Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Goodluck Ole Medeye (Mb) akijiandaa kuchangia majadiliano ya Mkutano wa 22 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Sheria ya Bahari ya Umoja wa Mataifa ( UNClOS) Mkutano huu wa Wiki Moja unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, na Mhe Medeye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo, ambao pia utaadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa mkataba huo unaosimamia masuala yote yanayohusu bahari na raslimali zake. Mkataba huo ulianzishwa mwaka 1982 na umekwisha kuridhiwa na nchi 162. katika mazungumzo yake. Mhe Naibu Waziri alielezea wasiwasi wake wa muda mrefu unaotumika katika kuhakiki, kupitia, kuridhia na kutoa mapendekezo ya madai yanayowasilishwa na nchi wanachama zikiomba kuongezewa mipaka ya Bahari. Tanzania ni kati ya nchi 59 ambazo tayari zimewasilisha Dai hilo, Dai ambao liliwasilishwa na waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Anna Tibaijuka ( Mb) katika tukio la kihistoria lililofanyika mwezi Januari mwaka huu. Aliyekaa nyuma ya waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizata hiyo, Mhe. Maria Bilia.
Mhe. Naibu Waziri akiwa na Bw. Nii Alloty Odunton Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kimataifa ya Chini ya Bahari (Seabed Authority), muda mfupi kabla ya ufunguzi wa mkutano wa 22 wa Mkataba wa Sheria ya Bahari ya Umoja wa Mataifa, kushoto ni Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Dkt. Justin Seruhele.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2012

    michuzi sasa wa tatu katika picha mbona hujamtaja jina lake tumjue mkuu umewataja watu wawili tu wakati wako watu watatu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...