Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Bi REGINA Chojo akimkabidhi Mwenge wa uhuru Mkuu wa wilaya ya Liwale,Ephraem Mfinga Mmbaga baada ya kumaliza mbio zake wilayani Nachingwea, Makabidhiano hayo yamefanywa katika kijiji cha Nangano wilayani Liwale Mkoa wa Lindi.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Bi Agness Hokororo(Mb)akikabidhi Risala ya utii kwa kiongozi wa mbio za Mwenge baada ya kukamilisha kazi za wilaya ya Ruangwa
Kiongozi wa Mbio za Mwenge akihutubia wananchi wa Mkoa wa Lindi.
Picha na Habari na Abdulaziz Video Lindi
KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa,capten Honest Mwanossa,amewataka wananchi wa mkoa wa Lindi na Taifa kwa ujumla,kutambua suala la kuchangia mchakato wa kutoa maoni ya katiba si jambo la kisiasa.
Hayo ameyaeleza alipokuwa akizungumza na wananchi wa wilaya ya Nachingwea kwenye makabidhiano ya mwenge wa uhuru yaliyofanywa kati ya wakuu wa wilaya za Nachingwea na Ruangwa,mpakani mwa wilaya hizo juni 12 mwaka huu.
Katen Mwanossa amesema kwamba wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa katiba wakati utakapofika kwa ajili ya maendeleo yao,huku akisisitiza kuwa suala la katiba sio la kisiasa tena.
Aidha akasema kama wananchi watashiriki vema katika zoezi hilo,ambalo ni muhimu litasaidia kuweka misingi ua utawala bora na kupunguza malalamiko yasiyokuwa ya msingi pamoja na migongano miongoni mwa jamii yetu.
Pia amewataka pia wananchi wa mkoa huo kuchukia na kuikataa rushwa kwani imekuwa ikikatisha tama katika kuchangia maendeleo yao na kuichukia serikali iliyopo madarakani kwamba imekuwa ikiwakumbatia wala rushwa.
Kapteni Mwanossa amewataka pia watendaji wa serikali kuwa waadilifu na kuacha tabia ya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wateja ambao wanahitaji huduma kutoka kwao.
Alisema hali ya vitendo vya rushwa nchini imezidi kuwa mbaya kiasi kwamba wananchi wamekosa imani na viongozi wa serikali wakiwemo na baadhi ya watendaji wanaohudumu.
Kiongozi huyo akasema kutokana na kukosa kwa uwadilifu huokunawakatisha tama wananchi kujiingiza kwenye miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao.
Nae,mkuu mkuu wa wilaya hiyo ya Nachingwea, Rejina Chonjo alisema mwenge huo wa uhuru umeweza kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo,ikiwemo ya elimu,afya na maghara yenye thamani ya sh,174,830,450/-.

Chonjo alifafanua kwa kusema sh,130.0 fedha kutoka serikali kuu,Sh,3.0 zimetolewa na halmashauri ya wilaya, Sh,15.0 milioni ni michango binafsi na Sh,26.5 ni michango kutoka jamii.
Pia alisema kwamba miradi hiyo ni ujenzi wa nyumba za walimu,ujenzi wa maghara,ofisi za watendaji wa kata,madarasa,vyoo na ukarabati wa wodi ya wagonjwa.

Interesting! Kabla ya kuja kwa waarabu Zanzibar, Lindi ndipo ilipokuwa makao makuu ya the Zenj Empire ambayo ilijumuisha visiwa vya Zanzibar and Pemba, enzi hizo za karne ya 15/16.
ReplyDeleteZenj ina maanisha "the land of Black people" - waafrika weusi walishafika huko Unguja na Pemba hata kabla waarabu hwajajua kutengeneza mashua!!
Halafu leo hii kuna wapuuzi Unguja wanadai eti mlengo wao mkubwa ni kwa waarabu kumbe waarabu wamekuja Unguja juzi juzi tuu katika karne ya 19!
Uamsho bwana, taabu kweli kweli!!