Mkuu wa mkoa wa Dar es Salam Saidi Meck Sadik (kulia) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bi. Tatu Saidi Mussa leo jijini Dar es Salaam . Mwenge wa Uhuru umewasili jijini Dar es Salaam ukitokea Mkoa wa Kusini Pemba.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akiahidi mbele ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadik kuupokea Mwenge wa Uhuru na kuukimbiza katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ambapo miradi 11 itafunguliwa na kuwekewa mawe ya msingi.
Askari kutoka jeshi la Polisi wakiimarisha ulinzi wakati wa sherehe za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
Wakimbiza Mwenge kitaifa wakiongozwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Capt. Ernest Mwanossa (wa kwanza mbele) wakianza safari kuelekea maeneo mbalimbali ya wilaya ya Temeke leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam waliojitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo.
Vijana wa halaiki kutoka wilaya ya Temeke wakiimba wimbo maalum wa Mwenge wakati wa mapokezi leo jijini Dar es Salaam.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 25, 2012

    akina ras makunja wanavituko kweli jamani sasa mwenge nao wanauvalia miwani,na kuuzunguka utafikiria mali yao!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2012

    Hivi halaiki si ina maana ya umati? Vijana wa halaiki ina maana gani?y

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...