi Juni 9, 2011. Angalia maelezo hapa chini.

MISA YA WAFU NA IBADA YA MAZISHI
Mzee George Mung'ong'o atalazwa kwenye nyumba yake ya milele Jumamosi, Juni 9, 2012.

KUMUAGA MAREHEMU
Mwili wa marehemu utaagwa katika Parokia ya Moyo Mtakatifu, 8245 W. 111th St Palos Hills, IL 60465 kati ya saa 02:00 asubuhi na saa 04:00 asubuhi mida ya kawaida ya kati (CST) Juni 9, 2012.

MISA YA WAFU
Misa ya wafu itasomwa katika Parokia ya Moyo Mtakatifu, 8245 W. 111th St Palos Hills, IL 60465 kutoka saa 04:00 asubuhi hadi saa 05:30 asubuhi mida ya kawaida ya kati (CST) Juni 9, 2012

HUDUMA YA MAZISHI
Huduma za mazishi zitafanyika katika makaburi ya wakatoliki ya ufufuo (Resurrection Catholic Cemetery) 7201 Archer Avenue, Justice, IL 60458 kati ya 06:00 na saa 07:00 mchana mida ya kawaida ya kati (CST)

SHUGHULI BAADA YA MAZISHI
Kuhitimisha matukio ya siku, tutakutana kwa ajili ya kusherehekea maisha ya George Mung'ong'o katika ukumbi mtakaotangaziwa baadae kati ya saa 08:00 mchana na saa 12:00 jioni mida ya kawaida ya kati (CST)

Akaunti imefunguliwa kuchangia gharama za huduma za mazishi, mnatiwa moyo kutoa kilicho bora. Maelezo ya akaunti ni kama ifuatavyo:

Jina la Akaunti: Martina Mungongo
Namba ya Akaunti: 291002179557
Jina la Benki: Bank of America
Routing namba ya benki: karatasi / elektroniki – 081904808
Routing namba ya benki: waya – 026009593
Zip code ya akaunti: 60465

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2012

    Raha ya milele umpe eebwana na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani,milele Ameen. Msiba mzito sana, mpendwa wetu tutakukumbuka kwa busara zako zisizo mfano,ulisimama kama baba yetu, mzee wetu kwa familia nyingi zilizokuzunguka hapa Marekani, kofia zote za busara mungu alikubariki nazo wewe na mke wako, familia yako imejawa na upendo usio kifani. Mipango ya muumba wetu haipingiki na sisi wote tuko safari moja, mwenzetu leo umetangulia nyuma umetuachia utajiri mkubwa wa busara.Poleni sana familia ya Mungongo, mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 02, 2012

    Pole sana Dr. Martina and family

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 02, 2012

    Poleni sana familia ya Mungongo. Msiba wetu wote huu. Mzee wetu ametutoka ametuachia busara nyingi nyingi!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 02, 2012

    RIP Mzee Mng'ong'o.
    Sisi huku Tanzania hususani Kijiji cha Ilembula, Njombe tupo pamoja na familia ya marehemu katika wakati huu mgumu.
    Pole sana Lusungu, Kangalage na wenzenu wote. Muhungilaghe vhonda uho, Pole sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...