Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Bi REGINA Chojo akimkabidhi Mwenge wa uhuru Mkuu wa wilaya ya Liwale,Ephraem Mfinga Mmbaga baada ya kumaliza mbio zake wilayani Nachingwea, Makabidhiano hayo yamefanywa katika kijiji cha Nangano wilayani Liwale Mkoa wa Lindi.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Bi Agness Hokororo(Mb)akikabidhi  Risala ya utii kwa kiongozi wa mbio za Mwenge baada ya kukamilisha  kazi za wilaya ya Ruangwa
Kiongozi wa Mbio za Mwenge akihutubia wananchi wa Mkoa wa Lindi.

Picha na Habari na Abdulaziz Video Lindi

KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa,capten Honest  Mwanossa,amewataka wananchi wa mkoa wa Lindi na Taifa kwa  ujumla,kutambua suala la kuchangia mchakato wa kutoa maoni ya  katiba  si jambo  la kisiasa.

Hayo ameyaeleza alipokuwa akizungumza na wananchi wa wilaya ya
  Nachingwea kwenye makabidhiano ya mwenge wa uhuru yaliyofanywa kati ya  wakuu wa wilaya za Nachingwea na Ruangwa,mpakani mwa wilaya hizo juni  12 mwaka huu.

Katen Mwanossa amesema kwamba wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi
  katika mchakato wa katiba wakati utakapofika kwa ajili ya maendeleo  yao,huku akisisitiza kuwa suala la katiba sio la kisiasa tena.

Aidha akasema kama wananchi watashiriki vema katika zoezi hilo,ambalo
  ni muhimu litasaidia kuweka misingi ua utawala bora na kupunguza  malalamiko yasiyokuwa ya msingi pamoja na migongano miongoni mwa jamii  yetu.

Pia amewataka pia wananchi wa mkoa huo kuchukia na kuikataa rushwa
  kwani imekuwa ikikatisha tama katika kuchangia maendeleo yao na kuichukia serikali iliyopo madarakani kwamba imekuwa ikiwakumbatia wala rushwa.

Kapteni Mwanossa amewataka pia watendaji wa serikali kuwa waadilifu na kuacha tabia ya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wateja ambao wanahitaji huduma kutoka kwao.


Alisema hali ya vitendo vya rushwa nchini imezidi kuwa mbaya kiasi
kwamba wananchi wamekosa imani na viongozi wa serikali wakiwemo na baadhi ya watendaji wanaohudumu.

Kiongozi huyo akasema kutokana na kukosa kwa uwadilifu
huokunawakatisha tama wananchi kujiingiza kwenye miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao.

Nae,mkuu mkuu wa wilaya hiyo ya Nachingwea, Rejina Chonjo alisema mwenge huo wa uhuru umeweza kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo,ikiwemo ya elimu,afya na maghara yenye thamani ya sh,174,830,450/-.

Chonjo alifafanua kwa kusema sh,130.0 fedha kutoka serikali kuu,Sh,3.0 zimetolewa na halmashauri ya wilaya, Sh,15.0 milioni ni michango binafsi na Sh,26.5 ni michango kutoka jamii.

Pia alisema kwamba miradi hiyo ni ujenzi wa nyumba za walimu,ujenzi wa
maghara,ofisi za watendaji wa kata,madarasa,vyoo na ukarabati wa wodi ya wagonjwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2012

    Interesting! Kabla ya kuja kwa waarabu Zanzibar, Lindi ndipo ilipokuwa makao makuu ya the Zenj Empire ambayo ilijumuisha visiwa vya Zanzibar and Pemba, enzi hizo za karne ya 15/16.

    Zenj ina maanisha "the land of Black people" - waafrika weusi walishafika huko Unguja na Pemba hata kabla waarabu hwajajua kutengeneza mashua!!

    Halafu leo hii kuna wapuuzi Unguja wanadai eti mlengo wao mkubwa ni kwa waarabu kumbe waarabu wamekuja Unguja juzi juzi tuu katika karne ya 19!

    Uamsho bwana, taabu kweli kweli!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...